Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,998
- 144,329
Wakati tukiwa tunashangazwa na kuumizwa na usaliti unaofanywa na baadhi ya wanasiasa wetu, binafsi naanza kupata mashaka kuwa huenda kuna rushwa kubwa inatumika kuwarubuni wanasiasa hawa mpaka kufikia hatua ya kusaliti wananchi wao na kusaliti msimamo yao.
Inawezekana wanapokea mlungula mrefu kisha na wao wanaugawa kwa walio chini yao na kwa vijana wachache wa kuwatetea mitandaoni na kwenye media. Bila shaka mlungula wanaotanguliziwa ndio unawafanya wakubali kubadili msimamo yao.
Kwa mtazamo wangu,maamuzi ya hawa wanasiasa yanahitaji kuundiwa Tume za Uchunguzi, Tume zinaweza kuja na matokeo ya kushangaza kabisa na kutuacha midomo wazi.
Tungekuwa na taasisi huru, ni wazi zingeanza kuchunguza mambo haya ili kuona kama kuna element za rushwa katika haya yanayoendelea.
Anyway, wao waendelee ila kama kuna mchezo machafu unaendelea, basi ipo siku ukweli utajulikana.