Inawezekana kuna Grand Corruption nyuma ya maamuzi haya ya wanasiasa wetu

Utofauti wake ni upi?

Utasema magu anabana wapinzani,

Sasa kama kipindi cha siasa ngumu mnakuwa softi bado kuna upinzani hapo?

Sio kwamba Magu anawabana wapinzani bali anatumia madaraka yake vibaya kuhujumu wapinzani wa kweli. Cdm ni chama cha siasa na sio kikundi cha kigaidi. Ili cdm waweze kufanya siasa chini ya rais huyu kama maelezo yako yalivyo, labda iingie msituni.
 
Sahihi kabisa kaka.
Toka limeanza sekeseke la Wapinzani kuhamia CCM, Upinzani walikuwa wanafanya kosa kubwa kuuza utetezi kuwa wamenunuliwa. Hii ilikuwa inawajengea taswira ya kutoaminiwa na wananchi. Kama katibu mkuu wa chama ananunuliwa, nani wa kumuamini? Huu mkakati magufuli amefanikiwa sana.
Kama amefanikiwa nguvu yote iliyotumika kwenye uchaguzi mkuu ilikuwa ya nini?
 
Kodi zetu za trillions zinatumika vibaya sana kuwanunua wanasiasa malaya malaya ili kuhakikisha huyo anayejiita mwendawazimu anaendelea kuwepo madarakani kwa njia za haramu.

Siku ya jana niliweka bandiko hapa nikionyesha wasiwasi wangu kuwa huenda kuna grand corruption ilionyuma ya usaliti huu wa wanasiasa unaoendelea. Nakumbuka kuna watu humu walinipinga sana kwani wengi wana mtazamo kuwa rushwa ya vyeo na madaraka pekee ndio inawashawishi huku MATAGA wao wakioni mimi kama mzushi au naongea jambo ambalo halipo.

Leo hii nashukuru yule whistleblower maarufu kule twitter kaibua tuhuma hizo na kwenda mbali kwa kuonyesha nia ya kuwaanika wahusika huku akisema liwalo na liwe.

Nashukuru pia kaweka wazi kuwa aliwasaidia CHADEMA kwa kuwapa taarifa, taarifa iliyopelekea baadhii ya watu kuondolewa kwenye kampeni za Lissu na sasa anakusudia kuwaanika wanasiasa wote wa upinzani waliohusika katika tuhuma hiyo ya kupokea mlungula na kusaliti wananchi.

Tusubiri.
 
Chadema mtalia weee lakini mwisho mtachoka. Mambo ya ACT- wazalendo hayawahusu, pambaneni na ya kwenu tu. Hamkuwa na muungano wo wote unaotambulika kisheria na ACT katika hizo kampeni zenu za kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020. Endeleeni kukiua chama chenu kwa kuamini hao vibaraka wa mabeberu walioko lockdown ughaibuni.
 
Yule hajawahi kuongopa .. akimwaga hiyo mboga na ugali msisahau kunitag
Ushasahau alivyoongopa kuhusu kifo cha Jiwe? Vipi kuhusu "tallying centre" wakati wa uchaguzi? Sema tu mnapenda umbeya na mnadanganyika kirahisi
 
Serikali yetu inafanya kazi kwa philosophy ya DOUBLE STANDARD & DOUBLE JEOPARDY, tena inafanya kazi kwa kutumia philosophy hizo kwa WELEDI wa hali ya juu kabisa.

DOUBLE STANDARD

Serikali inapiga kelele na kujigamba kwamba inapambana na rushwa/ufisadi kwa kiwango cha lami. Na inawawajibisha wahalifu hao kisawasawa mbele ya mahakama. Na imeanzisha MAHAKAMA YA MAFISADI.

Ila serikali hio hio ikitumia RUSHWA, UFISADI AU UTEKAJI dhidi ya wanasiasa wa upinzani au raia, sio kosa. Ila wanasiasa wa upinzani au raia akitumia hayo maswala ni kosa, na atakamatwa haraka sana, atatangazwa katika vyombo vyote vya habari sambamba na kufunguliwa mashtaka (Yasio na dhamana).

Kwa ufupi, kwetu ni kosa ila kwao sio kosa.

DOUBLE JEOPARDY

Mahakama inasema sheria hairuhusu mtu kushtakiwa au kuadhibiwa MARA MBILI KWA KOSA MOJA hata kama ametenda kosa hilo makusudi. Maandiko ya sheria pia yanasema hivo.

Ila kwa serikali hii raia/kampuni/wafanyabiashara wana adhibiwa zaidi hata ya mara 10 kwa kosa moja alilofanya (Hata kama sio makusudi), na baada ya adhabu hizo anafilisiwa kila kitu alichokua nacho, na bado serikali inaona haitoshi. Wengine huadhibiwa wao sambamba na wanaofanya nao biashara au mpaka familia (Kuna watu wametenda kosa ila adhabu inashuka mpaka kwa mke na watoto).

Kosa moja unaburuzwa MAHAKAMANI, na bado wanaona haitoshi unatumiwa TRA, POLICE, DC, MKURGENZI, DPP, WATU WASIOJULIKANA na wakati mwingine mpaka WAZIRI.

Serikali hii inaweza ikaongoza Afrika kwa uvunjifu wa Sheria na Katiba. Pamoja na kuinajisi heshima ya taifa letu iliochukua zaidi ya Miaka 59 kuitengeneza.
Jaanga hili alituletea mkapa bila yeye wala tusingekua na mwenyeki wa kijiji anaitwa jiwe never
 
Subiri muda mchache tuuuu na Chadema itawaruhusu akina Halima kuwa wabunge. Amka ndugu yangu kelele zako hazitawanyima wao kunywa maji. Watch this space.
 
Wakati tukiwa tunashangazwa na kuumizwa na usaliti unaofanywa na baadhi ya wanasiasa wetu, binafsi naanza kupata mashaka kuwa huenda kuna rushwa kubwa inatumika kuwarubuni wanasiasa hawa mpaka kufikia hatua ya kusaliti wananchi wao na kusaliti msimamo yao.

Inawezekana wanapokea mlungula mrefu kisha na wao wanaugawa kwa walio chini yao na kwa vijana wachache wa kuwatetea mitandaoni na kwenye media.Bila shaka mlungula wanaotanguliziwa ndio unawafanya wakubali kubadili msimamo yao.

Kwa mtazamo wangu,maamuzi ya hawa wanasiasa yanahitaji kuundiwa Tume za uchunguzi, Tume zinaweza kuja na matokeo ya kushangaza kabisa na kutuacha midomo wazi.

Tungekuwa na taasisi huru, ni wazi zingeanza kuchunguza mambo haya ili kuona kama kuna element za rushwa katika haya yanayoendelea.

Anyway, wao waendelee ila kama kuna mchezo machafu unaendelea,basi ipo siku ukweli utajulikana.
Inatakiwa TAKUKURU wakuhoji maana huwezi kila siku unalalamika na kuzusha kuhusu RUSHWA wakati wewe si mtoaji au mla rushwa.
 
Wakati tukiwa tunashangazwa na kuumizwa na usaliti unaofanywa na baadhi ya wanasiasa wetu, binafsi naanza kupata mashaka kuwa huenda kuna rushwa kubwa inatumika kuwarubuni wanasiasa hawa mpaka kufikia hatua ya kusaliti wananchi wao na kusaliti msimamo yao.

Inawezekana wanapokea mlungula mrefu kisha na wao wanaugawa kwa walio chini yao na kwa vijana wachache wa kuwatetea mitandaoni na kwenye media.Bila shaka mlungula wanaotanguliziwa ndio unawafanya wakubali kubadili msimamo yao.

Kwa mtazamo wangu,maamuzi ya hawa wanasiasa yanahitaji kuundiwa Tume za uchunguzi, Tume zinaweza kuja na matokeo ya kushangaza kabisa na kutuacha midomo wazi.

Tungekuwa na taasisi huru, ni wazi zingeanza kuchunguza mambo haya ili kuona kama kuna element za rushwa katika haya yanayoendelea.

Anyway, wao waendelee ila kama kuna mchezo machafu unaendelea,basi ipo siku ukweli utajulikana.
Watanzania, watanganyika na wazanzibar wanakatishwa tamaa na baadhi ya wanasiasa na maamuzi yao, hivyo wanaamua kuachana na mambo ya kufatilia Siasa!

Niwakumbushe tu ndugu zangu, sukari tunayokorogea Hot beverage ni siasa, mafuta tunayoweka kwenye automobile ni siasa, beer na condom tunazotumia ni siasa!

Tusiache, tuendelee kujadili SIASA, siasa ni maisha.
 
Ni kipindi kifupi sana tumeshuhudia MATUKIO ya kujichanganya kihamnazo....

Kila nikiiangalia ile VIDEO ya dada Hallima Mdee anapiga mayowe pale kituoni akituhumu kupatikana kwa Yale makaratasi....jasho lilivyokuwa linamtiririka....paji la uso lilivyokuwa linaonesha kuwa ana usingizi wa wiki nzima....🤣

Matokeo akayakataa....Leo amekwenda kuyakubalia BUNGENI....🤣

Nikamuangalia Nassor Mazrui katika PRESS yake....akirudia maneno "sijui kama Niko katika cabinet..nikiwepo...ama nisipokuwepo...nimeshawasamehe...".

Sasa hawa wanasiasa wa UPINZANI wao huwa wana madesk yao ya SAYANSI YA SIASA....wanashindwaje kuproject hali itakavyokuwa...yaani kwanini wawaingize WAFUASI WAO KWENYE TABU...ilihali wanajua YATAKAYOTOKEA....

Kwa mfano Zitto na ACT waliwataka WAFUASI WAO waende pale UBUNGO kwa ajili ya maandamano ya amani...najaribu kufikiri...iwapo WAFUASI wangeandamana na KUKATOKEA mgogoro na madhara MAKUBWA juu yao...halafu leo WANAJIUNGA NA SUK kwa moyo MMOJA....🤣🤣

Kweli MAENDELEO HAYANA VYAMA.
Ukikumbuka haya maneno...

"REMEMBER YOU GOT A FAMILY TO FEED NOT A COMMUNITY TO IMPRESS"

Basi utajikita katika kufanya mambo yako na kuachana kabisa na siasa za kibongo. Kila mtu anahangaika na maisha yake hakuna mtu anapigania maisha yako ndg mjumbe.
 
Wakati tukiwa tunashangazwa na kuumizwa na usaliti unaofanywa na baadhi ya wanasiasa wetu, binafsi naanza kupata mashaka kuwa huenda kuna rushwa kubwa inatumika kuwarubuni wanasiasa hawa mpaka kufikia hatua ya kusaliti wananchi wao na kusaliti msimamo yao.

Inawezekana wanapokea mlungula mrefu kisha na wao wanaugawa kwa walio chini yao na kwa vijana wachache wa kuwatetea mitandaoni na kwenye media.Bila shaka mlungula wanaotanguliziwa ndio unawafanya wakubali kubadili msimamo yao.

Kwa mtazamo wangu,maamuzi ya hawa wanasiasa yanahitaji kuundiwa Tume za uchunguzi, Tume zinaweza kuja na matokeo ya kushangaza kabisa na kutuacha midomo wazi.

Tungekuwa na taasisi huru, ni wazi zingeanza kuchunguza mambo haya ili kuona kama kuna element za rushwa katika haya yanayoendelea.

Anyway, wao waendelee ila kama kuna mchezo machafu unaendelea,basi ipo siku ukweli utajulikana.
Mkuu wanasiasa hawepewi cash mbali huwa wanapewa ahadi na kuakikishiwa maslahi yao na familia zao. Over
 
Back
Top Bottom