Inawezekana kuna Grand Corruption nyuma ya maamuzi haya ya wanasiasa wetu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,928
2,000
Wakati tukiwa tunashangazwa na kuumizwa na usaliti unaofanywa na baadhi ya wanasiasa wetu, binafsi naanza kupata mashaka kuwa huenda kuna rushwa kubwa inatumika kuwarubuni wanasiasa hawa mpaka kufikia hatua ya kusaliti wananchi wao na kusaliti msimamo yao.

Inawezekana wanapokea mlungula mrefu kisha na wao wanaugawa kwa walio chini yao na kwa vijana wachache wa kuwatetea mitandaoni na kwenye media. Bila shaka mlungula wanaotanguliziwa ndio unawafanya wakubali kubadili msimamo yao.

Kwa mtazamo wangu,maamuzi ya hawa wanasiasa yanahitaji kuundiwa Tume za Uchunguzi, Tume zinaweza kuja na matokeo ya kushangaza kabisa na kutuacha midomo wazi.

Tungekuwa na taasisi huru, ni wazi zingeanza kuchunguza mambo haya ili kuona kama kuna element za rushwa katika haya yanayoendelea.

Anyway, wao waendelee ila kama kuna mchezo machafu unaendelea, basi ipo siku ukweli utajulikana.
 

Lee

JF-Expert Member
Jul 31, 2013
39,012
2,000
Mkuu lakini wanasiasa wengi ile miaka mitano wanakuwa wanajiona wao ndo wao sasa itokee ghafla miaka mitano imeisha alafu pesa zote ziliishia kwenye v8 na luxuries akifikiria miaka mitano anasota benchiii hana cha kufanya ,hana biashara hayuko kwenye mfumo ni rahisi sana kufanya tunayoyaona sana ...kuna ule mda ambao wenzako mnaagana kila mtu nyumbani kwake hapo familia inakuangaliaa wewe sio wewe uingalie familia 😂
 

Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,739
2,000
Sijawahi waamini wale wenye maneno kama, ndani ya saa48 nitakuwa waziri mkuu wala niguse ninuke au yule mpenzi wa Mungu kwa sababu ya kusema ukweli au hatufanyi uhanithi safari hii!

Wote kwangu ni waigizaji!
Na uwezekano wa kulipana ili maigizo yanoge yawezekana kabisa hilo lipo.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,634
2,000
Mkuu unasema wakiitisha maandamano, kwani wakati wao wanaitisha hayo maandamano wanakuwa wako wapi ili tujue wamekamatwa wakiwa kwenye maandamano. Huko kwenye hiyo serikali wanayokwenda kuelewana ni kura za wananchi. Basi ngoja tuhamasishane kutokupiga kura ili tusipoteze maisha yetu, ili tuone kama wataitwa kwenye hizo serikali waelewane. Jukumu letu ni kupiga Kura na hilo tumeifanya vyema, kuandamana ni kujitoa muhanga ambao hata wao hawathubutu.
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
7,822
2,000
🤣🤣

Inawezekana pia wala hakuna BRIBERY nyuma yake....

Bali tabia yetu waafrika....

Hivi kuna kazi gani ya kuhudumia umma humu afrika mtu anaweza kukunja kiinua mgongo karibia milioni 300 baada ya miaka 5 tu?!!

Kumbuka connections ambazo anakuwa amezitengeneza....

Ingekuwa mishahara na marupurupu yao ni ya kawaida Wala usingeona hayo ya kututaka TUANDAMANE kwa nguvu kwa ajili YAO......
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
7,822
2,000
Ni kipindi kifupi sana tumeshuhudia MATUKIO ya kujichanganya kihamnazo....

Kila nikiiangalia ile VIDEO ya dada Halima Mdee anapiga mayowe pale kituoni akituhumu kupatikana kwa Yale makaratasi....jasho lilivyokuwa linamtiririka....paji la uso lilivyokuwa linaonesha kuwa ana usingizi wa wiki nzima....🤣

Matokeo akayakataa....Leo amekwenda kuyakubalia BUNGENI....🤣

Nikamuangalia Nassor Mazrui katika PRESS yake....akirudia maneno "sijui kama Niko katika cabinet..nikiwepo...ama nisipokuwepo...nimeshawasamehe...".

Sasa hawa wanasiasa wa UPINZANI wao huwa wana madesk yao ya SAYANSI YA SIASA....wanashindwaje kuproject hali itakavyokuwa...yaani kwanini wawaingize WAFUASI WAO KWENYE TABU...ilihali wanajua YATAKAYOTOKEA....

Kwa mfano Zitto na ACT waliwataka WAFUASI WAO waende pale UBUNGO kwa ajili ya maandamano ya amani...najaribu kufikiri...iwapo WAFUASI wangeandamana na KUKATOKEA mgogoro na madhara MAKUBWA juu yao...halafu leo WANAJIUNGA NA SUK kwa moyo MMOJA....🤣🤣


Kweli MAENDELEO HAYANA VYAMA.
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
10,924
2,000
Kujiunga na hiyo serikali ni kuua hatima yao. Wasitegemee tena kupata kura zetu kwa maamuzi haya.
Waliunga mkono juhudi 2010. Hatima yao ilikufa? Nop. Wakasusa 2015. Hatima yao ilikufa? Wangesusa tena 2020 ndio mngewasahau kabisa

Kwa Zanzibar kura yako doesn’t count by the way na kibaya zaidi mnapiga kura huku mkijua 100% nini watafanya
 

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
1,140
2,000
Ninachojua mimi au nilichokariri mimi na nitaendelea kusema kila nipatapo wasaa ni kuwa...

Hawa wanasiasa sio wa kuwaamini hata mmoja, lao moja wote hao na hapo anayepoteza muda ni shabiki/mwananchi wa kawaida tu

Si wao tu bali hawa watu maarufu maarufu wengi kama sio wote duniani lao ni moja na wanayapangilia/ wameyapangilia tayari yale yote mnayowaona wanayafanya japo kuna mengine ni kweli yanajitokeza tu coincidentally kutokana na nguvu ya natural.

Unaweza kuona kama nabwabwaja ila siku moja unaweza pia kuona niliandika ukweli... eti lissu wasielewane na magufuli au ccm iwe adui na CHADEMA au mufti dhidi ya pengo au kwamba rihanna na Chris Brown wanagombana mpaka wakabreak up au diamond na wema/zari

Hizo ni circles tu na kama ni sinema basi hizo ni series tu zinazoendelea
"Dunia ina wengi ila wanaoifaidi ni wachache sana" au "dunia ni ya wengi ila wachache wenye kuijua"
 

Mzee Kigogo

JF-Expert Member
Jun 3, 2018
4,583
2,000
Kujiunga na hiyo serikali ni kuua hatima yao. Wasitegemee tena kupata kura zetu kwa maamuzi haya.
Hata wakipata kura zetu haziwasaidii kwa sababu hawatangazwi na pia sisi wananchi hatujui thamani ya kura zetu, ndio maana hata uchaguzi ukivurugwa tunachukulia poa tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom