reggie8219
Member
- Jun 5, 2014
- 14
- 4
Nimekua nikiuliza swali hili mara nyingi kwa watu mbalimbali. Kati ya majibu mengi, wengi wamekua wakisema kwamba unapoanza kumtaka rafiki yako wa siku nyingi kimapenzi ni sawa na kutaka urafiki uvunjike na mkosane kimoja. Mnapokua wapenzi baada ya kutoka kwenye urafiki wa siku nyingi, mnaanza ingia kwenye mifarakano ambayo inasababisha mkosane kimoja na kuvunja kabisa urafiki wenu. Je ni kweli? Na ni kwa njia gani utamwelewesha rafiki yako wa siku nyingi kwamba umempenda kimapenzi bila kukosana? Na mkishakubaliana kuanza mapenzi, nini mfanye kuepuka mifarakano inayoweza kuwakosanisha kimoja?