Inawezekana kuitishwa Poo ili mambo ya msingi yawekwe sawa

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,823
35,828
Mabibi na mabwana kwa hakika hakuna aliye mkuu ila Allah mwenyewe. Sifa na utukufu wote na vimrejee yeye.

Ama kweli kuishi kwingi ni kuona mengi. Dunia inakwenda kwa kasi kiasi si haba kuwapa ushauri hata chama kongwe aka baba lao - Chama cha Mapinduzi.

Bandugu ni wazi kuwa kwenye chaguzi hizi mambo mengi yamekuwa yakienda fyongo. Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi.

Hapa tulipo kabla ya lolote kuharibika zaidi ilikuwa muhimu kuitisha "pooo."

Jamani si lazima hadi watoto wadogo waone!

Kiutu uzima inawezekana tu kuitishwa poo ili kwanza mambo ya msingi yakawekwa sawa. Twende kwa wananchi kwa haki bila kuhujumiana.

Nchi hii ni yetu sote na kidole kimoja hakivunji chawa.

Naambiwa kutokea kanda pendwa halipo neno jema kama hili: Tuhoye!

Kwa Kitaliano: Rajunah! Au kwa kiswahili: Maridhiano!

Uchaguzi 2020 - Mizengwe mizengwe ya nini Uchaguzi Mkuu?
 
Kiutu uzima inawezekana tu kuitishwa poo ili kwanza mambo ya msingi yakawekwa sawa. Twende kwa wananchi kwa haki bila kuhujumiana.

Ni kwa dhati kabisa upinzani unapenda uwanja sawa wa ushindani.

Ni hilo tu na bado maridhiano yanaweza kufikiwa.
 
Ni kwa dhati kabisa upinzani unapenda uwanja sawa wa ushindani.

Ni hilo tu na bado maridhiano yanaweza kufikiwa.
Kikubwa taratibu zisikiukwe na sheria zisivunjwe...mshindi ashinde kwa haki..na mshindwa ashindwe kwa haki
 
Kikubwa taratibu zisikiukwe na sheria zisivunjwe...mshindi ashinde kwa haki..na mshindwa ashindwe kwa haki

Kwa hakika hakuna hitaji la msingi kama uliloliweka hapo. Na hilo ndilo hitaji la kila mwungwana pasipo na kujali chama.
 
Sote tu wamoja. Pooo! Ni sehemu ya mchezo.

Kuhujumiana si lazima.

Ieleweke kuhujumiana hakuna hati miliki ya mtu, kikundi wala chama fulani.

Tunajenga nyumba moja.
 
Sote tu wamoja. Pooo! Ni sehemu ya mchezo.

Kuhujumiana si lazima.

Ieleweke kuhujumiana hakuna hati miliki ya mtu, kikundi wala chama fulani.

Tunajenga nyumba moja.
Tume imechomoa mapingamizi kwa style yake
 
Tume imechomoa mapingamizi kwa style yake

Matumaini ni kuwa jitihada zile hazijapotea bure. Bado kuna mapingamizi mengi ya wabunge. Haiyumkiniki akili inatuingia.

Bado kuna ma kesi ya kubumba bumba.

Wapende wasipende hali ya uwanja ni tete. 'Pooo' ya kistaarabu bado ni muhimu.

Tume katengeneza mazingira hayo.

Mambo ni mbele kwa mbele hakuna kulala.
 
Natumaini ni kuwa jitihada zile hazijapotea bure. Bado kuna mapingamizi mengi ya wabunge. Haiyumkiniki akili inatuingia.

Bado kuna ma kesi ya kubumba bumba.

Wapende wasipende hali ya uwanja ni tete 'pooo' ya kistaarabu bado ni muhimu.

Tume katengeneza mazingira hayo.

Mambo ni mbele kwa mbele hakuna kulala.
Niwape pole ya uchovu watumishi wa tume..wana masaa mengine mengi ya kukesha kabla ya October 28...uchaguzi huu ni tofauti kabisa na mingine..huu ni uchaguzi na kufundishana sheria
 
Niwape pole ya uchovu watumishi wa tume..wana masaa mengine mengi ya kukesha kabla ya October 28...uchaguzi huu ni tofauti kabisa na mingine..huu ni uchaguzi na kufundishana sheria

Tatizo ni kuwa wanalazimika kumkingia kifua mgombea fulani.

Mbona ingekuwa haki bin haki ilikuwa burudani tu?

Hata hivyo hadi hapa tulipo si mbaya sana. Kama kwa Sirro tunawapongeza pia tukiendelea kumsubiria Juma naye atupe raha kwenye anga yake:

Pongezi Sirro, Mahakama na Tume ya Uchaguzi kazi kwenu
 
Back
Top Bottom