Inawezekana kufikia muafaka wa pamoja wa Legacy ipi ya Magufuli iendelee na ipi ifike mwisho. Tuelezane faida na hasara za kila Legacy

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,527
46,053
1.Kwa nini serikali inamiliki ndege?

Ndege zilinunuliwa kama hitaji muhimu kwa wananchi au fahari ya taifa?

2. Serikali kuhamia Dodoma.
Serikali ilihamia Dodoma ili kumuenzi Nyerere kama baba wa Taifa au lilikuwa ni hitaji muhimu la lazima la Taifa?

3.Kujenga miradi mikubwa kwa pesa zetu wenyewe za ndani ni akili kubwa au ndogo?
Sio kwamba hiyo ni kuongeza maumivu kupitia kukusanya kodi kwa nguvu zaidi badala akili? Tunazo pesa nyingi kiasi hicho?

4.Gesi ya Kusini bado ina mchango katika umeme wa nchi yetu? Mabeberu wamepewa au bado ni yetu?

5.Bandari ya Bagamoyo. Nani alisema au anasema kweli hasa?

6.Katiba mpya. Je tunahitaji au bado haina umuhimu kwa sasa?

7. Kila zama inaruhusiwa kuandika kitabu chake? Hii ni zama ya nani? Mwenye zama hii na yeye anaruhusiwa kuandika kitabu chake au lazima aendelee na kitabu alichokikuta?

Hizi nazo ni baadhi ya "Legacies" ambazo wafahidhina na wataka mabadiliko wanazozana!

Faida gani zilipatikana au zitapatikana kwa wananchi wanyonge na wasio wanyonge kwa maamuzi haya?

Tukiweza kupata majibu ya pamoja ya mambo hayo na mengine machache makubwa tutafunga kabisa huu mjadala wa "Legacy".
 
Kila wakitaka kufanya upigaji/deal lazima wamsingizie Nyerere.

Utasikia Bwala hili tutalipa Jina la Nyerere.

Tunahamia Dodoma kumuenzi Nyerere.

Ooh tunaongea kiswahili kumuenzi Nyerere(kumbe kuongea kiingereza ni shida)?

Lkn cha ajabu wamegoma kuishi maisha ya Mwl ya kila siku(wamejirundikia mali,wamegawa vyeo kwa watoto wao/michepuko,wanatugawa kikabila/kikanda).

Kwa hio ndg mwana JF popote pale ukisikia tunafanya hili kumuenzi Nyerere jua hapo wanataka kupitisha deal lao kwa kumsingizia Mwl Nyerere.
 
Wenye kusajiri legacy ni UN wamemaliza kazi kuhusu legacy ya hayatiJP Magufuli.Sikiliza hotuba za wawakilishi wa mabara mbalimbali leo kwenye kikao chao.
 
Back
Top Bottom