Inawezekana kuajiriwa serikalini na idara binafsi kwa wakati mmoja? Msaada

Vangigula

JF-Expert Member
Aug 13, 2015
844
2,717
Salamu wanajamvi,

Mimi ni mwajiriwa serikalini, nafundisha chuo. Kabla ya kupata ajira serikalini, nilishawahi kutuma maombi kwenye chuo kimoja kinachoendeshwa na taasisi ya kidini.

Nimeshafanya kazi serikalini mwaka mmoja, ila jana wale wa chuo binafsi wameniita kwenye interview, kwa kutumia applications nilizofanya miaka miwili nyuma.

Kibinadamu naelewa kwamba, kwa kwenda kwangu kwenye interview nitakuwa nawabania madogo wengi ambao bado wana hustle mtaani bila ajira.

Ila pia, tangazo la ajira lilitolewa zaidi ya miezi miwili, kwa maana kwamba fresh applicants wangepewa kipaumbele, jambo linalonipelekea kuamini kuwa naweza nikawakosesha wanafunzi utaalamu niliojifunza kwa kutokwenda kwenye interview.

Nikiwa bado natafakari hili la morals za kwenda au kutokwenda, naomba ushauri kwa yeyote mwenye uzoefu au ufahamu kama naweza kufanya kazi sehemu zote mbili kwa wakati mmoja.
 
Hata tatu inaruhusiwa! Ila fahamu utakua busy sana na hutakua na muda kukaa na mwenzio.Hapo ndipo hao unaowaita "jobless" watapata kazi kumfuraisha bby wako..
 
Kama ni mwalimu nahisi utapata muda wa kufanya kote.... nenda ... kwani mjini mmekuja kulima lami????
 
Unaweza, uwe muangalifu tu na muda usiingiliane kati ya hizo kazi mbili.
 
Hata tatu inaruhusiwa! Ila fahamu utakua busy sana na hutakua na muda kukaa na mwenzio.Hapo ndipo hao unaowaita "jobless" watapata kazi kumfuraisha bby wako..
Nashukuru. Umeliangalia kwa namna ambayo sikuwa nimeiwazia kabla. Nitaliweka maanani
 
Back
Top Bottom