Inawezekana ikawa kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inawezekana ikawa kweli?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tiba, Nov 4, 2009.

 1. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Nimefuatilia kwa karibu posting zinazofanyika kwa siku za hivi karibuni nyingi na kugundua kwamba nyingi zinahusu mahusiano na mambo ya mapenzi ukilinganisha zile zinazohusu mijadala juu ya mustakabali wa nchi kuhusu rushwa, matumizi mabaya ya madaraka, uhujumu uchumi, EPA na mafisadi wake na siasa za nchi yetu kwa ujumla.

  Nikiangalia kwa karibu kulikuwa na wimbi la watu kujiunga na JF some 6 months ago ambapo mijadala juu ya ufisadi ilikuwa imepamba moto na ninajikuta nalazimika kufikiria kwamba kulikuwa na msukumo fulani kutoka kwa mafisadi kuingiza "watu wao" kwa wingi hapa JF na kupost issues za mahusiano ili kupindisha attention ya watu kutoka kwenye kupigia kelele ufisadi na badala yake tuzame kwenye kujadili mambo yanayohusu mahusiano na mapenzi.

  Ikibidi Mods watupe data za aina za posting kwa siku za karibuni (at least for the past 6 months) ili tupime ukweli wa fikira zangu.

  Mnalionaje wazo hili, je lina ukweli wowote?
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  toa maelezo mazuri kijana!haupo uchi unajua?
  bado umevaa nguo.nenda straight kwenye point
   
 3. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,111
  Likes Received: 24,173
  Trophy Points: 280
  Mi bado naisoma sijaimaliza bado. Nikimaliza ntatoa comments zangu.
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hee kwani kama mtu ana interest na siasa anawezakupotea mlango aingie kule kwenye mahusiano? Ingekuwa mahusiano na siasa yapo chumba kimoja basi ingekuwa ni rahisi kwa mtu kuwa distracted. Mimi sidhani kama kuna ukweli katika hili. Ni mtazamo wangu tu
   
 5. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mhhh! hii nayo kali,leo nimekosa coment,ngoja na mimi nisome vizuri kama mchumba anavyofanya,labda nitapata mchango badae.
   
 6. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,111
  Likes Received: 24,173
  Trophy Points: 280
  Turudi kwenye nyumba yetu mama, tuache wanasiasa waendelee na mambo yao. Watu wengine bana, eti wanafikiri threads ndio nguvu za kupambana na ufisadi. Chukua form kagombee ubunge uwaletee watu wako maendeleo na kubwabwaja kuupiga vita ufidani. Ngoja nisepe, napitwa kule na utamu.
   
 7. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  Mkuu Tiba heshima mbele sana,

  Niseme tu kwamba kwanza hii hoja yako imenishangaza, I mean where is diversity in JF? kwa nini kuna majukwaa tofauti tofauti? ungependa wote wachangie siasa?

  Pili, hadi leo hii jukwaaa ka siasa lina posts zaidi ya 220,000, huku jukwaa la mahusiano na mapenzi likiwa na posts 36,000 hivi, je huo wingi unaozungumzia uko wapi? Huo uchunguzi mkuu uliufanyia forum hii hii ama nyingine?


  mkuu labda tukumbushane karibu serikali nzima ilijiuzulu mwezi wa pili mwaka jana (2008), ungesema hapo kulikuwa na mijadala mizito nitakuelewa. Hoja ya EPA na Richmond au kagoda na wadogo zake si za mwaka huu wala mwaka jana ni za muda mrefu na zimejadiliwa hapa kwa mapana na marefu. Ni kitu gani cha ajabu kimetokea 6 months ago kiasi cha mafisadi kutuma watu wao huku kudivert mada?


  mkuu hapa utakuwa unawapa mods kazi bila sababu, wenyewe wana kazi nzito kuhakikisha tupo hewani.

  Mwenyewe kwa nini usicheki tu ukaja hapa na data kila kitu si kipo hewani ?

  Otherwise, with all due respect, hii hoja siwezi kusema kama ina ukeli au haina, naiona totally irrelevant na isiyotegemewa kutoka kwa mtu wa kiwango chako.

  respect.
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Nov 4, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Yametengwa majukwaa tofauti kwa sababu watu tuna interests tofauti vilevile. Si wote waliojiunga na JF wanapendelea mambo ya EPA na SIASA, na kwa maoni yangu naona si kweli kuwa watu tuliojiunga miezi sita iliyopita tumetumwa na mafisadi kufunga mijadala ya ufisadi(tuombe[niombe] radhi tafadhali), mbona mijadala inaendelea kama zamani?
  Kuhusu jukwaa la mahusiano kuwa na post nyingi kipindi hiki, labda watu wengi wana matatizo ya kimahusiano zaidi na pale ni sehemu ya kupata ushauri na mafunzo.
  Ni hayo tu mkuu!!!!!!!!!!
   
 9. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Haujajibu hoja ndugu yangu. Sema kuna ukweli kwenye observation yangu au hakuna na utoe sababu!!!

  Tiba
   
 10. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Nakushukuru sana kwa mchango wako lakini sioni sababu ya kuomba radhi kwani sikumhukumu mtu hapa. Just my observations ambazo not necessarily ziwe kweli.

  Tiba
   
 11. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Tiba.

  Tafadhali elewa sio kila mtu ni mwanasiasa na mimi sipendi kabisa siasa, na kutokana na data zako unaonekana unaongea kwa hisia za kisiasa zaidi ya utashi ambao Mungu amekujalia na kama jina lako TIBA lilivyo.

  Mfano mimi nimejiunga tangu 2008 fwatilia thread zangu so utaona kwamba unasukumwa na hisia zaidi.

  Kama ni mapendekezo wafungie jukwaa la mapenzi pamoja na watu wake ambalo linachangiwa zaidi ili wabakie wanasiasa tu.

  Ningeomba pia uongozi wa JF utoe tamko au jibu kwa TIBA kwa kukaa kimya inaweza kuwa mme msupport au mmemuignore kitu ambacho sio haki kwani hizo ni fikra zake.
   
 12. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kaizer,

  Asante kwa mchango wako lakini nisaidie kunielewesha kiwango changu ni kipi mkuu, nisaidie hapa!!! Inawezekana sijijui sawasawa!!!!

  Hizo data ulizotoa ni kwa kipindi kipi mkuu? Tangia JF ianzishwe? au kuanzia tarehe ngapi mpaka lini?

  Tiba
   
 13. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  sasa si ungekuja na thread kwenye siasa? Instead of talking politics, you r talking about people not talking about politics!! Unafaa kuwa mwenyekiti wa kijiji wewe kweli?
   
 14. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu nakushukuru kwa hiyo Offer lakini ungevumilia mapungufu yangu na kujibu hoja. Mkuu mtu yupi niliyemsema mimi hapa?

  Asante.

  Tiba
   
 15. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  My God!,kweli ugonjwa huu wa kuhisi ni mbaya sana,unaweza kufa bure! huu ukweli hebu tuthibitishie wewe uliyekuja na hiyo hoja.
  ushauri wangu jiunge na jukwaa la mapenzi na mahusiano kwa kuwa naona siasa haikufai kwa mtaji huu kwani ishakuchanganya akili.Hivi tutawaondoa mafisadi kweli hapa? kazi bado ipo.
   
 16. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Nakushukuru kwa mchango wako lakini nasikitika umekwenda mbali kwa kutaka JF watoe tamko. Mimi nimeomba kama wanaweza kutoa data kusupport au kukanusha mawazo yangu. Very simple.

  Najua post kama hii inawagusa wengi hapa na hasa wale waliojiunga kwa nia niliyoifikiria mimi (sijasema na wewe ni mmoja wapo lakini!).

  Hizi ni fikira zangu tu sio lazima ziwe sahihi.

  Tiba
   
 17. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #17
  Nov 4, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  we tibakyenda wewe, kwani lazima wote tuongee siasa? wengine hatutaki stress bado tu wadogo kufa na pressure, nchi yenyewe ishauzwa hii, kwa nini sasa tuendelee kujipa machungu? sisi na mahusiano na mapenzi tu maana ndo maisha yetu tunayoyaishi kila siku, so kama unapenda siasa nenda kwenye siasa, wanaopenda mapenzi waache kwa raha zao maana naona unawapa mods kibarua kisichokuwa na maana wakati yeye mwenyewe ndo alipanga jukwaa la siasa, elimu, mahusiano, habari mchanganyiko etc. so have peace bro.
   
 18. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hizo fikra zako ni potofu, but in a way i understand you, you must be very stressed na politics, don worry it happens.
  BTW karibu kule jukwaa la mahusiano , you should be ok after 30 minutes when you are there. Karibu.
   
 19. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145

  Mkuu asante kwa mchango wako. Je tutaupiga vita ufisadi kwa kutumia muda wetu kuchangia hoja za mapenzi? Au inawezekana sijakuelewa mkuu!!!

  Tiba
   
 20. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #20
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu, naomba uthibitishe upotofu wa fikra zangu.

  Tiba
   
Loading...