Mkaruka
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 19,617
- 34,062
Anyway, kwanza usafiri binafsi ni gharama na ni mzigo.Mkuu hakuna gari jipya (miaka ya karibuni) lenye kodi nafuu kuliko gari la zamani (miaka ya nyuma) la aina hiyohiyo. Angalia na kucompare kwenye kalkuleta ya TRA na angalia mitaani gari nyingi ni zipi, mpya au za zamani.
Serikali haidiscourage watu kununua magari ya zamani bali kupitia ushuru inadiscourage watu kununua magari tu kwa ujumla (yawe mapya au ya zamani) bila sababu ya msingi.
Ndio sababu inayofanya watu waone kuwa serikali bado ina mawazo ya zamani, kuona gari kama anasa na kuwabania tu raia wake.
Muhimu serikali iboreshe usafiri wa umma.
Hata nchi zilizoendelea usafiri wa umma unaboreshwa ili watu wautumie kurpusha mifoleni isiyokuwa na sababu.
Unakuta msululu wa FOLENI ya magari 100 halafu yote ukichungulia ndani yana mtu MMOJA MMOJA tu. Upuuzi tu.
Nchi zetu masikini tunachukulia kuwa na gari ndio mafanikio kitu ambacho ni mindset ya kijinga tu.