Inawezekana chanzo kikubwa cha matatizo yetu kinaanzia katika Lishe

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
36,623
44,284
Kichwa kikubwa cha habari katika Mwananchi leo Jumapili ni "Lishe ina uhusiano na akili ya mtoto"
Mtaalamu anasema wakati mwingine unaweza kukimbazana na mtoto darasani kwa kuona haelewei kumbe ana udumavu.
Yaeleweza msingi mkubwa wa kumjengea lishe ni siku 1000 za kwanza na chini ya miaka mitano.

Inawezekana hata huku kwenye siasa, utumishi wa umma na mambo mengineyo ya kijamii tuna watu wengi ambao hawajielewei na hata ukiwasikiliza tu jinsi wanaongea unaona uduni na utepetevu wa fikra zao na kwamba hawewezi kubadilika tena kamwe.

Tuanzie kuandaa watoto wetu kiakili mapema kwa kuhakikisha wanapata Lishe bora yenye virutubisho vyote na sio kuwashindilia tu uji wa sembe,vitumbua,maandazi na chai ya rangi huenda tukaisidia na kuikwamua nchi yetu.
 
Hata akili, IQ kuwa kubwa au ndogo inatokana na chakula ulichokula kuanzia ulipokuwa tumboni kama mimba na ulivyokuwa unakua. ndio maana tunatakiwa kuhakikisha watoto wetu wanapewa lishe bora kwa makuzi bora ya akili/ubongo etc. vyakula vyenye omega3 ya kutosha, madini ya chuma etc. nimhimu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom