Inawezekana CCM ikawa ndio tatizo la nchi hii?

Blackafrica

Senior Member
Jun 26, 2021
141
401
Hii nchi ina kila kitu cha kuifanya iwe nchi Tajiri, lakini bado ni nchi maskini inayotegemea misaada kutoka kwa walipa kodi wa nchi nyingine, kila mradi unaofanyika Tz karibu yote inafadhiriwa na wahisani yaani ni aibu sana.

Nchi ambayo tunajivuna ina amani na rasilimali za kutosha, ilipaswa iwe nchi yenye maendeleo ya kujivuna, lakini ukweli ni kwamba ni nchi ya ajabu sana, idara zake nyingi zinanuka rushwa yaani kufanya biashara Tanzania inakubidi uwe na moyo kweli kweli, coz hakuna haki katika biashara, pia watu sio waamininfu na vile vile vyombo vingi vinavyohusika na mambo ya biashara havitekelezi wajibu wake vizuri.

Tunashindwa na nchi kama Rwanda kanchi kadogo, hata kenya yenyewe sio wa kutushinda sisi ambao tupo zaidi ya watu milioni 60, nchi haina dira, kila kiongozi anapangua na kupanga anavyotaka yeye, wananchi wengi ni wa hovyo, yaani kutokana na nchi kuwa ya hovyo hovyo hata wananchi tumekuwa wa hovyo hovyo, ni suala la muda tu, ila tunakoelekea wananchi wengi watanzania tutakuwa na sifa ya kuwa matapeli kama wanaigeria.

Tulipofika hapa tunahitaji mabadiliko kwa kweli, inawezekana CCM ikawa ni tatizo, hofu ya wengi yupi atakuwa mbadala wa CCM, nadhani waliopo ndani ya CCM waone hii fursa, wananchi wanataka mabadiliko sio vibaya tupate mabadiliko kwa kuwa na chama imara mbadala wa CCM, hicho chama kitokane na wanaccm waliochoshwa na wanaotaka mabadiliko, lakini vile vile kiwe na muunganiko na watanzania wazalendo wanaohitaji mabadiliko ya kweli katika nchi yao.

Tukubaliane hapa mda tuliowapa hawa jamaa CCM wa kuwa madarakani umetosha, sasa iwe zamu ya wengine nao pia tuwajaribu, labda wanaweza kutuvusha katika mabadiliko tunayoyataka, tuanze kujianda sasa kuhakikisha Tanzania tunayoitaka tunaifikia kwa kuhakikisha tunawaondoa madarakani hawa walioshindwa kazi miaka yote hiyo tuliyowapa kazi, 2025 ipo karibu tutumie fursa ya uchaguzi na fursa nyingine zozote kuwaondoa hawa jamaa ni tatizo katika nchi hii.
 
mawazo kama yako ndiyo yanatufanya kuwa nchi maskin...............huwez kuifananisha Tanzania na Rwanda.................Tanzanian ni nchi kubwa............tatzo vijana mnazani nchi inaendelea tu accidentally but kiukweli inachukua karne nyingi hadi hapa tulipo fika CCM imefanya kazi kubwa.
 
mawazo kama yako ndiyo yanatufanya kuwa nchi maskin...............huwez kuifananisha Tanzania na Rwanda.................Tanzanian ni nchi kubwa............tatzo vijana mnazani nchi inaendelea tu accidentally but kiukweli inachukua karne nyingi hadi hapa tulipo fika CCM imefanya kazi kubwa.
Kijana amka upo kwenye usingizi mzito unaota ndoto unakojoa, matokeo yake ni kukojoa kitandani, acha ujinga huo nchi hii inazo rasilimali zote za kufanya hata kila mwisho wa mwezi uwe unalipwa, pigania nchi yako acha mawazo mgando hayo
 
1637930516039.png
 
CCM walivyoingia kwenye mikataba ya madini miaka ya 90 nilijua sababu ya ujinga na ugeni labda ndyo ilipelekea kuingia mikataba ya hovyo vile Ila hata kwenye mikataba ya gesi 2015 kipindi nchi inawataalamu WA kila kitu nchi haipati chochote aisee ni Mambo ya kuuzunisha sana gesi waliyoipigia kelele na kuipitisha bungeni Kwa Hati ya dharura dah inaumiza sna ichi chama ni kansa kwenye hii nchii bila kuitoa ata iwe Kwa maumivu ya damu haitakaa ipone kamwe
 
mawazo kama yako ndiyo yanatufanya kuwa nchi maskin...............huwez kuifananisha Tanzania na Rwanda.................Tanzanian ni nchi kubwa............tatzo vijana mnazani nchi inaendelea tu accidentally but kiukweli inachukua karne nyingi hadi hapa tulipo fika CCM imefanya kazi kubwa.
Hii nchi umasikini ni mkali sana aisee tusidanganyane!!! Eti!!! Ninachofurahi ni mikoa ccm yenye ngome namna walivyo mafukara huwezi amini! Ukienda Dodoma kongwa ,singida,Moro,nk mmmmh kweli hii nchi ni duni sana
 
Kuna RAIA wa Kenya alitembelea vivutio vya utalii Tanzania!!! Akasema anaomba Mungu Tanzania iendelee kulala hivi hivi kwani Tanzania ikishituka utalii wa Kenya utahamia Tanzania!!!
Kauli iliniumiza sana hii
 
Back
Top Bottom