Inawahusu walio vyuoni na Waliomaliza degree na masharobaro

Think Hard

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
318
303
Hebu vuta picha, namna ulivyosota kuipata hiyo degree yako. Miaka isiyopungua 16 imeteketea darasani! Umebeba vidumu na ufagio kama wafagiaji wa jiji ukiwa shule msingi. Umepiga jaramba maili kadhaa kuifata shule. Umekumbana na kashkashi za walimu "wanoko", ukiwaona tu bandama zilikuwa zinacheza "ndombolo" na tumbo liliunguruma kama jenereta la kiwanda. Kasheshe ni pale ulipochaguliwa high school shule ya bweni! Enzi zile za ugali na maharage kama Segerea, wadudu ni wengi kuliko maharage! Hukukata tamaa ulivumilia kwa kuamini ipo siku tochi ya mafanikio itakumulika.

Ukupigao ndio ukufunzao, ila hukujifunza pale ulipochaguliwa chuo! Masikini akipata....Boom lote liliyeyuka kwenye nguo! ulitaka na wewe ufanane na "watoto wa jiji"! Ulihudhuria disco zaidi kuliko lecture. Flat screen, "dance floor" vikahamia chumbani kwako! Suplimentary zikakukosa kosa, tia maji tia maji MUNGU si Athumani ukamaliza chuo na gamba lako!

Wazazi wakawa na matumaini sasa ndio muda wa kula "pensheni" maana msomi umeshavaa joho! Umerudi chuo na rundo la makaratasi tu kama gari la magazeti! Yote hayo ukawaambia wazazi yanaitwa "madesa" na uliyasoma sana kumbe ulikuwa bingwa wa kuzima moto na"vizenga"(vibomu). Ulijulikana kama mzee wa"kujilipua". Mtaa ukakukaribisha kwa shangwe na vifijo. Haikupita wiki zile "Bata" za chuo ukaanza kuzimiss, daah! ulifulia hasa hata kifurushi uligongea cha bi mkubwa! Hizo zilikuwa salamu za rasharasha tu za kukukaribisha mtaani! Uliowaacha ambao hawakuendelea na masomo, wapo mtaani, baadhi wamepauka kama kopa la Mtwara, wengine "ngoma inogile" wanang'aa kama kikalio cha stova-wamewekeza kwenye biashara zao!

Enzi zile uko chuo ulikuwa unawavalia miwani ya mbao na kujifaragua kama joka la mdimu kuwa si class yako utaongea nao nini? Sasa ndio wamekuwa wenyeji wako mtaani! Aibuuu! Umeshikwa na haya,sura imekushuka kama viraka ya nyongeza vilivyoisaliti suruali! Kila kazi unayoomba unaambulia usaili tu! Nyingine hata usaili hutii pua! kazi moja mnaitwa alfu tano! khaa! Ulidhani mlisoma "Survival for the fittest " ili mfaulu mtihani tu?ndiyo uko maabara sasa.

Unazikumbuka pesa ulizozitumia "kula bata" chuoni, lol leo "bata" anakula wewe! "umeanza kuisoma namba" !Umepauka kama koti la mtunguo Tandika!Mungu si athumani ukabahatika ajira mpya huko kwetu "Nanjilinji". Mshahara laki 3,huna jinsi inabidi tu uende! Miaka mitatu sasa imepita huna tofauti na uliowakuta hapo "kijijini". Zile ndoto na hekaya za chuoni za kuwa na kazi ya 1.5M, ununue gari, ujenge nyumba, uwe na "demu" mkali, zoote zimeyeyuka kama samli kikaangoni! Magari unayaona mjini tu,"mademu" wakali unaendelea tu kuwaita "shemeji"! ndio hivyo, amtunzae mpiga zumari ndie anaechagua wimbo! Utatunza nini na wewe pangu pakavu tia mchuzi!sasa umekuwa mzee wa kaunda suti zakupauka kama inzi wa chooni.

Gucci unaziona kwenye filamu tu ,wewe ni magauni ya chirimeni tu! Mjini unakuja mara moja kwa mwezi kufuata mshahara! Mwanzoni ulikuwa unaona taabu kukaa kijijini, kila weekend uko mjini, unajifanya alwatani "vasco da Gama", baada ya shida kukutandika vibao, sasa huna jeuri ya kupanda gari kila wiki! Hivi si ulisema ukimaliza chuo nakupata kazi utaunga kusoma masters? Vipi kwani vyuo vimefungwa?Haya ndio maisha ya vijana wengi!

Hudhani mtaani kuna asali na maziwa wakishamaliza degree zao! Mtaani kuna hitaji zaidi ya hiyo degree!Kuna wakati degree inabidi uiweke pembeni ili ufunike kombe "mwanaharamu "apite! Lakini pia mtaa unakupokea kama ulivyojiandaa nao! kama kwa kutumia bumu lako ulijibana na kuhifadhi kidogo basi mtani utaziona fursa za kuwekeza hicho kidogo ulichonacho.

Kama ulikula bata tu na mtaani umerudi na mawigi, kucha feki na "modo" za kuvaa mlegezo basi mtaa hautakuonea aibu, utakupa swaga zake. Nguo ya ijumaa hufuliwa Alhamisi ‪Jipange jombaaaaaaaaaa
 
Hebu vuta picha,namna ulivyosota kuipata hiyo
degree yako. Miaka isiyopungua 16 imeteketea
darasani! Umebeba vidumu na ufagio kama
wafagiaji wa jiji ukiwa shule msingi. Umepiga
jaramba maili kadhaa kuifata shule.Umekumbana
na kashkashi za walimu "wanoko",ukiwaona tu
bandama zilikuwa zinacheza "ndombolo" na
tumbo liliunguruma kama jenereta la kiwanda.
Kasheshe ni pale ulipochaguliwa high school
shule ya bweni! Enzi zile za ugali na maharage
kama Segerea, wadudu ni wengi kuliko
maharage! Hukukata tamaa ulivumilia kwa
kuamini ipo siku tochi ya mafanikio itakumulika.
Ukupigao ndio ukufunzao,ila hukujifunza pale
ulipochaguliwa chuo!
Masikini akipata....Boom lote liliyeyuka kwenye
nguo! ulitaka na wewe ufanane na "watoto wa
jiji"! Ulihudhuria disco zaidi kuliko lecture. Flat
screen, "dance floor" vikahamia chumbani
kwako! Suplimentary zikakukosa kosa, tia maji
tia maji MUNGU si Athumani ukamaliza chuo na
gamba lako!
Wazazi wakawa na matumaini sasa ndio muda
wa kula "pensheni" mana msomi umeshavaa
joho! Umerudi chuo na rundo la makaratasi tu
kama gari la magazeti!Yote hayo ukawaambia
wazazi yanaitwa "madesa" na uliyasoma sana
kumbe ulikuwa bingwa wa kuzima moto na
"vizenga"(vibomu).Ulijulikana kama mzee wa
"kujilipua".
Mtaa ukakukaribisha kwa shangwe na
vifijo.Haikupita wiki zile "Bata" za chuo ukaanza
kuzimiss, daah! ulifulia hasa hata kifurushi
uligongea cha bi mkubwa! Hizo zilikuwa salamu
za rasharasha tu za kukukaribisha mtaani!
Uliowacha ambao hawakuendelea na masomo,
wapo mtaani, baadhi wamepauka kama kopa la
mtwara, wengine "ngoma inogile" wanang'aa
kama kikalio cha stova-wamewekeza kwenye
biashara zao!
Enzi zile uko chuo ulikuwa unawavalia miwani ya
mbao na kujifaragua kama joka la mdimu kuwa
si class yako utaongea nao nini? Sasa ndio
wamekuwa wenyeji wako mtaani! Aibuuu!
Umeshikwa na haya,sura imekushuka kama
viraka ya nyongeza vilivyoisaliti suruali!
Kila kazi unayoomba unaambulia usaili tu!
Nyingine hata usaili hutii pua! kazi moja
mnaitwa alfu tano! khaa! Ulidhani mlisoma
"Survival for the fittest " ili mfaulu mtihani tu?
ndiyo uko maabara sasa.
Unazikumbuka pesa ulizozitumia "kula bata"
chuoni,lol leo "bata" anakula wewe! "umeanza
kuisoma namba" !Umepauka kama koti la
mtunguo Tandika!
Mungu si athumani ukabahatika ajira mpya huko
kwetu "Nanjilinji". Mshahara laki 3,huna jinsi
inabidi tu uende! Miaka mitatu sasa imepita
huna tofauti na uliowakuta hapo "kijijini". Zile
ndoto na hekaya za chuoni za kuwa na kazi ya
1.5M, ununue gari, ujenge nyumba, uwe na
"demu" mkali,zoote zimeyeyuka kama samli
kikaangoni! Magari unayaona mjini tu,"mademu"
wakali unaendelea tu kuwaita "shemeji"! ndio
hivyo, amtunzae mpiga zumari ndie anaechagua
wimbo! Utatunza nini na wewe pangu pakavu tia
mchuzi!sasa umekuwa mzee wa kaunda suti za
kupauka kama inzi wa chooni. Gucci unaziona
kwenye filamu tu ,wewe ni magauni ya chirimeni
tu!
Mjini unakuja mara moja kwa mwezi kufuata
mshahara! Mwanzoni ulikuwa unaona taabu
kukaa kijijini, kila weekend uko mjini, unajifanya
alwatani "vascoda Gama", baada ya shida
kukutandika vibao,sasa huna jeuri ya kupanda
gari kila wiki! Hivi si ulisema ukimaliza chuo na
kupata kazi utaunga kusoma masters?Vipi kwani
vyuo vimefungwa?
Haya ndio maisha ya vijana wengi! Hudhani
mtaani kuna asali na maziwa wakishamaliza
degree zao! Mtaani kuna hitaji zaidi ya hiyo
degree!Kuna wakati degree inabidi uiweke
pembeni ili ufunike kombe "mwanaharamu "apite!
Lakini pia mtaa unakupokea kama ulivyojiandaa
nao! kama kwa kutumia bumu lako ulijibana na
kuhifadhi kidogo basi mtani utaziona fursa za
kuwekeza hicho kidogo ulichonacho.Kama ulikula
bata tu na mtaani umerudi na mawigi,kucha feki
na "modo" za kuvaa mlegezo basi mtaa
hautakuonea aibu, utakupa swaga zake.Nguo ya
ijumaa hufuliwa Alhamisi ‪Jipange
jombaaaaaaaaaa
Hakika neno la ukwel si zuri na neno zuri halina ukwel. Nimekusoma
 
Aisee we jamaa unawezafanya watu wajinyonge maana umeongea ukweli haswaaa! Haya sasa kazi kwao maisha ya kwenye TV yanawatafuna vijana wetu wanapokuwa chuoni ..kumbe! Maisha hayahitaji ukomedy...
 
Ukweli kabisa! Umepengilia vizuri matukio SMS sent ila ukweli hatujauzoea langu sikio mkuuuu!!;
 
Wambie wenye masikio watasikia hata zile smart phone wauze wawekeze kwenye kilimo na ufugaji wa kuku wa kisasa
 
Uliowaongelea ndo wako mtaani wanasubiri UKUTA Sept 1 WAKIDHANI NDO FURSA YA AJIRA.

Wakijaribu tu, watakuwa wanaangalia vyeti vyao kwa kuvipapasa maana yatabaki matobo yanayoonyesha kulikuwa na macho.
 
Hebu vuta picha,namna ulivyosota kuipata hiyo
degree yako. Miaka isiyopungua 16 imeteketea
darasani! Umebeba vidumu na ufagio kama
wafagiaji wa jiji ukiwa shule msingi. Umepiga
jaramba maili kadhaa kuifata shule.Umekumbana
na kashkashi za walimu "wanoko",ukiwaona tu
bandama zilikuwa zinacheza "ndombolo" na
tumbo liliunguruma kama jenereta la kiwanda.
Kasheshe ni pale ulipochaguliwa high school
shule ya bweni! Enzi zile za ugali na maharage
kama Segerea, wadudu ni wengi kuliko
maharage! Hukukata tamaa ulivumilia kwa
kuamini ipo siku tochi ya mafanikio itakumulika.
Ukupigao ndio ukufunzao,ila hukujifunza pale
ulipochaguliwa chuo!
Masikini akipata....Boom lote liliyeyuka kwenye
nguo! ulitaka na wewe ufanane na "watoto wa
jiji"! Ulihudhuria disco zaidi kuliko lecture. Flat
screen, "dance floor" vikahamia chumbani
kwako! Suplimentary zikakukosa kosa, tia maji
tia maji MUNGU si Athumani ukamaliza chuo na
gamba lako!
Wazazi wakawa na matumaini sasa ndio muda
wa kula "pensheni" mana msomi umeshavaa
joho! Umerudi chuo na rundo la makaratasi tu
kama gari la magazeti!Yote hayo ukawaambia
wazazi yanaitwa "madesa" na uliyasoma sana
kumbe ulikuwa bingwa wa kuzima moto na
"vizenga"(vibomu).Ulijulikana kama mzee wa
"kujilipua".
Mtaa ukakukaribisha kwa shangwe na
vifijo.Haikupita wiki zile "Bata" za chuo ukaanza
kuzimiss, daah! ulifulia hasa hata kifurushi
uligongea cha bi mkubwa! Hizo zilikuwa salamu
za rasharasha tu za kukukaribisha mtaani!
Uliowacha ambao hawakuendelea na masomo,
wapo mtaani, baadhi wamepauka kama kopa la
mtwara, wengine "ngoma inogile" wanang'aa
kama kikalio cha stova-wamewekeza kwenye
biashara zao!
Enzi zile uko chuo ulikuwa unawavalia miwani ya
mbao na kujifaragua kama joka la mdimu kuwa
si class yako utaongea nao nini? Sasa ndio
wamekuwa wenyeji wako mtaani! Aibuuu!
Umeshikwa na haya,sura imekushuka kama
viraka ya nyongeza vilivyoisaliti suruali!
Kila kazi unayoomba unaambulia usaili tu!
Nyingine hata usaili hutii pua! kazi moja
mnaitwa alfu tano! khaa! Ulidhani mlisoma
"Survival for the fittest " ili mfaulu mtihani tu?
ndiyo uko maabara sasa.
Unazikumbuka pesa ulizozitumia "kula bata"
chuoni,lol leo "bata" anakula wewe! "umeanza
kuisoma namba" !Umepauka kama koti la
mtunguo Tandika!
Mungu si athumani ukabahatika ajira mpya huko
kwetu "Nanjilinji". Mshahara laki 3,huna jinsi
inabidi tu uende! Miaka mitatu sasa imepita
huna tofauti na uliowakuta hapo "kijijini". Zile
ndoto na hekaya za chuoni za kuwa na kazi ya
1.5M, ununue gari, ujenge nyumba, uwe na
"demu" mkali,zoote zimeyeyuka kama samli
kikaangoni! Magari unayaona mjini tu,"mademu"
wakali unaendelea tu kuwaita "shemeji"! ndio
hivyo, amtunzae mpiga zumari ndie anaechagua
wimbo! Utatunza nini na wewe pangu pakavu tia
mchuzi!sasa umekuwa mzee wa kaunda suti za
kupauka kama inzi wa chooni. Gucci unaziona
kwenye filamu tu ,wewe ni magauni ya chirimeni
tu!
Mjini unakuja mara moja kwa mwezi kufuata
mshahara! Mwanzoni ulikuwa unaona taabu
kukaa kijijini, kila weekend uko mjini, unajifanya
alwatani "vascoda Gama", baada ya shida
kukutandika vibao,sasa huna jeuri ya kupanda
gari kila wiki! Hivi si ulisema ukimaliza chuo na
kupata kazi utaunga kusoma masters?Vipi kwani
vyuo vimefungwa?
Haya ndio maisha ya vijana wengi! Hudhani
mtaani kuna asali na maziwa wakishamaliza
degree zao! Mtaani kuna hitaji zaidi ya hiyo
degree!Kuna wakati degree inabidi uiweke
pembeni ili ufunike kombe "mwanaharamu "apite!
Lakini pia mtaa unakupokea kama ulivyojiandaa
nao! kama kwa kutumia bumu lako ulijibana na
kuhifadhi kidogo basi mtani utaziona fursa za
kuwekeza hicho kidogo ulichonacho.Kama ulikula
bata tu na mtaani umerudi na mawigi,kucha feki
na "modo" za kuvaa mlegezo basi mtaa
hautakuonea aibu, utakupa swaga zake.Nguo ya
ijumaa hufuliwa Alhamisi ‪Jipange
jombaaaaaaaaaa
Money is an ideal so if you are degree holder change you r ideal to monetary form
 
We unahisi ukiwa unasomea degree unakuwa isolated na society au....shida zote tunazifahamu ni kwamba tukianza kulia huwa tunavaa miwani nyeusi asione mtu na maisha yanaenda!
 
Hebu vuta picha, namna ulivyosota kuipata hiyo degree yako. Miaka isiyopungua 16 imeteketea darasani! Umebeba vidumu na ufagio kama wafagiaji wa jiji ukiwa shule msingi. Umepiga jaramba maili kadhaa kuifata shule. Umekumbana na kashkashi za walimu "wanoko", ukiwaona tu bandama zilikuwa zinacheza "ndombolo" na tumbo liliunguruma kama jenereta la kiwanda. Kasheshe ni pale ulipochaguliwa high school shule ya bweni! Enzi zile za ugali na maharage kama Segerea, wadudu ni wengi kuliko maharage! Hukukata tamaa ulivumilia kwa kuamini ipo siku tochi ya mafanikio itakumulika.

Ukupigao ndio ukufunzao, ila hukujifunza pale ulipochaguliwa chuo! Masikini akipata....Boom lote liliyeyuka kwenye nguo! ulitaka na wewe ufanane na "watoto wa jiji"! Ulihudhuria disco zaidi kuliko lecture. Flat screen, "dance floor" vikahamia chumbani kwako! Suplimentary zikakukosa kosa, tia maji tia maji MUNGU si Athumani ukamaliza chuo na gamba lako!

Wazazi wakawa na matumaini sasa ndio muda wa kula "pensheni" maana msomi umeshavaa joho! Umerudi chuo na rundo la makaratasi tu kama gari la magazeti! Yote hayo ukawaambia wazazi yanaitwa "madesa" na uliyasoma sana kumbe ulikuwa bingwa wa kuzima moto na"vizenga"(vibomu). Ulijulikana kama mzee wa"kujilipua". Mtaa ukakukaribisha kwa shangwe na vifijo. Haikupita wiki zile "Bata" za chuo ukaanza kuzimiss, daah! ulifulia hasa hata kifurushi uligongea cha bi mkubwa! Hizo zilikuwa salamu za rasharasha tu za kukukaribisha mtaani! Uliowaacha ambao hawakuendelea na masomo, wapo mtaani, baadhi wamepauka kama kopa la Mtwara, wengine "ngoma inogile" wanang'aa kama kikalio cha stova-wamewekeza kwenye biashara zao!

Enzi zile uko chuo ulikuwa unawavalia miwani ya mbao na kujifaragua kama joka la mdimu kuwa si class yako utaongea nao nini? Sasa ndio wamekuwa wenyeji wako mtaani! Aibuuu! Umeshikwa na haya,sura imekushuka kama viraka ya nyongeza vilivyoisaliti suruali! Kila kazi unayoomba unaambulia usaili tu! Nyingine hata usaili hutii pua! kazi moja mnaitwa alfu tano! khaa! Ulidhani mlisoma "Survival for the fittest " ili mfaulu mtihani tu?ndiyo uko maabara sasa.

Unazikumbuka pesa ulizozitumia "kula bata" chuoni, lol leo "bata" anakula wewe! "umeanza kuisoma namba" !Umepauka kama koti la mtunguo Tandika!Mungu si athumani ukabahatika ajira mpya huko kwetu "Nanjilinji". Mshahara laki 3,huna jinsi inabidi tu uende! Miaka mitatu sasa imepita huna tofauti na uliowakuta hapo "kijijini". Zile ndoto na hekaya za chuoni za kuwa na kazi ya 1.5M, ununue gari, ujenge nyumba, uwe na "demu" mkali, zoote zimeyeyuka kama samli kikaangoni! Magari unayaona mjini tu,"mademu" wakali unaendelea tu kuwaita "shemeji"! ndio hivyo, amtunzae mpiga zumari ndie anaechagua wimbo! Utatunza nini na wewe pangu pakavu tia mchuzi!sasa umekuwa mzee wa kaunda suti zakupauka kama inzi wa chooni.

Gucci unaziona kwenye filamu tu ,wewe ni magauni ya chirimeni tu! Mjini unakuja mara moja kwa mwezi kufuata mshahara! Mwanzoni ulikuwa unaona taabu kukaa kijijini, kila weekend uko mjini, unajifanya alwatani "vasco da Gama", baada ya shida kukutandika vibao, sasa huna jeuri ya kupanda gari kila wiki! Hivi si ulisema ukimaliza chuo nakupata kazi utaunga kusoma masters? Vipi kwani vyuo vimefungwa?Haya ndio maisha ya vijana wengi!

Hudhani mtaani kuna asali na maziwa wakishamaliza degree zao! Mtaani kuna hitaji zaidi ya hiyo degree!Kuna wakati degree inabidi uiweke pembeni ili ufunike kombe "mwanaharamu "apite! Lakini pia mtaa unakupokea kama ulivyojiandaa nao! kama kwa kutumia bumu lako ulijibana na kuhifadhi kidogo basi mtani utaziona fursa za kuwekeza hicho kidogo ulichonacho.

Kama ulikula bata tu na mtaani umerudi na mawigi, kucha feki na "modo" za kuvaa mlegezo basi mtaa hautakuonea aibu, utakupa swaga zake. Nguo ya ijumaa hufuliwa Alhamisi ‪Jipange jombaaaaaaaaaa
Umeingia mulemule kama ulikuepo vile.
 
Back
Top Bottom