Inaundwa tume kuchunguza kaburi la faru John

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
145,635
2,000
Ni maamuzi yenye ukakasi mkubwa....je tuna mangapi mazito ndani ya nchi hii yanayohitaji kutatuliwa? Ni kweli kabisa tunahitaji kuunda kikosi kizima cha tume kwa ajili ya faru mmoja tu?
Mbona habari mlizonazo mpaka sasa zinatosha kabisa kuwachukulia hatua waliohusika
Imeundwa timu ya kwanza ikaja na taarifa yake... .waziri hajaridhika nayo
Kuna kikosi kazi cha uchunguzi kinaendelea na na kazi
Kuna timu nyingine inafuatilia vinasaba
Na sasa Kuna tume nyingine inaundwa kwa ajili ya jambo hilohilo
Tunajua wanyama wetu hawa hatari wanazokabiliana nazo lakini naona kama ni too much sasa
 

goodluck5

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
4,028
2,000
Hata mie binafsi mh wm hapo sijamkubali.....utawala huu wa awamu ya tano na matume tume wapi na wapi??
Sie tunajua ni kata funua mwendo mdundo, tafadhali mh usiturudishe enzi za awamu ya nne.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
145,635
2,000
Ni uwajibikaji pia mkuu sioni tatizo, kama uhuni unaendelea pamoja na matatizo tuliyonayo hatuna budi kushughulika nao bila kuangalia mtu usoni.
Jeshi la police lingetosha kabisa kufanya hiyo kazi mbona? Umeona huo mlolongo wa hizo task force lakini?
 

kisingi

JF-Expert Member
Apr 9, 2014
493
500
Msiwe na wasi baada ya faru utafuata uchunguzi wa DNA za waliotupwa kwenye viroba kuthibitisha kama ni wahamiaji haramu. Nchi ipo makini na viumbe hai wake wakiwemo binaadamu.
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
22,751
2,000
Wakati wa Mkapa 1996 iliwahi kuundwa Tume kuchunguza hukumu ya Kifo aliyopewa Mbwa mmoja huko Mbeya kwa kosa la kupewa Jina la Afisa Uhamiaji wa Mbeya aliekuwa hapendwi na wakazi wa huko
 

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,871
2,000
Kimsingi ukiishi karibu na mbuga za wanyama utajua hawa viumbe wamepewa thamani na umuhimu hapa tz kuliko binadamu. Tembo kuua watu serengeti ni jambo la kwaida , tembo kuharibu mazao ya watu na kusababisha njaa huko Mugumu na serengeti kwa ujumla wala si jambo geni na serikali inaweza kufidia kidogo au wasitoe kabisa fidia. Lakini tembo akiuwawa hata baada ya kumuua mtu utajua kama kuku anakojoa au lah. Hivi kama serikali wanajua faru John kauzwa sehemu kwanini wasitoe tu ushahidi na kuwakamata hao wahusika?, kwanini wafanye kuzunguka na kukataa kile wanachoambiwa na wahifadhi ilhali hawataki kutoa ukweli wao?. Wapi tume inayochunguza vifo vya watu huko Ruvu? . Siungi mkono wananchi kuua tembo au faru, siungi mkono ujangili ILA PIA SIUNGU MKONO JUHUDI NYINGI ZINAZOFANYWA NA SERIKALI KWA HAWA WANYAMA KULIKO KWA BINADAMU.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom