Inaumiza : Mali zetu zinapogeuka kuwa chanzo cha kupoteza uhai wetu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inaumiza : Mali zetu zinapogeuka kuwa chanzo cha kupoteza uhai wetu...

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by only83, May 22, 2011.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  ...Wiki iliyopita kumetokea mahuaji ambayo kila mtanzania mpenda haki na mzalendo atakuwa ameguswa sana na vifo hivi...Ni vifo vya watanzania wenzetu wachumiaji juani kama sisi walipopoteza uhai baada ya kuitwa ni majambazi wa mali za wawekezaji ktk mgodi wa dhahabu kule Musoma....Napata shida kidogo ni nani jambazi kati ya hawa wawekezaji+serikali au wakazi wa Nyamongo...Nilizidi kuumia sana pale nilipomsikia waziri mmoja akisema wale hawakuwa wananchi bali majambazi,na kushangaza serikali hiyohiyo ikapeleka rambirambi kwa wafiwa,nawapongeza wafiwa kwa kukataa unafiki na udhalilishaji huu wa hawa wahuni...Nacho jiuliza

  • Je,mpaka lini mali zetu zitakuwa chanzo cha kutoa uhai wetu?
  • Je,ni nani jambazi kati ya serikali ya CCM au Wananchi wa Nyamongo?
  • Ni nini suluhisho la matatizo haya katika sekta ya madini?
  • Je,kuna haja kuwa na serikali isiyowajibika kulinda mali na uhai wa wananchi wake badala yake inakuwa ni kibaraka wa wawekezaji mabeberu?
   
Loading...