INAUMA SANA: Unayempenda kwa dhati kabsa, anapokuchukulia kama Rafiki yake wa kawaida

Evans-Arsenal

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
868
1,385
Ninapoandika huu Uzi inawezekana yeye yupo katika hali ya kawaida kabsa lakini ajue ya kwamba kuna mtu ambaye anampenda na anatamani awe Nuru itakayomulika Maisha yake.

Kweli huyu mtu nmempenda tena sana na ninatamani one day ndo awe Nuru yangu na karibu yangu, lakini inawezekana Distance ya urafiki wetu imezidi kiasi cha kwamba hata Neno lolpte nitakalolitoa kinywani kwangu ataliona kama vile nimesema kama ushauri/ujumbe kwake.

Nimemwambia hivi:
" J nakupenda kwa dhati na ninhitaji kuwa karibu yako zaidi ya urafiki wetu ulivyo sasa...really nakupenda sans J"

J Akajibu hivi:
" Hata mimi nakupenda F na ninahitaji uwe karibu na mimi siku zote kunielimisha na kuniasa kama rafiki yangu..."

Kuna vitu vinauma sana kama kuibiwa Mume au Mke au may be kugongewa Demu/Mchumba wako unayempenda na mtu mwingine lakini kuambiwa wewe ni Rafiki na yule unayempenda ni MAUMIVU makubwa sana na inauma kwa kweli.

Niseme tu pamoja na kwamba kila mtu ana haki ya kukubali na kukataa lakini kwa kweli Jambo la kukataliwa na mtu ambaye ulikuwa naye muda mwingi katika mambo mbalimbali ni jambo linaloumiza sana.

Nashindwa nianzie wapi tena kutokana na Maneno yake ya "FriendShip"
d272f5742c3eb194f05ec9a8bfc6bc33.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, ukiambiwa hivyo tambua kabisa hauna mvuto wa kifamilia /ndoa au mahusiano kwa mtu husika, yaani ni kweli ninyi ni marafiki ila kwenye kwichikwichi hot-eheh anakuona mtoto wa chekechea au gulagula fulani hivi.

Any way, unaweza ukalazimisha ukawa naye, ila kumbuka you're likely to be badly injured in the near future.
 
Katika kitu ambacho sijawahi na sitawahi kufanya ni kuwa na urafiki na mtoto wa kike au mwanamke... aiseee Mungu anisamehe tu katika hili.o_O:(;):):D
 
Mkuu pole sana, we fanya kukatisha mazoea ya waziwazi kwa ghafla tu, kama ulikuw unampigia kila siku basi usipige kabisa, kama rafiki yako huyo anajali ukaribu wenu lazima atakuuliza shida ni nini mbona umebadilika ghafla, sasa hapo na wewe ndo umwagike ki utu uzima kwamba umefikia mahali pa kushindwa kuvumilia ukaribu wa kirafiki na mtu ambaye unampenda kimapenzi. Nafkiri atakuwa anaelewa unamaanisha nini kuanzia hapo

G.Man
 
COPY AND PASTE

Jinsi Ya Kuuhepa Mtego Wa Kuwa Rafiki Na Mwanamke Unayempenda

Kama kuna kitu ambacho wanaume wanachukia ama kuogopa ikija katika maswala ya mahusiano ni kuona yule mwanamke unayempenda amejeuka rafiki yako badala ya mpenzi wako. Hii inajitokeza wakati mwanamume anaposhindwa kutumia mbinu mwafaka ambazo zitamwezesha yeye kutofautisha kati ya rafiki na mpenzi. Hii inadhihirika wakati ambapo mwanamume anakuwa rafiki wa mwanamke sana kupiti kiasi, inafikia level ambayo mwanamke anakuona wewe kama mtu ambaye akikumbwa na tatizo basi anakufikiria wewe. Wanaume wengi ikifikia hatua kama hii wanashindwa kujitatua na wanaishia kuwaona wanawake wanaowapenda kuchukuliwa na waume wengine huku wao wakiwa wameachwa katikati bila kujua la kufanya.
Ok. Kama wewe ni mmoja wa wanaume ambao wameachwa katika sehemu ya urafiki (friend zone) basi fahamu kuwa kuna habari njema. Tatizo lako limetatuliwa kwa njia rahisi.

1. Kuwa rafiki yake lakini tofauti na marafiki zake wengine
Msiongee vitu vya kijinga kwa masaa mengi ama mkae mnaongea kuhusu matatizo yake anayokumbana nayo maishani. Mnafaa kuongea vitu kama sinema, sehemu anazotembea, vitu ambavyo anapanga kufanya wikendi nk. Ongea vitu ambavyo vinahusiana na kudate. Hapo utafanya kuwe na msisimko kati yenu juu ya hewa.

2. Jaribu kuongea naye mkiwa pekeenu
Kama yuko na marafiki zake wengine, unaweza kuongea na yeye ama ukaamua kutoongea kabisa manake hauwezi kumrushia matamu akiwa pamoja na kundi zima la marafiki.
Mkiwa wawili unaweza kujaribu kutumia maujanja wa kumsuka bila yeye kutambua halafu kama kumekuja mtu wa tatu fanya kujeuza stori fasta. Hii itamuacha yeye kujiuliza kama kweli ulikuwa unafanya mzaha ama uko serious.
Hii itampa fikra za kuwa wewe unapenda zaidi kuongea na yeye mkiwa wawili pekee. Mwonyeshe dhahiri kuwa unapenda company yenu zaidi mkiwa wawili. Lakini chunga usithubutu kumwambia kuwa unampenda ama wataka kumtoa out.

3. Msifu wakati ambapo inahitajika
Kama amependeza usisahau kuchukua nafasi ya kumsifu. Pia unaweza kutumia ujanja wa kuchungulia kifua chake halafu kama amekuona ukimuangalia, fanya kutabasamu, mwombe msamaha halafu umwambie kuwa ulikuwa umeshindwa kujizuia. Jaribu kuongea na maneno ya ucheshi wa mapenzi na kutoa maoni ya mapenzi. Amini usiamini ataanza kukufikiria tofauti na utakuwa ukijinasua pole pole kutoka friend zone.

4. Mshike na mchukulie kama ni girlfriend wako
Lakini fanya na heshima. Unaweza kumshika mkono wakati mnavuka barabara na pia kumfungulia mlango kwa nyinyi wawili. Mfanye ajihisi yeye kama malkia na ataanza kupenda ateshen yako. Akiwa na marafiki wengine usimwonyeshe dalili hizi. Mfanye aelewe kwamba hii inatokea kama mko wawili pekee.
5. Mfanye ajihisi kuwa yeye specially
Mtuze kwa kumletea zawadi ndogo ndogo na binafsi mfano waweza kumletea ushanga nk lakini hakikisha kuwa umemwambia kuwa iwe siri kati yenu. Ukifanya iwe siri yenu utakuwa automatically unafungua mlango wa mapenzi na ataanza kukufikiria na mtizamo mwingine. Utakuwa mnajenga kemia kati yenu.

7. Muulize kama anataka kutoka out halafu ubadilishe stori fasta
Kama unaongea na yeye unaweza kumwambia kuwa unataka kumtoa lunch ama kwa mkahawa. Lakini kabla hajajibu fanya kumjeuzia topic nyingine ili abaki ajiuliza kama ulikuwa unafanya mizaha au la. Hivi itakuwa ikondoa tenshen ambayo itakuwa imejitokeza wakati wa kuuliza swali kama hilo.

Hii ndio njia rahisi ya kutumia na mara kwa mara utaona kuwa amevutiwa na wewe. Baada ya muda flani unaweza kuchukua hatua ya kumuuliza kama angetoka date na wewe na hapo hawezi kukataa.
 
Utaambiwa ndefu sana mkuu..
 
Sure mkuu mwanamke anayekuita KAKA ilo hali unampenda kimapenzi duuuuhhhhh homa kweli !!..

But anyway keep going ..you feel like you are passing though the hell just keep going ,endelea kumfanyia mema wala usikate tamaa na kurudi nyuma.

Ila nawewe go straight mwambie namna gan unamhitaji thibitisha unamhitaji kama mwenza wa maisha yako , ""kua mkorofi wafaida kwake"" .

Hayo mambo ya ushauri tuuuuuuuuuuuuuuuu ndo maana ana....
 
Usione soo sema nae kama unampenda
Nimekumbuka ule wimbo wa usione soo sema nae kuhusu kusubiri kuwa mwaminifu au kutumia kondomu ... Walikuwaga wanauweka kabla au baada ya maigizo ya fukuto, johari na mengine huko ya kina kanumba jumamosi jioni
 
Back
Top Bottom