Inauma sana, Serikali itazame upya jambo hili

Kijana masikini aliyekesha internet cafe kwa siku mbili mfululizo kuhakikisha taarifa zake za maombi ya ajira anazi-upload OTEAS kwa umakini asikosee, leo kakosa ajira, na anaambiwa hao waliopata ajira walikosea kujaza form, TAMISEMI wakawarekebishia na kuwapa ajira!

Watu hawa wanamjibu hivi huyu kijana wakifikiri atawaelewa kweli?

Yaani nimekesha kuhakikisha taarifa zangu sahihi zinaenda lakini anaeajiriwa ni yule aliyetuma taarifa za uongo? SERIOUS? SERIKALI YA WANYONGE?

Hakuna mtu kutoka familia bora anayeweza kuacha starehe nyumbani kwao na kwenda kufundisha shule za umma tena bila malipo yoyote ama kwa kulipwa 30k per month, most of volunteers ni watoto wa maskini wasiona koneksheni yoyote, hawana cha kufanya ndio wameamua angalau kwenda kuwasaidia wadogo zao walioko mashuleni japo kwa shida tena bila malipo yoyote, kwa serikali makini hawa vijana walitakiwa kutazamwa kwa jicho la kipekee sana, badala ya kukaa vijiweni kuilaumu serikali kwa kutotoa ajira za kutosha wao wameamua kuisaidia serikali na Taifa lao

Leo iweje tunawaona kama takataka na kuamua kuingiza watu tunaojuana nao ama Tamisemi kuthamini zaidi rushwa na kuwaacha vijana hawa wakiendelea kuteseka mtaani? Mmethamini hao ambao hata hamjui walikuwa wakijihusisha na mambo gani huko mtaani mnawaacha hawa ambao waliamua kuendeleza taaluma zao na kukuza zaidi uwezo wao wa kuderiver materials kwa wanafunzi?

Binafsi pia nimuombaji, mfumo wa OTEAS ilikuwa ukikosea ku-upload informations zako haukuruhusu uendelee na hatua inayofuata mpaka utakaporekebisha makosa, swali ni je, hao wahitimu wa 2017, 2018 & 2019 waliomba kupitia mfumo gani? (HAPA KUNA HARUFU YA RUSHWA)

Leo ndio ile siku, vijana masikini walioamua kujitoa kulitumikia taifa lao kwa kujitolea kwenye mashule ya umma wataanza kupokea watoto wa vigogo na wakurugenzi makazini kwao wakiwa wameajiriwa tayari, hawa volunteers waliotiwa moyo na TAMISEMI kimagumashi, sijui wataendelea kujitolea kwa moyo uleule? Ama watakata tamaa?

Maafisa elimu waliokuja kwenye mashule yetu na kutukuta vijana tunajitolea huku tukiwa tumechoka, hali mbaya, na kutuahidi kuwa tusife moyo serikali yetu haitatutupa mkono kwa fulsa yoyote itakayotokeza, watakuja tena?
Wakija watatueleza nini tena?

Je, vijana tutaendelea kuiamini serikali hiii?

Je, kama tutapoteza imani juu ya serikali na viongozi wake nini kitafuata?

VIONGOZI
Mmewahi kujiuliza mnajenga attitude gani kwa vijana dhidi yenu?

Mnafikiri hiki mnachokitengeneza sasa kitaleta positive ama negative impacts kwa Taifa siku za usoni?

Leo hii kama mmetufuata vituoni kwetu nakutuahidi mtatupa kipaumbele na zaidi mkachukua na taarifa zetu, na sisi tukawaeleza mama zetu kuwa serikali imesema haitatuacha fulsa zikitokea, haya maumivu tuliyonayo sisi wazazi wetu na jamii zetu yataisha tu hivi hvi? Hayatakuwa na madhara yoyote?

Mimi binafsi kunidanganya sio tatizo, tatizo mmemdanganya mpaka mama yangu aliyeuza nguo zake ili nisome, leo ananiuliza namwambia nimekosa ajira, ananiuliza tena kwani serikali si ilisema mtaajiriwa kwanza? Nikakosa jibu, mama katoa chozi

Mimi ninauvumilivu wakushuhudia mama yangu akilizwa na serikali hiii?

Any way. Newton's third law of motion "To every action there is an equal and opposite reaction".

MUNGU WETU NI MWEMA.
MITANO TENA
 
Tumeleta fursa za ajira kupitia bomba la mafuta vijana watapata ajira wabeba zege,wachimba mitaro,mama lishe,watoa huduma za fedha takriban ajira 200000.nasema kwa dhati ya moyo wangu maendeleo ni ya mutu mumoja mumoja ipeni kura ccm
 
Hoja alizotoa hata

Li

Hoja alizotoa hata hazina mashiko. Hivi kutuma taarifa kwa usahihi kunahitaji kukesha two nights cafe!!??.
Ajira zilitangazwa kwa watu wenye taaluma au kwa maskini???
Mfumo wa kuomba ajira haukuwa perfect ndo maana na wenyewe wamejaribu ku adjust fairness ili ku clear makosa ya mfumo. Trust me or not, kama kuna mtu alijaza taarifa sahihi kwa 100% bas hawafiki 5% tukianza tu na DoB ambapo ilikuwa inajiadjust yenyewe kurudi nyuma siku moja, yaani ukiweka ulizaliwa tar 21 yenyewe ilikuwa inajiweka tar 20. Ili ioneshe umezaliwa 21 ni lazima uweke tar 22, Sasa yeye anasemaje amekesha siku mbili kuweka taarifa kwa usahihi??!

Akubali tu amekosa na awe mpole maana kulikuwa hamna namna ya wote walio apply kupata. Sio kuleta vigezo vya umaskini na kukesha ambavyo havikuwepo kwenye system.
Aah we unasema kweli?kwa hiyo kama ni wa tarehe moja unaandika tarehe 30/31vya mwezi wa nyuma?
 
Back
Top Bottom