Inauma sana, Serikali itazame upya jambo hili

Oct 14, 2020
12
53
Kijana masikini aliyekesha internet cafe kwa siku mbili mfululizo kuhakikisha taarifa zake za maombi ya ajira anazi-upload OTEAS kwa umakini asikosee, leo kakosa ajira, na anaambiwa hao waliopata ajira walikosea kujaza form, TAMISEMI wakawarekebishia na kuwapa ajira!

Watu hawa wanamjibu hivi huyu kijana wakifikiri atawaelewa kweli?

Yaani nimekesha kuhakikisha taarifa zangu sahihi zinaenda lakini anaeajiriwa ni yule aliyetuma taarifa za uongo? SERIOUS? SERIKALI YA WANYONGE?

Hakuna mtu kutoka familia bora anayeweza kuacha starehe nyumbani kwao na kwenda kufundisha shule za umma tena bila malipo yoyote ama kwa kulipwa 30k per month, most of volunteers ni watoto wa maskini wasiona koneksheni yoyote, hawana cha kufanya ndio wameamua angalau kwenda kuwasaidia wadogo zao walioko mashuleni japo kwa shida tena bila malipo yoyote, kwa serikali makini hawa vijana walitakiwa kutazamwa kwa jicho la kipekee sana, badala ya kukaa vijiweni kuilaumu serikali kwa kutotoa ajira za kutosha wao wameamua kuisaidia serikali na Taifa lao

Leo iweje tunawaona kama takataka na kuamua kuingiza watu tunaojuana nao ama Tamisemi kuthamini zaidi rushwa na kuwaacha vijana hawa wakiendelea kuteseka mtaani? Mmethamini hao ambao hata hamjui walikuwa wakijihusisha na mambo gani huko mtaani mnawaacha hawa ambao waliamua kuendeleza taaluma zao na kukuza zaidi uwezo wao wa kuderiver materials kwa wanafunzi?

Binafsi pia nimuombaji, mfumo wa OTEAS ilikuwa ukikosea ku-upload informations zako haukuruhusu uendelee na hatua inayofuata mpaka utakaporekebisha makosa, swali ni je, hao wahitimu wa 2017, 2018 & 2019 waliomba kupitia mfumo gani? (HAPA KUNA HARUFU YA RUSHWA)

Leo ndio ile siku, vijana masikini walioamua kujitoa kulitumikia taifa lao kwa kujitolea kwenye mashule ya umma wataanza kupokea watoto wa vigogo na wakurugenzi makazini kwao wakiwa wameajiriwa tayari, hawa volunteers waliotiwa moyo na TAMISEMI kimagumashi, sijui wataendelea kujitolea kwa moyo uleule? Ama watakata tamaa?

Maafisa elimu waliokuja kwenye mashule yetu na kutukuta vijana tunajitolea huku tukiwa tumechoka, hali mbaya, na kutuahidi kuwa tusife moyo serikali yetu haitatutupa mkono kwa fulsa yoyote itakayotokeza, watakuja tena?
Wakija watatueleza nini tena?

Je, vijana tutaendelea kuiamini serikali hiii?

Je, kama tutapoteza imani juu ya serikali na viongozi wake nini kitafuata?

VIONGOZI
Mmewahi kujiuliza mnajenga attitude gani kwa vijana dhidi yenu?

Mnafikiri hiki mnachokitengeneza sasa kitaleta positive ama negative impacts kwa Taifa siku za usoni?

Leo hii kama mmetufuata vituoni kwetu nakutuahidi mtatupa kipaumbele na zaidi mkachukua na taarifa zetu, na sisi tukawaeleza mama zetu kuwa serikali imesema haitatuacha fulsa zikitokea, haya maumivu tuliyonayo sisi wazazi wetu na jamii zetu yataisha tu hivi hvi? Hayatakuwa na madhara yoyote?

Mimi binafsi kunidanganya sio tatizo, tatizo mmemdanganya mpaka mama yangu aliyeuza nguo zake ili nisome, leo ananiuliza namwambia nimekosa ajira, ananiuliza tena kwani serikali si ilisema mtaajiriwa kwanza? Nikakosa jibu, mama katoa chozi

Mimi ninauvumilivu wakushuhudia mama yangu akilizwa na serikali hiii?

Any way. Newton's third law of motion "To every action there is an equal and opposite reaction".

MUNGU WETU NI MWEMA.
 
Kwa maana hiyo tangu unasoma hadi unahitimu elima yako bado unashindwa kutofautisha Siasa na uhalisia wenyewe.

1. serikali hainauwezo wa kuajiri watu wote tena kwa wakati mmoja.

2. Usisome ukitegemea ajira bila kujali umetoka familia ya aina gani. Kufanya hivyo utakuwa unaishi maisha ya kimiujiza.

3. Kujitolea huo ni utashi wako mkuu, unategemea afisa elimu akukute kituoni umejitolea akupe neno gani la kukutia moyo zaidi ya kusema serikali itawaajiri ili kutokukatisha tamaa. Huyo Afsa elimu mwenyewe ameajiriwa na sio muajiri wako.

MYTAKE!
kwa vijana wenzangu ebu ifikie mahali tuikubali hii changamoto ya ajira maana idadi ndio kwanza inaongezeka kila mwaka hapo tunategemea nini? zaidi ya kutafuta njia nyingine ya kujinusuru
 
Kwa maana hiyo tangu unasoma hadi unahitimu elima yako bado unashindwa kutofautisha Siasa na uhalisia wenyewe.

1. serikali hainauwezo wa kuajiri watu wote tena kwa wakati mmoja....
Yaani nimekesha kuhakikisha taarifa zangu sahihi zinaenda lakini anaeajiriwa ni yule aliyetuma taarifa za uongo?
 
Yaani nimekesha kuhakikisha taarifa zangu sahihi zinaenda lakini anaeajiriwa ni yule aliyetuma taarifa za uongo?????

Naomba utambue hili.

Mfumo wa kuomba ajira ulikuwa na changamoto nyingi hii ni kutokana na kushindwa kuwapa watu wenye waledi katika mambo ya IT. Ulikuwa ukiapload vyeti na docoment zingine leo kesho ukija kutazama inaambiwa incomplete:

Kwa mantiki hiyo watu wengi walidhani wamekamilisha kufanya application, kumbe mfumo uliwatema na taarifa zao hazikufika mahala husika. Tafuta idadi ya walio omba uone ukweli wa ninachokisema:

Serikali yetu haijawa makini kabisa katika mambo ya muhimu ipo makini na siasa za kipumbavu hiyo yote ni kila mtu anatafuta pesa
 
Naomba utambue hili.
Mfumo wa kuomba ajira ulikuwa na chsngamoto nyingi hii ni kutokana na kushindwa kuwapa watu wenye waledi katika mambo ya IT.
ulikuwa ukiapload vyeti na docoment zingine leo kesho ukija kutazama inaambiwa incomplete:
Kwa mantiki hiyo watu wengi walidhani wamekamilisha kufanya aplication , kimbe mfumo uliwatema na taarifa zao hazikufika mahala husika. Tafuta idadi ya walio omba uone ukweli wa ninachokisema:

Serikali yetu haijawa makini kabisa katika mambo ya mhimu ipo makini na siasa za kipumbavu hiyo yote ni kila mtu anatafuta pesa
Daaaah!
 
So sad! Kuna kijana mmoja anafanya kazi ya kujitolea kwa zaidi ya mwaja 1 sasa. Kwenye ile shule kila mzazi anatakiwa kulipa tsh. 600 kila mwezi Kama gharama ya ada kuwasaidia walimu wanaojitolea.
 
Kwa maana hiyo tangu unasoma hadi unahitimu elima yako bado unashindwa kutofautisha Siasa na uhalisia wenyewe.

1. serikali hainauwezo wa kuajiri watu wote tena kwa wakati mmoja....
Naona pia vijana hawalilii kukosa ajira wanachohoji na utata kwenye utoaji wa ajira mfumo umekuwa mbaya kuzidi hata miaka ilopita
 
Acheni kulialia, kwani hao tamisemi ni malaika? Hawakosei?
Ungekuwa umepata usingekuja na hili povu...
Lazima tutambue jitihada za serikali hata kwa kile kidogo, sio kuona madhaifu tu...
 
Walioomba hizo kazi za ualimu walikuwa watu 97000 na serekali ilikuwa inajtaji walimu 130000

Ingekuwa ww ungempa nan ungemuacha nan?
 
Yaani nimekesha kuhakikisha taarifa zangu sahihi zinaenda lakini anaeajiriwa ni yule aliyetuma taarifa za uongo?
Unaulaumu mfumo, serikali, umaskini wako au aliyeajiriwa?
Halafu kila aliye apply alikuwa ana uhitaji kwahyo ulitaka upate wewe wengine wakose?
Pambana na hali yako. Subiri hizo 5000 zilizobaki ndio za maskini waliotuma taarifa kwa usahihi.
 
Unaulaumu mfumo, serikali, umaskini wako au aliyeajiriwa???!
Af kila aliye apply alikuwa ana uhitaji kwahyo ulitaka upate wewe wengine wakose?
Pambana na hali yako. Subiri hizo 5000 zilizobaki ndo za maskini waliotuma taarifa kwa usahihi.

Ngumu kumeza
 
Ukishakubali kua The world is unfair and no one owes u shit basi hakuna kitu kitakusumbua. Count your loses and keep on.
 
Pole sana mwalimu..tambua siasa ni maneno tu ukiziaminj utapotea..wao wanatafuta ulaji..chamsingi pambana tu kiume..ondoa matumaini kwenye siasa..Mungu Akuongoze..zaidi lower your expectations.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kijana masikini aliyekesha internet cafe kwa siku mbili mfululizo kuhakikisha taarifa zake za maombi ya ajira anazi-upload OTEAS kwa umakini asikosee, leo kakosa ajira, na anaambiwa hao waliopata ajira walikosea kujaza form, TAMISEMI wakawarekebishia na kuwapa ajira!

Watu hawa wanamjibu hivi huyu kijana wakifikiri atawaelewa kweli?

Yaani nimekesha kuhakikisha taarifa zangu sahihi zinaenda lakini anaeajiriwa ni yule aliyetuma taarifa za uongo? SERIOUS? SERIKALI YA WANYONGE?

Hakuna mtu kutoka familia bora anayeweza kuacha starehe nyumbani kwao na kwenda kufundisha shule za umma tena bila malipo yoyote ama kwa kulipwa 30k per month, most of volunteers ni watoto wa maskini wasiona koneksheni yoyote, hawana cha kufanya ndio wameamua angalau kwenda kuwasaidia wadogo zao walioko mashuleni japo kwa shida tena bila malipo yoyote, kwa serikali makini hawa vijana walitakiwa kutazamwa kwa jicho la kipekee sana, badala ya kukaa vijiweni kuilaumu serikali kwa kutotoa ajira za kutosha wao wameamua kuisaidia serikali na Taifa lao

Leo iweje tunawaona kama takataka na kuamua kuingiza watu tunaojuana nao ama Tamisemi kuthamini zaidi rushwa na kuwaacha vijana hawa wakiendelea kuteseka mtaani? Mmethamini hao ambao hata hamjui walikuwa wakijihusisha na mambo gani huko mtaani mnawaacha hawa ambao waliamua kuendeleza taaluma zao na kukuza zaidi uwezo wao wa kuderiver materials kwa wanafunzi?

Binafsi pia nimuombaji, mfumo wa OTEAS ilikuwa ukikosea ku-upload informations zako haukuruhusu uendelee na hatua inayofuata mpaka utakaporekebisha makosa, swali ni je, hao wahitimu wa 2017, 2018 & 2019 waliomba kupitia mfumo gani? (HAPA KUNA HARUFU YA RUSHWA)

Leo ndio ile siku, vijana masikini walioamua kujitoa kulitumikia taifa lao kwa kujitolea kwenye mashule ya umma wataanza kupokea watoto wa vigogo na wakurugenzi makazini kwao wakiwa wameajiriwa tayari, hawa volunteers waliotiwa moyo na TAMISEMI kimagumashi, sijui wataendelea kujitolea kwa moyo uleule? Ama watakata tamaa?

Maafisa elimu waliokuja kwenye mashule yetu na kutukuta vijana tunajitolea huku tukiwa tumechoka, hali mbaya, na kutuahidi kuwa tusife moyo serikali yetu haitatutupa mkono kwa fulsa yoyote itakayotokeza, watakuja tena?
Wakija watatueleza nini tena?

Je, vijana tutaendelea kuiamini serikali hiii?

Je, kama tutapoteza imani juu ya serikali na viongozi wake nini kitafuata?

VIONGOZI
Mmewahi kujiuliza mnajenga attitude gani kwa vijana dhidi yenu?

Mnafikiri hiki mnachokitengeneza sasa kitaleta positive ama negative impacts kwa Taifa siku za usoni?

Leo hii kama mmetufuata vituoni kwetu nakutuahidi mtatupa kipaumbele na zaidi mkachukua na taarifa zetu, na sisi tukawaeleza mama zetu kuwa serikali imesema haitatuacha fulsa zikitokea, haya maumivu tuliyonayo sisi wazazi wetu na jamii zetu yataisha tu hivi hvi? Hayatakuwa na madhara yoyote?

Mimi binafsi kunidanganya sio tatizo, tatizo mmemdanganya mpaka mama yangu aliyeuza nguo zake ili nisome, leo ananiuliza namwambia nimekosa ajira, ananiuliza tena kwani serikali si ilisema mtaajiriwa kwanza? Nikakosa jibu, mama katoa chozi

Mimi ninauvumilivu wakushuhudia mama yangu akilizwa na serikali hiii?

Any way. Newton's third law of motion "To every action there is an equal and opposite reaction".

MUNGU WETU NI MWEMA.
Mkuu,Pole ila najua hataka ukipewa nafasi ya kuzaliwa na kuishi tena utachagua hali hii hii.Na utakubali kupitia haya haya.
 
Unaulaumu mfumo, serikali, umaskini wako au aliyeajiriwa???!
Af kila aliye apply alikuwa ana uhitaji kwahyo ulitaka upate wewe wengine wakose?
Pambana na hali yako. Subiri hizo 5000 zilizobaki ndo za maskini waliotuma taarifa kwa usahihi.
Sawa mwalim tajiri namba moja
 
Hoja alizotoa hata
Sawa mwalim tajiri namba moja
Li
Duuh..ukweli mchungu.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Hoja alizotoa hata hazina mashiko. Hivi kutuma taarifa kwa usahihi kunahitaji kukesha two nights cafe!!??.
Ajira zilitangazwa kwa watu wenye taaluma au kwa maskini???
Mfumo wa kuomba ajira haukuwa perfect ndo maana na wenyewe wamejaribu ku adjust fairness ili ku clear makosa ya mfumo. Trust me or not, kama kuna mtu alijaza taarifa sahihi kwa 100% bas hawafiki 5% tukianza tu na DoB ambapo ilikuwa inajiadjust yenyewe kurudi nyuma siku moja, yaani ukiweka ulizaliwa tar 21 yenyewe ilikuwa inajiweka tar 20. Ili ioneshe umezaliwa 21 ni lazima uweke tar 22, Sasa yeye anasemaje amekesha siku mbili kuweka taarifa kwa usahihi??!

Akubali tu amekosa na awe mpole maana kulikuwa hamna namna ya wote walio apply kupata. Sio kuleta vigezo vya umaskini na kukesha ambavyo havikuwepo kwenye system.
 
Back
Top Bottom