hayaland
JF-Expert Member
- May 4, 2012
- 712
- 399
Kama tujuavyo Zanzibar kama nchi yenye serikali yake kamili, inazo serikali zake za mitaa na zinajitegemea zikiongozwa na rais wa Zanzibar. Rais wa Zanzibar anatoa maelekezo na maagizo kwa halmashauri hizo. Rais wa jamhuri ya Muungano hana nafasi kutoa maagizo na maelekezo katika Halmashauri za Zanzibar akifanya hivo jua kuwa anaziagiza halmashauri za Bara tu.
Mfano Mh rais alivyotoa maagizo kwa halmashauri zote nchini kutenga fedha za kununulia dawa ya kuua vimelea vya malaria (larvacides) na alitoa muda kwamba halmashauri zote kwenda katika kiwanda kinachotengeneza dawa hizo kununua dawa hizo mara moja. Agizo hili lilizihusu Halmashauri zote za Bara tu.
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka visiwani anayo mamlaka ya kaziagiza Halmashauri za Bara kutekeleza maagizo ya rais huku hana mamlaka ya kaziagiza halmashauri za visiwani kutekeleza maagizo hayo.Rais huyu anayetoka visiwani anajua vyema changamoto zinazokabiri Halmashauri za Bara?
Je anaweza kuwa na nia njema ya kuhakikisha halmashauri za Bara zinapiga hatua? Mie siamini kama rais huyo anaweza kutoa maelekezo swahihi kwa Halmashauri asizozijua vyema.