Inauma sana Rais wa Zanzibar akafanya maamuzi na maelekezo katika Halmashauri za Bara

hayaland

JF-Expert Member
May 4, 2012
712
399
Kama tujuavyo Zanzibar kama nchi yenye serikali yake kamili, inazo serikali zake za mitaa na zinajitegemea zikiongozwa na rais wa Zanzibar. Rais wa Zanzibar anatoa maelekezo na maagizo kwa halmashauri hizo. Rais wa jamhuri ya Muungano hana nafasi kutoa maagizo na maelekezo katika Halmashauri za Zanzibar akifanya hivo jua kuwa anaziagiza halmashauri za Bara tu.

Mfano Mh rais alivyotoa maagizo kwa halmashauri zote nchini kutenga fedha za kununulia dawa ya kuua vimelea vya malaria (larvacides) na alitoa muda kwamba halmashauri zote kwenda katika kiwanda kinachotengeneza dawa hizo kununua dawa hizo mara moja. Agizo hili lilizihusu Halmashauri zote za Bara tu.

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka visiwani anayo mamlaka ya kaziagiza Halmashauri za Bara kutekeleza maagizo ya rais huku hana mamlaka ya kaziagiza halmashauri za visiwani kutekeleza maagizo hayo.Rais huyu anayetoka visiwani anajua vyema changamoto zinazokabiri Halmashauri za Bara?

Je anaweza kuwa na nia njema ya kuhakikisha halmashauri za Bara zinapiga hatua? Mie siamini kama rais huyo anaweza kutoa maelekezo swahihi kwa Halmashauri asizozijua vyema.
 
Hakuna ila mtu kutoka visiwani kufanya maamuzi ya ndani ya Bara siamini
 
Inawezekana maana yeye ndie makamu wa kwanza wa rais na ataagiza kama makamu wa rais na siyo kama rais
 
Hakuna katiba uliyoshindwa kama kitu kinachoitwa katiba ya Tanzania; sijui viongozi wetu wanajisikiaje wanapoibeba kwenye koti.

Yaani ukitoka nje ya nchi unsikia MTU kutoka Unguja anajitambulisha kua yeye ni Mzanzibari alafu MTU kutoka Kahama anajitambulisha kua yeye ni Mtanzania; ukishika na kuangalia makabrasha zao yaani kichefuchefu......kama hamtaki kuifuta Zanzibar basi tambueni pia Tanganyika.
 
Mwaka 1890 Zanzibar ilikuwa Empire of Zanzibar
Mwaka 2017 Zanzibar imekuwa Manispaa ya Mji mdogo wa Zanzibar

Hongera zao wa Znz kwa Mafanikio

Kwa Mtazamo wangu naamini ingefaa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar nayo ingejumuishwa kwny Tamisemi iungane na Serikal za Mitaa za Bara!
 
Hakuna katiba uliyoshindwa kama kitu kinachoitwa katiba ya Tanzania; sijui viongozi wetu wanajisikiaje wanapoibeba kwenye koti.

Yaani ukitoka nje ya nchi unsikia MTU kutoka Unguja anajitambulisha kua yeye ni Mzanzibari alafu MTU kutoka Kahama anajitambulisha kua yeye ni Mtanzania; ukishika na kuangalia makabrasha zao yaani kichefuchefu......kama hamtaki kuifuta Zanzibar basi tambueni pia Tanganyika.
Si mlimpiga Mzee Warioba makofi?
 
Kama tujuavyo Zanzibar kama nchi yenye serikali yake kamili, inazo serikali zake za mitaa na zinajitegemea zikiongozwa na rais wa Zanzibar. Rais wa Zanzibar anatoa maelekezo na maagizo kwa halmashauri hizo. Rais wa jamhuri ya Muungano hana nafasi kutoa maagizo na maelekezo katika Halmashauri za Zanzibar akifanya hivo jua kuwa anaziagiza halmashauri za Bara tu.

Mfano Mh rais alivyotoa maagizo kwa halmashauri zote nchini kutenga fedha za kununulia dawa ya kuua vimelea vya malaria (larvacides) na alitoa muda kwamba halmashauri zote kwenda katika kiwanda kinachotengeneza dawa hizo kununua dawa hizo mara moja. Agizo hili lilizihusu Halmashauri zote za Bara tu.

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka visiwani anayo mamlaka ya kaziagiza Halmashauri za Bara kutekeleza maagizo ya rais huku hana mamlaka ya kaziagiza halmashauri za visiwani kutekeleza maagizo hayo.Rais huyu anayetoka visiwani anajua vyema changamoto zinazokabiri Halmashauri za Bara?

Je anaweza kuwa na nia njema ya kuhakikisha halmashauri za Bara zinapiga hatua? Mie siamini kama rais huyo anaweza kutoa maelekezo swahihi kwa Halmashauri asizozijua vyema.
Kwa mtu makini hawezi kuelewa huyo Rais wa jamhuri yauungano wa Tanzania kutoka visiwani ni yupi kwani hatuna rais wa aina hiyo.
 
DAB alitoka bara akaenda visiwani tena mkoa wa mwengine kuchukua mchango wa mil.50 ambazo hata wao wazanzibar walikuwa na tatizo la mchango kipibdi cha mafuriko huko..
 
Hakuna ila mtu kutoka visiwani kufanya maamuzi ya ndani ya Bara siamini
Then naunga mkono hoja yako ambayo nafikiri inamaanisha kwamba ni wazanzibari wachache wenye mapenzi ya kweli na Tanganyika au Muungano
 
Kwani kuna kipengele cha katiba kilichovunjwa?
Hata kikivunjwa watafanywa nini? Mbona huyu wa Tanganyika ameshavunja katiba na hakuna lolote analofanywa. Kwa nchi za kiafrika rais huwa ndiye katiba yuko huru kufanya lolote analotaka na akashangiliwa. Na rais ndiye huonekana ndiye mwenye akili kuliko watu wote katika nchi
 
Mkuu wanadai ni nchi,hata ukienda kwenye maandiko, wanadai ina sifa zote za nchi kama vile bendera, rais,katiba,mipaka, baraza la mawaziri.
 
Je anaweza kuwa na nia njema ya kuhakikisha halmashauri za Bara zinapiga hatua? Mie siamini kama rais huyo anaweza kutoa maelekezo swahihi kwa Halmashauri asizozijua vyema.
Kutoka bara haimaanishi unazijua halamshauri zote za Tanzania bara.
Rais ana mifumo mingi ya kupata habari popote pale atakapo.
Ukishakuwa mtanzania ni sifa mojawapo ya kuwa Rais wa JMT,bila ya kujali unatoka upande gani wa jamhuri hii
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom