Inauma sana nakuwa mkubwa halafu nazidi kuwa maskini

Tulia dogo tupo bize na kuhamisha wanyama kwenda burigi Hizo kelele zitafanya wanyama wachanganyikiwe
Yaani zamani miaka ya nyuma nilikuwa siwazi kabisa Kama nguo nimeipenda Basi natoa hela nainunua nakumbuka nilikuwa napenda Sana mashati na suruali za dickers yaani haipiti week nishanunua nguo mpya

Leo hii namaliza hata miezi miwili sijanunua nguo.Mwanangu wa kiume Mara ya mwisho kumnunulia kiatu ni mwezi February mwaka huu.Yaani nakuwa mkubwa nazidi kuchakaa nazidi kuchoka nazidi kufilisika

Halafu watu wamekaa miaka zaidi ya 20 umasikini haujaisha?Are we serious?

Naona Kama tunaleta mzaha.Jamani wakubwa huko tufikirieni na sisi basi maana tumeanza kuwakimbia mpaka wake zetu sasa hivi hakuna tena mapenzi ni mawazo juu ya mawazo.

Pesa zimeenda wapi mbona kama ni kazi tunafanya biashara lakini hazinunuliki watu hawana hela kila mtu anakwambia hana hela.

Yangu ni hayo tu kwa leo.
 
Back
Top Bottom