Inauma sana likikukuta hili, mama mjamzito anateseka

April26

JF-Expert Member
Jul 14, 2020
1,403
2,118
Wataalam wa afya nawasalimu.

Naomba niende kwenye mada moja kwa moja, kuna mtu nae mfahamu mke wake ni mjamzito. Wakati anaanza clinic dispensary moja ya serikali hapa Dar alipimwa kila kitu ikiwemo na group la damu na kukutwa na group "O negative".

Kilichofata hakuambiwa kuwa hilo group lina changamoto gani tofauti na magroup mengine ya positive, nadhani walisahau au ufanisi ni big ZERO, hivo aliendelea kuhudhulia clinic pale dispensary had akafikisha mimba ya miezi 8, siku ya mwisho anarudi hapo dispensary ndo nesi mmoja akagundua huyu mtu anatakiwa achomwe sindano ya Ant-B (wataalamu watakuwa wamenielewa, alikuwa hajachoma ) lakini ikumbukwe baada ya kujifungua atachoma tena nyingine ili kumrinda mtoto na hivo nesi alipojuwa hili alishikwa taharuki na kumwambia aondoke muda ule ule awnde kuchoma hiyo dawa hapo zile week 27 zilikuwa zishapita. Alipofika kule walimshauri aje kuchoma baada ya kujifungua maana ni mimba ya kwanza haina shida sana.

Narudi nyuma kidogo, basi, ikabidi atoke pale apewe rufaa kwenda hospital kubwa ya serikali ili hudhurio la mwisho clinic afanyie huko na atajifungulia huko, taarifa zote mhimu za client walizitoa na akaenda nazo.

Ameenda kapewa makisio ya tarehe 22/4/21 hakujisikia uchungu, akaambiwa arudi nyumbani ikifika 24/4/21 hajaona dalili zozote aende 28/4/21 na kweli alihudhuria hiyo 28/4/21 akafanya utra sound na kupima kiwango cha damu.

Ikaonekana mtoto yuko poa ila ni mkubwa approximately 4 point 8 weight. Na damu iko 9 na point kadhaa japo mwanzo ilikuwa 11 na points.

Hivo kwa ushauri wa madaktari akalazimika afanyiwe operation kama emergency case, na kuongeza kuwa njia yake haijafunguka, na maji ndani ya mfuko wa uzazi yamepungua jambo linaloweza kuleta shida kwenye kujifungua kawaida,kapewa wodi 28/4/21 hadi naandika huu uzi hajafanyiwa na anazuiwa kula kwa kudai kuwa muda wowote anaweza fanyiwa huduma

Hadi usiku wa kuamkia leo 1/5/21 amepelekwa chumba cha upasuaji akafanyiwa hatua za mwanzo bahati nzuri mmoja wa wahudumu akagundua group la damu la client wao ni O negative, halafu damu iko 9 na pengine imepungua maana tangu 28/4/21 hapati mulo sahihi wala hamezi dawa za kuongeza damu.

Wakaahirisha huduma baada ya kutafuta group hilo la damu usiku wa leo hapo hospital kwao wakakoswa, napoandika hapa wamemrudiaha wodini wanatafuta hiyo damu.

Wataalam kiukweli binafsi najiuliza hizo taarifa za clients wanazoandika hawazipitiii??? Au wanafanya kazi kwa mazoea? Au kitaalam hii ya kuchelewesha ina mantiki kitabibu?

Binafsi sio mtalaamu wa afya ila kwa hili naona kabisa huduma zetu za uzazi baadhi ya hospital hazizingatiwi ipasavyo.

Mjamzito analia njaa hadi machozi analalamika mtoto anafurukuta balaa tumboni. Je hii haiwezi kumdhuru mtoto ?

Nafahamu huwenda wengi wetu yunaofata hizi huduma kwenye hospital zetu tena hizi kubwa sio KWA SABABU TUNAZIPENDA SANA, BALI KWA SABABU TUNAANGALIA KIPATO NA KUMUDU MALIPO YA HUDUMA ila kiwastani huduma kwa baadhi ya watumishi wa afya ni MBOVU.

Naamini huyo mmoja anaepitia mateso hayo ni sample ya wengi wasio kuwa na sauti ila wana maumivu makali sana.

Mungu wasaidie. Ngoja niishie hapa na ninyamaze.
 
Amana mkuu.
Mkuu kwa hosptari hizi za serikali hizi za serikali usipojiongeza itakuwa tatizo hilo group hadimu sana lkn halikosekani madaktari na manesi wa hosptari za serikali hawana utu
Jiongezee kidogo

Na ukipata uhakikishe kweli ni group hilo uwaulize mara 2 2 waliwahi mtia mgonjwa wetu group tofauti kisa washachukua bakshishi na hilo ikawa matatizo makubwa
 
Wataalam wa afya nawasalimu.

Naomba niende kwenye mada moja kwa moja, kuna mtu nae mfahamu mke wake ni mjamzito. Wakati anaanza clinic dispensary moja ya serikali hapa Dar alipimwa kila kitu ikiwemo na group la damu na kukutwa na group "O negative"...
Group yake O negative ni changamoto sana, (ndugu zake wa karibu wangechangia ingekuwa rahisi kidogo kupata hilo group). Lkn kuna vitu vingine sio rahisi kama tufikiriavyo.

Procedure hiyo ingawa ni ya kawaida, ni vema kuwa na standby damu in case anything happens. Suala la blood products scarcity sio la kulaumu watoa huduma wa afya mahospitalini.

Since Corona watu wachache sana wanachangia damu mahospitalini. Lkn pia upande wa afya, ktk sehemu ambapo huduma zimeboreshwa sana ni huduma za wajawazito na ndio maana vifo vitokanavyo na ujauzito vimepungua sana. I'm sure she'll be just fine..
 
Mi nilisemaga sitamani kua daktari maana ntamkosea Sana Mungu kwa sasa udaktari sio wito ni kozi za kibiashara
Bora uligundua hilo, ni wachache wanaweza hilo.

Mimi naona sio kwa sasa yaani tanzania asilimia kubwa wanaroho mbaya, tofauti Na wenzetu Magharibi.
 
Back
Top Bottom