Inauma sana kumpenda mtu asiyekupenda

Course Coordinator

JF-Expert Member
Jul 27, 2019
1,681
3,065
Mapenzi ni kama mchezo wa kandanda unaombea team yako ishinde na wapinzani wako wanaombea team yako ishindwe pia.

Umemtumia mtu text lakini hajakujibu, meseji imepokelewa lakini hajajihangaisha kukujibu. Ukaamua kuiweka simu pembeni kuendelea na mambo mengine baadae unarudi bado unaona kimya hajakujibu.
Lakini ukitizama Watsapp unaona yuko online busy akichati na kubadili DP na status.
Unabaki ukijiuliza ana chat na nani mpaka asizione meseji zako na kuzijibu?

Unabaki ukiendelea kujiuliza umemkosea nini?
Unaanza kujiambia kuwa labda amekuchoka. Inauma sana kupuuzwa na mtu umpendae kwa moyo wote.
Je unajua kuna uwezekano nae anapitia kipindi kigumu kama hicho? Sawa anaweza akakwambia anakupenda au amekumiss, lakini anae mtu mwingine ambae anampenda haswa.

Unavyohangaika kumpigia, kumtumia meseji na asizijibu nae aweza kuwa anafanyiwa hivyo na ampendae.
Anamtumia meseji, anamcall lakini nae simu zake hazipokelewi kama wewe. Nao wanapitia magumu kama wewe!
Kufikia hatua hii, unafikiri kukata tamaa juu ya huyo mtu lakini inakuwa sio rahisi. Unafikiri kumuacha huyo mtu, kumblock hata kum "unfriend" fb lakini bado unaona moyo wako bado unampenda. Na unamatumaini ipo siku atarudi.

Kila muda unapotaka kuichukua simu yako unaomba Mungu ukute meseji yake lakini ukishika tu simu unakuta meseji ya TIGO VODA ,HALOTEL AU AIRTEL wakikukumbusha kulipa deni ulilokopa kwa ajili ya muda wa maongezi ,mbaya zaidi deni hilo ulikopa umpigie au unapata sms mteja mwenye namba hii alijaribu kukutafuta lakini hakufanikiwa ,jaribu kuwasiliana nae...unakuta namba ni yake unampigia anakwambia ilijibonyeza .
Unakata kwa sababu hauna la kumwambia ,unakaa unaanza kuandika sms na kuzifuta ,unaandika unafuta ..unamwambia usiku mwema anakujibu unalala muda sa hivi.

Unajikuta unaichukia simu yako na unamchukia kila mtu anaye kuongelesha, unatamani uipasue simu vipande vipande!
Lakini kwanini ifikie hatua hiyo? Kwa hali kama hiyo inaonesha kabisa wewe hupendwi labisa. Kwanini upoteze muda wako kumpenda mtu asiyekupenda?

Usimlazimishe akupende, wewe sio mzee kiasi kwamba huwezi kupata mtu mwingine. Usijipe stress kwa asiyekupenda kuwa na ujasiri wa kumuacha aende na wewe enenda na maisha yako.
Hata iwe vipi maisha lazima yaendelee

Maisha ya mapenzi ni mzunguko ,kula ,ishi kwa raha .

Epuka strees

1+1=11
 
Djamaa yangu yuko Kahama kafirisiwa na muke tena muvhepuko ya mutu, djamaa snstsks kumuuuaaa. Ogopeni wanaewake

Don't make a promise you can't fulfill...
 
Back
Top Bottom