fredj2
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 235
- 93
Umemtumia mtu text lakini hajakujibu, meseji
imepokelewa lakini hajajihangaisha kukujibu.
Ukaamua kuiweka simu pembeni kuendelea na
mambo mengine baadae unarudi bado unaona
kimya hajakujibu.
Lakini ukitizama Watsapp unaona yuko online busy
akichati na kubadili DP na status.
Unabaki ukijiuliza ana chat na nani mpaka asizione
meseji zako na kuzijibu?
Unabaki ukiendelea kujiuliza umemkosea nini?
Unaanza kujiambia kuwa labda amekuchoka.
Inauma sana kupuuzwa na mtu umpendae kwa
moyo wote.
Je unajua kuna uwezekano nae anapitia kipindi
kigumu kama hicho? Sawa anaweza akakwambia
anakupenda au amekumiss, lakini anae mtu
mwingine ambae anampenda haswa.
Unavyohangaika kumpigia, kumtumia meseji na
asizijibu nae aweza kuwa anafanyiwa hivyo na
ampendae.
Anamtumia meseji, anamcall lakini nae simu zake
hazipokelewi kama wewe. Nao wanapitia magumu
kama wewe!
Kufikia hatua hii, unafikiri kukata tamaa juu ya huyo
mtu lakini inakuwa sio rahisi. Unafikiri kumuacha
huyo mtu, kumblock hata kum "unfriend" fb lakini
bado unaona moyo wako bado unampenda. Na
unamatumaini ipo siku atarudi.
Kila muda unapotaka kuichukua simu yako
unaomba Mungu ukute meseji yake lakini ukishika
tu simu unakuta meseji ya TIGO wakikukumbusha
kulipa deni ulilokopa kwa ajili ya muda wa
maongezi.
Unajikuta unaichukia simu yako na unamchukia kila
mtu anaye kuongelesha, unatamani uipasue simu
vipande vipande!
Lakini kwanini ifikie hatua hiyo? Kwa hali kama hiyo
inaonesha kabisa wewe hupendwi labisa. Kwanini upoteze muda wako kumpenda mtu asiyekupenda?Usimlazimishe akupende, wewe sio mzee kiasi kwamba huwezi kupata mtu mwingine.
Usijipe stress kwa asiyekupenda kuwa na ujasiri wa
kumuacha aende na wewe enenda na maisha yako.
Hata iwe vipi maisha lazima yaendelee.