Inauma: Ajali ya Karatu yasababisha mama kupoteza maisha kwa mshtuko

dimaa

JF-Expert Member
Jul 30, 2016
4,143
5,609
Habari zenu wakuu.

Katika tukio ambalo limeleta majonzi makubwa na mtikisiko kwa nchi, ni tukio la vifo vya wanafunzi takribani 33 wa shule ya Lucky Vincent ya mjini Arusha, la kusikitisha zaidi ni wanafamilia watatu kufariki dunia, wawili walikuwa ni mapacha na mmoja alikuwa akilelewa na huyo mama.

Kutokana na mshituko wa vifo hivyo mama naye kapoteza maisha alivyoskia tu wanawe wamefariki kwa ajali , majuzijuzi tu kampoteza mmewe. Hili ni tukio kubwa sana, hata mimi nimeumia sana, kila nikikumbuka tu machozi yananitoka, huruma zaidi ni kwa huyu mama kuwapoteza wanawe watatu ambao ndo alikuwa akiwaangalia kwa jicho la pili.

Allah awafanyie wepesi huko waendako.

Inauma sana.
 
Hivi kwenye majanga kama haya serikali kuwa inapeleka wataalamu wa kisaikologi?
Au wanaishia tu kutuma mameseji huko facebook na twitter?

Naskia kuna mama kafa kwa sababu ya mshtuko?
Kama ni kweli basi kuna walakini mkubwa huko serikalini.
Ushauri nasaha ni tiba moja nzuri sana
 
Daah, so sad!
Mama amekufa kwa mshtuko mkubwa was kupoteza wapendwa wake wote kwa pamoja..
Mungu azipumzishe roho za marehemu mahali pema pepon. Amen!
 
Machozi, machozi..... eeh Mungu haya yote yanatokea ili mapenzi yako yatimizwe na ukuu wa ujidhihirishe kwetu
RIP mama na watoto wako
 
Back
Top Bottom