Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,279
- 25,857
Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni mkuu wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu. Ndiye kiongozi wetu nambari moja wa nchi. Sisi watanzania tunapaswa kumuunga mkono Rais wetu Magufuli. Anachokifanya na Serikali yake kwa ustawi wa nchi yetu, anakifanya kwa maslahi yetu sote.
Rais anapoamua kwa maslahi ya Taifa, tumeamua kama Taifa na tunapaswa kupongezana. Rais anapoteua au kutengua, baada ya mchakato unahusisha vyombo vyetu mbalimbali vya kitaifa, ameteua au kutengua kwa niaba yetu sote watanzania. Tanzania ni nchi yetu sote tuliyopewa na Mwenyezi Mungu. Tunapaswa kumuunga mkono Rais na Serikali yake katika kuistawisha nchi yetu.
Rais anapofanya mema, kila mtanzania anafaidika. Rais anapofanya ya makosa, kila mtanzania ataguswa nayo. Ni wajibu wetu kukosoa kwa staha na kutoa suluhisho. Rais wetu si malaika, ni binadamu kama tulivyo sisi. Anapokosea katika kusema na kutenda, kama watanzania wazalendo wa nchi yetu, tunapaswa kusema kwa kutoa suluhisho ili makosa yasijirudie.
Sisi watanzania ndio mzizi wa mamlaka yote kikatiba. Rais wetu tunaomba awe anatusikiliza. Tunapotoa maoni yetu kwa mustakabali wa Taifa letu na kwa mujibu wa Sheria, Mhe. Rais asikilize wananchi wake kwakuwa ndio hao tu alipewa na Mwenyezi Mungu awaongoze kama Rais wao. Wananchi wanapokuwa na sababu za kukubali au kukataa jambo wakiwa na sababu za kutosheleza, wanapaswa kusikilizwa.
Nchi hii ni yetu sote, inaponeemeka tunaneemeka sote. Tunapoheshimiana, tunapokosoana kwa staha, tunasikilizana na kukubaliana kutokukubaliana kwa hoja na kwa mujibu wa Sheria na tunapojadiliana kwa kuweka maslahi mapana ya Taifa mbele, tunamtendea haki Mama Tanzania tuliyepewa bila kuomba kuwa nchi yetu.