Inatisha!

Natamani watanzania wote tungekuwa watu jasiri kama wanaTarime, dawa ya moto ni moto.
 
Hivi jamani ni kweli kabisa inawekana kura 20,316 out of 90,789 zinaharibika inaingia akilini kweli? Kituo kina wasimamizi waliopatiwa mafunzo wanatoa out put ya 20,316 zimeharibika.

Hii inatisha, kama tutaruhusu mambo namna hii......... sijui tutakuwa tunanuia kufika wapi.
 
Watz hakikisheni majina yenu yapo vituoni ili tuone ccm watatokea waapi. Nahisi majina ya wapiga kura hayatakuwepo vituoni na mwisho wake hatutakuwa na amani.
 
Duh kweli Tanzania ina unyanyasaji. Hawa jamaa hawakubali kushindwa, ila najua Tarime waliweka nguvu nyingi sana kwa kuwa ilikuwa inapiga kura peke yake.. ila mwezi huu itakuwa nchi nzima hawatokuwa na nguvu ya kunyanyasa hivyo... CCM wabaya sana!
 
Kweli ukiangalia hii kitu, inasisimua na kujenga uzalendo!
Hv hawa wenzetu wamefundishwa na nani ujasiri huu?
Kwanini wengi wetu tunashindwa?
Ama kweli ccm choka mbaya!
 
Aiseee Inasikitisha sana Lakini kwanini nyinyi askali mtumiwe kwani nyinyi si watanzania?
 
Nimenunua laptop nitatembelea vijiji vingi kule kyela nikawaonyeshe ujasiri wa wanatarime muone moto utakaowaka huko.Nitakuwa nawapa update kila mara.
 
- Hapa waandishi wa habari wanastahili pongezi sana....wamefanya kazi yao kwa ujasiri.

- Wana tarime ni mfano wa kuigwa, wao wana wapima viongozi waliowachagua kwa vigezo makini sana i.e mfumuko wa bei za bidhaa, mazingira duni ya kufanyia biashara.

- Naamini ni kutokana na Tarime ndio sababu mwaka huu Makamba, Msekwa hawasikiki kabisa...Ridhiwani na Mama JK wameamua kukampeni wenyewe.

- Mageuzi ya kweli Tanzania (pamoja na sababu nyingine) yanakwamishwa sana na wachache wanaojiona wajanja wenye elimu bila kuelimika waliopo mijini kama Dar es salaam.

- That said, hii documentary haitoi fursa ya kuona picha halisi...watengenezaji wake wameipendelea Chadema.
 
Hivi ndo vitu Marehemu Wangwe alikuwa anawaeleza CHADEMA,tuimalishe mashina,matawi na majimbo,vyama vijengwe kuanzia kwenye vijiji..pumbavu pesa inaliwa Makao makuu...
 
Tarime tumeanza je wewe ulieona hii Documentary umechukua uamuzi gani ndugu wametolewa jicho,Tanzania imegeuka Baghdad jamani....ewe CCM,ewe makamba,ewe kikwete huoni aibu?unadhani utaishi milele?jicho la mtu gharama yake kubwwa kwa mungu,ana watoto kama wewe,ni baba kama wewe Kikwete,kwa sababu kataka maendeleo unamtoa JICHO?Kwa sababu anataka CHADEMA anapigwa risasi ya Mguu?Kwa sababu anataka ukombozi unamnyima haki yake?CCM wakati wako umeisha ndugu....
 
Hii inatisha na hatutaki tufike hapa... Video kama hizi ni propaganda chafu sana za watu wasioitakia mema demokrasia.

Video vya namna hii vinapenyezwa na mafisadi ili uchaguzi wa 2010 usimamiwe na JWTZ na ili kura zichakachuliwe kulingana na matakwa ya watawala... hii ni njama ya CCM na wametumia nembo ya CHADEMA kwa makusudi, ili kusudi chadema kionekane chama cha fujo na kisichohubiri amani. Hakuna Mtanzania hata mmoja anayetamani maisha ya Tarime, ni maisha ya hofu na huu ni mtaji mkubwa wa mafisadi kubaki madarakani, wanaanza kuwahubili watanzania kuwa Chadema ni cha fujo na hakistahili! WASHINDWE na WALEGEEE
 
Nimenunua laptop nitatembelea vijiji vingi kule kyela nikawaonyeshe ujasiri wa wanatarime muone moto utakaowaka huko.Nitakuwa nawapa update kila mara.
Ukifika Kyela upload kwenye zile komputa za Mwakalinga alizoahidi nafikiri zitakuwa tayari zimeshafika.
 
Mi nisha anza mazoezi muda mrefu. Mi naapa kufia watoto wangu. Sitakubali kuburuzwa, naapa mi ntakuwa mstari wa mbele, mafunzo ya JKT walitoa wenyewe nami nilikuwa kinara wa kwata, msidhani tunatania!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom