Inasikitisha, Tukuyu Stars ipo daraja la nne. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inasikitisha, Tukuyu Stars ipo daraja la nne.

Discussion in 'Sports' started by Nazjaz, Apr 30, 2011.

 1. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  Timu hii kali ya Tukuyu Stars ilishiriki kwa mara ya kwanza ligi kuu mwaka 1986 na kuchukua ubingwa.
  Timu hii ilitisha bara na visiwani, lakini leo tunapoongea haya inashiriki ligi daraja la nne na inataka eti ipande daraja. Kikubwa na kizuri zaidi bado ina ndoto za kucheza ligi kuu.
   
 2. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ndio mpira huo mama.
  Hata maisha kwa ujumla kuna kupanda na kushuka
   
 3. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Niliposoma post yako nimekumbuka timu kama nyota nyekundu, RTC Kagera, Sigara, Pan African nk na enzi za kusikiliza matangazo ya mpira ktk Radio Tanzania, those days dah
   
 4. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,496
  Trophy Points: 280
  Duuh! So sad. Hakuna timu imewahi kupendwa Mbeya kama 'Banyambala', hadi kina mama walikuwa wanaenda uwanjani kuangalia mazoezi (uwanja wa mpira tukuyu mjini, karibu na stendi) na wakati wa mechi sokoine. Hizo ni enzi za kina 'Kaka' ambaye alikuwa mmoja wa wafadhili wa hiyo timu. 'Banyambala' ndo timu kongwe ya wananchi, acha hii prison ya serikali.

  Ghafla, nimeikumbuka pia MECCO! Enzi za kuruka ukuta wa uwanja wa sokoine na raha nyingine ya uwanja wa sokoine kipindi hicho ni kwamba ukiwa nje unaweza kuona nusu uwanja muda wote. Machokora wa Isanga na ubabe wao, almanusura wanitoe kafara kwa kosa la kumwambia mmoja wao asigeukegeuka, ananizuia kuona mpira, nikaviziwa mpaka lift valley hotel mie sina habari. Watu wazima waliniokoa. Kipindi hicho Yanga akija kucheza na Banyambala inakuwa mechi kali balaa, kulikuwa na upinzani mkali sana tofauti na leo ambapo upinzani hasa ni simba na yanga. Hakuna tena 'TP Lindanda' ya masatu na john makelele 'zigzag', wala si majimaji ya celestine sikinde mbunga.
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,184
  Trophy Points: 280
  Mungu aisadie. Safari ya kutoka daraja la nne hadi la ligi kuu ni ndefu sana.
  Bora timu haijafa.
   
 6. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  kuna siku pale uwanjani watoto wa Isanga walipigana na wa Nonde, balaa lake likachafua mji mzima.
   
 7. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Dah Mkuu umenikumbusha mbali sana. Enzi za Mecco na Tukuyu Stars. Those were the days. karibu kila mkoa kulikuwa na timu ligi daraja la kwanza except kama sijakosea Mara, Rukwa, Singida, Pwani na Lindi. Wakati mpira ulikuwa balanced. Mambo yalianza kuharibika pale simba na yanga walipoanza kununua wale wachezaji wazuri na kuwalundika Dar. Inawezekana Dewji na Gulamali walituharibia mpira kwa pesa zao.
   
 8. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  Maponjoro ni waharibifu daima, huja kama malaika wa nuru kumbe ni mashetani kabisa.
  Ona manji alichoifanya yanga
   
 9. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  kuna siku hizi yanga na simba zitakuja kuwa historia.
   
 10. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 418
  Trophy Points: 180
  dah! Poleni sana wana Mbeya,Tukuyu stars wana safari ndefu sana
   
 11. sekulu

  sekulu JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ubabe wa kipindi kile ulikuwaga noma,
  Nilishawahi kupita kwenye ule mtaro wa maji machafu, Kufika uwanjani nikakuta sehemu ya kutokea kuna FFU na Mbwa, alafu siwezi kurudi nyuma kwani kulikuwa kuna watu nyuma yangu na kupishana ni ishu, Jamaa akanambia "dogo lete hela au kama vipi naachia mbwa uhangaike nae" nilikua ninajiti Nikampa na akaniruhusu kuingia kazi ilikua kwa jamaa wa nyuma yangu hakuwa na hela ilikua noma, kula virungu mpaka noma!

  Memories
   
 12. sekulu

  sekulu JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 934
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ninachokifurahia ni kwamba Haijafa!
   
 13. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,354
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Dah Tukuyu Stars maskini, ilileta burudani kweli miaka ile, mara ya mwisho kuiona Tukuyu Stars ni siku ilipocheza na Yanga pale Sokoine,Yanga walishinda 2-0,la kwanza alifunga Mohamed Hussein na la pili alifunga Said Mwamba kama sikosei.
  Kipindi maisha ya soka yalikuwa sana redioni na uwanjani, natamani turudi kule tulikotoka!
   
 14. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,354
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Kweli kabisa, Ken Mkapa, Godwin Aswile na kuna mchezaji jina limenitoka wote walitokea Tukuyu Stars!
   
 15. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #15
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mkuu, umenikumbusha enzi hizo "nikiwa mtoto wa laini" sisi enzi hizo tulikuwa tunadandia tu kalandinga la ffu tunaingia kiulaini uwanjani, du nilitokea kuwa shabiki wa mpira ghafla kwa sbabu ya kuzamia kila mechi bila jasho. ni kipindi hicho ndo nilishuhudia kila timu live, na zilikuwa zinakuja mara mbilimbili, mara moja mecco na nyingine tukuyu, duh, kumbe na mimi nimetoka mbali eeeh?

  hahah nakumbuka mechi moja ya fungua dimba myambala mmoja anaekwenda kwa jina la ikupilika nkoba, alitia nuksi sana simba, bila kumsahau mzee mmoja mtata sana alikuwa maarufu kama "ahadi" alikuwa shabiki la kutupwa la banyambala! hahahaa , i like those old days!!
   
 16. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #16
  Jun 2, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Na zile timu za NMC na RTC?
   
 17. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,496
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa, lile karavati linatokea zilipokuwa zinapaki karandinga. Hata hivyo watoto wa kipindi hicho walikuwa hawaoni shida kuamkia central jumatatu yake..
   
 18. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,184
  Trophy Points: 280
  Ile ilikuwa ni raha ya kuangalia mpira enzi hizo.
  Unalikumbuka jukwaa la makaburu?
   
 19. Wakwetu03

  Wakwetu03 Senior Member

  #19
  Jun 4, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kaka unanikumbusha enzi za kupita fonka hahahaaa...ukishaingiza kichwa tu hurudi maana ukitaka kurudi nyuma yako kuna mtoto wa isanga na kiwembe anakuparuza unyayoni hahahaaaaa nimecheka hadi mbavu zinaniuma
   
 20. Wakwetu03

  Wakwetu03 Senior Member

  #20
  Jun 4, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  hahahaaaa....kule jukwaa la makaburu mtu ukiruka ukuta unakimbilia kule askari hakufuati
   
Loading...