Inasikitisha Sana - Kutoka Temeke Hospitali

Huwa hawakosi hawa. Wana bima za ARR, VX zao huwa zina majenereta, pia huwa wanatembea na ambulance ambazo ziko full equiped. Cha moto tutakiona sisi na jamaa zetu.

ambulance si huwa anatembea nay mmoja tu kwani wengine nao huwa wanatembea nazo?
 
Unaju siyo kila jambo linasababishwa na CCM,Hilo ni swala la utawala wa hospital ambao ni Non Poltical Administrative,Hivi ktk mafungu wanayopewa wameshindwa kununua jenerata au hata kuiombea fungu kwenye bajeti na pengine ukute fedha zilitengwa na wajanja hapo hospitali wametafuna.Watanzania tumeoza mtu anaenda kazini anawaza kuswaga mafungu ya fedha za umma .watanzania wote inabidi tubadilike ktk utendaji wetu wa kazi na tutangulize utu na kulinda rasimali fedha za umma na kuzitumia pale panapohitajika au pale ilipokusudiwa kutumika.

hapo kwenye red, kwenye hoja ya msingi uliyoinukuu CCM haijatajwa kabisa.

tunaongelea habari ya utawala, issue ya hospitali kukosa umeme na watu kufa, hata kama watendaji wa hospitali walifanya uzembe, ni vigumu kuiondoa dhamana ya kuhakikisha wagonjwa wanapata matibabu bora kutoka mikononi mwa serikali, haijalishi hiyo serikali ni ya ccm au ni ya chama kingine
 
Mkuu CCM kama chama kinachotawala kina sera na ilani zake ambazo hawa watendaji wanazifuata.. Ni juu ya CCM na Serikali yake kuhakikisha sera na iliani zinakuwa implemented.. Kama kuna sehemu ambayo utendaji unapwaya.. au hauendi sambamba na sera na ilani ya chama tawala.. basi ni juu ya chama tawala kwa kutumia serikali yake ku-replace hiyo sehemu ya utendaji.. ili iende sawa.. Kama haifanyi hivyo basi CCM haikwepi lawama ya kushindwa kuisimamia serikali yake..! CCM haitoki kwenye hili..
Haya ni majukumu ya kiutumishi na kiutendaji na watendaji hawajalishi wanatoka chama gani bali cha msingi ni watazania ambao hawatekelezi majukumu yao vyema.Kama watu wanaweza kuomba fedha za semina wanashindwa vipi kuomba fedha za jenereta.Hii hospitali ipo chini ya manispaa ya Temeke na wana vyanzo vingi vya mapato hivi viongozi wa hospitali wameshindwa hata kuomba fungu la jenereta.Hii ni failure kwao.
 
hapo kwenye red, kwenye hoja ya msingi uliyoinukuu CCM haijatajwa kabisa.

tunaongelea habari ya utawala, issue ya hospitali kukosa umeme na watu kufa, hata kama watendaji wa hospitali walifanya uzembe, ni vigumu kuiondoa dhamana ya kuhakikisha wagonjwa wanapata matibabu bora kutoka mikononi mwa serikali, haijalishi hiyo serikali ni ya ccm au ni ya chama kingine[/QUOTE
Nilijibu na kuzingatia hoja za wachangiajia wengine pia rejea bandiko 4 na 6.
 
kwa mjini wengi wameshaelimika, nguvu iongezwe vijijini kuikabili ccm.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom