Inasikitisha sana kama Serikali imeamua kuminya utumiaji wa Mitandao kwa njia hii

Wewe badala uchape kazi unataka kushinda mitandaoni ufuatilie umbea wa akina Wema Sepetu na Bugati, tena serikali inakosea sana, kifurushi cha chini kabisa ilibidi kiwe 10k na unapewa MB 200 tu! Wanaotumia mitandao kufanya biashara pekee ndiyo wangesajiliwa na kupewa vifurushi vyao maalum vya bei nafuu
Si unaona akili zenu zilivyo za hovyo? Nashindwa nianzie wapi kukujibu ila haujanishangaza kwa ulichoandika. Tulishajua tunadeal na watu wa aina gani wanaoendesha hii nchi.
 
Si unaona akili zenu zilivyo za hovyo? Nashindwa nianzie wapi kukujibu ila haujanishangaza kwa ulichoandika. Tulishajua tunadeal na watu wa aina gani wanaoendesha hii nchi.
Chapa kazi, acha kuwa busy na umbea wa akina Bugati mitandaoni
 
Nimefuatilia trend ya huduma za internet kwa mitandao kadhaa na kusema kweli hali ni mbaya na ya kusikitisha sana.

Kwa miaka kadhaa sasa, Serikali imejaribu mbinu mbalimbali za kubana uhuru wa watu kuongea. Siku za nyuma watu walikuwa wananyakuliwa kutokana na post zao. Lakini mbinu hiyo imeonekana kutofanya kazi sana.

Ambacho naona kinafanyika sasa ni kufanya gharama za vifurushi kuwa aghali mno. Nia ni kupunguza muda ambao watu watakaa kwenye mitandao, na mategemeo yao ni kuwa itasaidia watu wasifuatilie au kuchangia mijadala ya kisiasa inayoendelea.

Bei za vifurushi zimekuwa kubwa mno. Na si kubwa kwa sababu ya bei tu ya vifurushi lakini kiasi cha data ambazo unapewa kwa kila kifurushi kimepungua mno kiasi kwamba kwa vifurushi vingi, ndani ya siku moja mtu unalazimika kununua zaidi ya mara moja hata kama una matumizi ya kawaida tu.

Huu ni ushetani na sidhani kama utaleta faida wanazozifikiria. Sana sana inapunguza fursa za watu kupata elimu na kujifunza mambo ya msingi mitandaoni, kufanya biashara mtandao na hata kubadilishana mawazo na watu mbalimbali duniani ambayo mwisho wa siku yatasaidia kujenga nchi.

Wakiona wameshindwa huko kote watasema mtu haruhusiwi kununua zaidi ya kiwango fulani cha data kwa siku bila kibali maalumu! Tunapokwenda, ukiwa mnunuaji mkubwa wa bundle za internet unaweza kuwa suspect wa ugaidi!
Inauma sana.

Sisi watu wa sayansi tumekuwa tukijifunza mengi sana kupitia mitandao.

Wanataka tuwe na mawazo ya kijima
 
Kwa mfano sasa wamefungia mitandao ya ngono.Je hilo ni suluhisho??

Nadhani biashara ya kununua CD za ngono itarudi kwa kasi sana
 
Kwani nani kasema sio hitaji muhimu we tumbili jike..

Hiyo intaneti ukiitumia vibaya unaliwa.
Madikteta uchwara kama ninyi mko mstari wa mbele kupanga namna gani mtu atumie internet. Jaribu kuangalia faida zaidi katika uchumi wa taifa kuliko kuangalia faida za kulinda udikteta wenu. Tembeeni na mjifunze kuona faida za internet hivi leo. No wonder nchi inazidi kuwa maskini sababu ya wajinga wengi kama wewe kuinfluence uongozi wa taifa.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom