Inasikitisha sana! Jela maisha kwa kubaka, kuambukiza ukimwi

Shoo Gap

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
246
71
MAHAKAMA ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, imewahukumu kifungo cha maisha vijana wawili kwa makosa mawili ya ubakaji na kumuambukiza ugonjwa wa ukimwi mtoto wa miaka minne.
Akitoa hukumu hizo kwa nyakati tofauti, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ushindi Swalo, alisema mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa huku mmoja wa watuhumiwa hao akikiri kutenda kosa hilo la kumbaka mtoto wa miaka minne.
Katika tukio la kwanza, Mwendesha Mashtaka wa mahakama hiyo, Zephania Mnisi, alisema kuwa Desemba 21 mwaka jana, mshitakiwa Revocatus Mihayo (25) alimbaka mtoto wa miaka minne katika Kijiji cha Msonga wilayani Bukombe.
Mnisi aliiambia mahakama hiyo kuwa katika tukio hilo, Mihayo alikamatwa akiwa amempakata mtoto huyo mapajani, huku akimbaka na uchunguzi wa awali wa daktari ulionesha alikuwa ameharibika sehemu zake za siri.
Alisema wakati kesi hiyo ikiendelea na miezi kadhaa ikipita, mtoto huyo alifanyiwa uchunguzi wa daktari kwa mara ya pili na kubainika tayari ameambukizwa virusi vya ukimwi, shitaka ambalo liliongezwa kwenye kesi yake ya msingi ya ubakaji.
Katika shtaka la pili, Shija Marko (18) mkazi wa Lulembera anadaiwa kumbaka mtoto wa miaka minne baada ya kukutana naye shambani wakati mtuhumiwa akiwa na shughuli za kilimo.
Mwendesha mashtaka huyo aliiambia mahakama hiyo kuwa, katika tukio hilo mtoto huyo alipita shambani kwa Marko akiwa uchi wa mnyama jambo ambalo kijijini ni kawaida, lakini mshitakiwa alimshika na kumlaza kwenye matuta na kuanza kumbaka.
Hata hivyo mshitakiwa Marko alikiri papo hapo kutenda kosa lake na kumfanya hakimu Swalo, amhukumu kifungo cha maisha kwa kosa hilo.
Akitoa adhabu hizo kwa nyakati tofauti kwa washtakiwa hao wawili, Mihayo na Marko, hakimu Swalo alisema kwa kuwa washitakiwa wametenda makosa ya kubaka watoto chini ya umri wa miaka kumi, kifungo cha miaka 30 na viboko 12 kimejifuta na sasa watatumikia kifungo cha maisha ili liwe funzo kwa vijana wengine.

By Ally Lityawi, Geita
Tanzania daima
 
Poor little kids, watoto wetu wanahitaji sana ulinzi wetu dhidi ya hao wanyama watu....!!!!
 
tena hao inatakiwa wapewe na adhabu ya unyanyapaliwa, maana huko jela wataanza kugawa tigo kama chai, nawajua sana watu wenye visasi na roho mbaya
 
Je wazazi wa huyo mtoto nao wamepimwa na kuonekana hawana virus vya ukimwi???? Isije ikawa mtoto pia labda alizaliwa na virus.....
 
Duh jamani 2mrejee muumba dunia ndio ileeee ina kwenda, hivi mtt wa 4ano ananoga nini?
 
wangetakiwa wanyongwe hadi wafe.

Mkuu Mamndenyi: Watu wa haki za binadamu hawataki kabisa hicho kitu na wanapambana kuhakikisha kua katiba mpya inaondoa hukumu ya kifo. Kama ikifanikiwa basi watu watazidi kujichukulia sheria mkooni maana haiwezekani mtu ana virusi hala anamuambukiza mwanao kwa njia ya kubaka halafu baada ya miaka michache unamuona mtaani ukakubali yaishe kirahisi.
 
i have twins wa miaka mi4! both girls, nimeimagine kwa kuvuta taswira zao kichwani mwangu, nimelia!! MUNGU WETU MWEMA ULIYETUPA ZAWADI YA WATOTO, UWALINDE WATOTO WETU, AMEN!
 
Mkuu Mamndenyi: Watu wa haki za binadamu hawataki kabisa hicho kitu na wanapambana kuhakikisha kua katiba mpya inaondoa hukumu ya kifo. Kama ikifanikiwa basi watu watazidi kujichukulia sheria mkooni maana haiwezekani mtu ana virusi hala anamuambukiza mwanao kwa njia ya kubaka halafu baada ya miaka michache unamuona mtaani ukakubali yaishe kirahisi.

This is controversy.Huyu mtu ana VVU definately one day atakufa-na yeye analitambua hilo.Ukimnyonga leo,kwake yeye kifo ni kifo tu!Kwa maana nyingine utakuwa umemsaidia sana bila wewe kujua;na pengine ndilo lilikuwa lengo lake! Ni kweli kifo ni kifo,ila maumivu yanatofautiana.Kifo cha kunyongwa,marehemu anapata maumivu kwa sekunde chache tu,ila kifo cha kuumwa(HIV/AIDS),mgonjwa anapata maumivu kwa muda mrefu.

Siwanyanyapai watu wanaoishi na VVU,ila kwa huyu jamaa kuishi jela/kuugua HIV/AIDS ni adhabu kali kuliko kama angesaidiwa kunyongwa in few seconds.Huko atapata muda wa kutambua ukubwa wa kosa alilotenda.On the other hand kwa ile mijamaa inayochangamkia 0713 huko gerezani,jamaa ataigawia LUKU halafu mwisho wa siku inawaka yote,huh!

Anyway,kitendo alichotendewa huyu mtoto kinasikitisha sana kiukweli.Tunatakiwa kukilaanai kwa nguvu zetu zote.By the way,inaonekana teknolojia imepanuka sana siku hizi,maana kwa vipimo tulivyozoea,mtu anagundulika kuwa na VVU baada ya miezi 3!
 
Still I'm on contrary with that, siku hizi kuna ARVs tofauti na zamani ambapo watu walikua wanakufa kwa mateso sana. Siku hizi hata magerezani wanapewa chakula cha uhakika kwa watu wenye matatizo ya afya.
 
Mkuu ogopa theories maishani! Magereza we pasikie tu ndugu yangu. Ndio maana nikasema sio nia yangu kunyanyapaa wanaoishi na VVU,ila laiti ungekuwa unajua maisha ya watu wanaotumia ARVs halafu ukalinganisha na maisha ya magereza zetu,naamini ungekuja kivingine.Jaribu kuongea na wanaotumia dawa hizo,wakwambie masharti yanayoambata na matumizi ya dawa hizo,kisha uongee na watu waliopta kukaa jela wakupe picha halisi ya maisha ya mule ndani,then comment on the survival ya mgonjwa mwenye VVU mule ndani.

Anyway,hayo ni mawazo yangu tu na hayana effect yoyote kwenye kesi ya huyo jamaa.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom