Inasikitisha, Nimelia sana: Hii picha ya Dr Bashiru ni usaliti mkubwa, sikutarajia

nzagambadume

JF-Expert Member
Apr 9, 2018
2,430
5,769
Kwa kweli kama Watanzania hatutasimama pamoja na wazalendo wakubwa nchii hii yaani RC Gambo pamoja na RPC shana basi historia itatuhukumu sana

Jana nimeweka picha ya jaji namba 62 alivyopost picha ya kuidhalilisha nchi na kuhujumu uchumi leo tena tunaona Dr Bashiru kafanya the same, tunaomba Rais Magufuli uingilie kati uchukue hatua kali dhidi ya Bashiru na yule jaji ili umpe moyo kijana wako mpendwa ambaye unamuamini yaani RC Gambo katika kulipigania taifa

Jamani tupo kwenye vita ya kiuchumi,kupost haya mapicha yanayodaiwa kuwa ni barabara mbovu ni kuhujumu uchumi,haikubaliki, maadaui wanaweza wakajiona wameshinda kisaikolojia

NAUNGANA NA RC GAMBO NA RPC SHANA KATIKA KUISHINDA VITA HII YA WANAOPOST BARABARA MBOVU kama kweli ni mbovu si watoe taarifa kwa wahusika zitengenezwe?
Screen Shot 2020-02-19 at 2.54.55 PM.png
 
Kwanza hueleweki unalilia nini

Nchi ina changamoto ya barabara serikali ijitahidi kutatua changamoto kuliko kujisifia, kwani barabara zikiwa bora itakuwa siri? Si kila mtu ataona barabara nzuri?

Kuna maeneo serikali imejitahidi barabara ni nzuri na watu hupiga picha na kupost mbona hukuja kulalamika juu ya hilo?
 
Dah hivi inawezekana je mtu kama Bashiru anafanya kitendo kama hiki, ni ukatili kwa nchi yetu siyo kwa Gambo na Rpc peke yao.
Huu ni uhujumu uchumi ni kweli hauna jina lingine.

Hivi kaipost wapi au status yake ya whatsapp😀😀
 
Kwanza hueleweki unalilia nini

Nchi ina changamoto ya barabara serikali ijitahidi kutatua changamoto kuliko kujisifia, kwani barabara zikiwa bora itakuwa siri? Si kila mtu ataona barabara nzuri?

Kuna maeneo serikali imejitahidi barabara ni nzuri na watu hupiga picha na kupost mbona hukuja kulalamika juu ya hilo?
Read btn lines 😀😀
 
Sent using Jamii Forums mobile app
Angekuwa Arusha huyu angewekwa ndani,hairuhusiwi ku post barabara mbovu kwani si angeripoti kwa wahusika ifanyiwe kazi?yaani ingekuwa kule Arusha kwa RC Gambo na Rpc shana huyu jamaa angekuwa ndani na kesi ya uhujumu uchumi
 
Kwanza hueleweki unalilia nini

Nchi ina changamoto ya barabara serikali ijitahidi kutatua changamoto kuliko kujisifia, kwani barabara zikiwa bora itakuwa siri? Si kila mtu ataona barabara nzuri?

Kuna maeneo serikali imejitahidi barabara ni nzuri na watu hupiga picha na kupost mbona hukuja kulalamika juu ya hilo?

Hujaelewa kilichoandikwa hapo.
 
Truth is the biggest enemy in the kingdom of lie" (Ukweli ni adui mkubwa kwenye ufalme wa uongo)

Swali la kujiuliza je hio picha ni kweli hilo eneo lipo au halipo? Kama lipo kwanini umuite muhujumu uchumi wakati ni kweli eneo hilo lipo nchini kwetu hapa, issue ya kusema anawatisha watalii wasije haitakiwi kutumika kama excuse .. Je huoni picha kama hii inatoa tahadhari kwa watalii ambao kama wakija wanajua kabisa watakutana na changamoto fulani.

Jamani mambo mengine hata kama ni maslahi au ndo upendo wenyewe tupunguze hata kidogo tubaki kwenye uhalisia Prince Ea aliwahi kusema "Is good to be smart but don't too smart for your own good"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza hueleweki unalilia nini

Nchi ina changamoto ya barabara serikali ijitahidi kutatua changamoto kuliko kujisifia, kwani barabara zikiwa bora itakuwa siri? Si kila mtu ataona barabara nzuri?

Kuna maeneo serikali imejitahidi barabara ni nzuri na watu hupiga picha na kupost mbona hukuja kulalamika juu ya hilo?
Mtoa mada ametumia tungo tata wenye akili wameelewa. Vijana wa siku hizi akili ndogo sana sijui kama mngeweza kuyaelewa mashairi ya kina Shaaban Robert
 
Kwanza hueleweki unalilia nini

Nchi ina changamoto ya barabara serikali ijitahidi kutatua changamoto kuliko kujisifia, kwani barabara zikiwa bora itakuwa siri? Si kila mtu ataona barabara nzuri?

Kuna maeneo serikali imejitahidi barabara ni nzuri na watu hupiga picha na kupost mbona hukuja kulalamika juu ya hilo?
Kama umeshindwa kuelewa FASIHI basi utakuwa ngumu kumwelewa mtoa mada...
 
Back
Top Bottom