Artificial intelligence
JF-Expert Member
- Jan 28, 2021
- 1,262
- 2,191
- Thread starter
- #61
Hapa umeongea point ya msingi, na kuna member nimemwambia basics ni kitu cha muhimu, uzoefu tu haitoshi.Tatizo shule. Mtu anaweza akasema eti uzoefu. Anayefanya kwa uzoefu na aliyepita shule ni vitu tofauti kabisa. Huyu wa mtaani anajua kuwa unachanganya cyanide. Lakini uliepita shule unafahamu kuwa unachanganya cyanide kutengeneza complex compounds, unakuwa unajua kinachofanyika. Unajua chemical reaction zinazofanyika. Unafahamu kuwa cyanide ni moja ya sumu hatari duniani. Ukijua hayo huwezi handle hizo kemikali kizembe, ni kama mabomu.
Sasa mtu anayefanyia uzoefu anafanya tu, yupo peku, hana googles nk. Hata principle rahisi za usimiminie asidi kwenye maji haifahamu. Ajali kila leo.
Japo watu wanatafuta pesa lakini serikali inabidi kuweka uthibiti mkali kwenye afya ya watu na mazingira. Afadhali ziwa victoria linatoa maji, maziwa yasiyotoa maji kama ziwa Rukwa miaka ijayo yatakuwa sumu tupu.