Inasikitisha na kuhuzunisha sana jinsi 'plants' za madini zinavyohatarisha maisha ya watu

Kaka kanda ya ziwa kuna shida sana kwenye issue za plant na elution suala la usalama na hata utunzaji wa chemical zinazotumika kuna shida kidgo japo siyo sehemu zote, kweny suala la mkemia hapa tukubaliane kwamba tanzania wakemia wa masuala ya madini wapo ila lazima tupate wakemia bora ili kupata faida nzuri tatzo ni kwamba hao pia wapo ila ni wachache sana, na ni kama serikali haijawekeza sana kwao na kwa watu wenye plant na elution hasa kwenye suala la elimu ya afya za watu, utunzaji wa mazingira na kuwa updated kila mara
Wakemia wapo, ila wenye plants zao hukwepa kuwatumia kutokana na gharama zao kwa sababu wana uelewa mpana wa madhara ya hizo kemikali.
 
Nishawahi kutembelea hizo plants mpaka ellusion ambapo ndio final stage ya process ya kupata dhahabu

Kwanza siku niliyofika nikiwa geti la kwanza kabisa huku karibia na barabara nikaribishwa na harufu kali ya cyanide.

Kufika ndani nikakutana na vijana wanacheza draf wengine wanakula nguna hawana habari na ile harufu wakati huo mimi nimevaa mask na bado nimeshikila pua at the same time

Kuingia geti la pili nikakutana na kesi, ng'ombe za wasukuma zilikunywa maji ya mto ambayo yalikua contaminated na sumu za plant. Ng'ombe kama 15 zimedanja wasukuma wamekuja kuweka bunge wanataka walipwe

Mmiliki wa plant alikua na mkwanja, akawanyamazisha wale wasukuma wakasepa.

Tulizunguka maeneo ya mle ndani tukagundua kuna vijana wengi sana ambao wameajiriwa kwa ajili ya kuopoa mchanga kwenye tanks ambazo wanachanganyia hizo sumu hii kazi imebatizwa kwa jina la chepe

Mazingira ya kiusalama kiukweli ni mabovu sana, wale vijana hawapewi vizuizi vya kujikinga na sumu na wao wanaona freshi tu as long as wanalipwa on time

Kwenye yale matank ya michanga nilishuhudia kuona vitu vingi vyenye kuashiria hatari ya ile kazi na kufikiria kwamba ilikua ni kazi iliyopaswa ifanywe na maroboti na sio watu.

Ile harufu ya ile sumu kwenye zile tanks ilikua ikivutia sana wadudu na ndege, kuna zile ndege ambazo zinaruka juu na kushuka chini ya maji kisha kunywa maji bila kutua zikiwa zina hang angani, hizi nimeshuhudia kwa macho yangu zikishuka na kudonoa yale maji na kuanguka hapo hapo yani hata kufurukuta hakupo
Mkuu ulivuta hewa ya cyanide yenyewe kabisa au ni kemikali nyingine???
 
Wakemia wapo, ila wenye plants zao hukwepa kuwatumia kutokana na gharama zao kwa sababu wana uelewa mpana wa madhara ya hizo kemikali.
Na hilo ndo tatzo kubwa ila hii ni industry ambayo inatoa pesa nying tu sema vitu vingi vinafanyika kihuni tu na pia rushwa sana ila chemicala zote zina madhara makubwa sana
 
Isitoshe hili suala linaweza kumalizwa hata na mkuu wa wilaya tu,sijui wanafeli wapi,wakati vijana nguvu kazi ya taifa inapotea kizembe kabisa!!!
 
Nishawahi kutembelea hizo plants mpaka ellusion ambapo ndio final stage ya process ya kupata dhahabu

Kwanza siku niliyofika nikiwa geti la kwanza kabisa huku karibia na barabara nikaribishwa na harufu kali ya cyanide.

Kufika ndani nikakutana na vijana wanacheza draf wengine wanakula nguna hawana habari na ile harufu wakati huo mimi nimevaa mask na bado nimeshikila pua at the same time

Kuingia geti la pili nikakutana na kesi, ng'ombe za wasukuma zilikunywa maji ya mto ambayo yalikua contaminated na sumu za plant. Ng'ombe kama 15 zimedanja wasukuma wamekuja kuweka bunge wanataka walipwe

Mmiliki wa plant alikua na mkwanja, akawanyamazisha wale wasukuma wakasepa.

Tulizunguka maeneo ya mle ndani tukagundua kuna vijana wengi sana ambao wameajiriwa kwa ajili ya kuopoa mchanga kwenye tanks ambazo wanachanganyia hizo sumu hii kazi imebatizwa kwa jina la chepe

Mazingira ya kiusalama kiukweli ni mabovu sana, wale vijana hawapewi vizuizi vya kujikinga na sumu na wao wanaona freshi tu as long as wanalipwa on time

Kwenye yale matank ya michanga nilishuhudia kuona vitu vingi vyenye kuashiria hatari ya ile kazi na kufikiria kwamba ilikua ni kazi iliyopaswa ifanywe na maroboti na sio watu.

Ile harufu ya ile sumu kwenye zile tanks ilikua ikivutia sana wadudu na ndege, kuna zile ndege ambazo zinaruka juu na kushuka chini ya maji kisha kunywa maji bila kutua zikiwa zina hang angani, hizi nimeshuhudia kwa macho yangu zikishuka na kudonoa yale maji na kuanguka hapo hapo yani hata kufurukuta hakupo
Kwamba kazi ya maroboti, ndiyo kazi za wakemia hizo, ndiyo maana ukikutana na mkemia ambaye ashafanya kazi maabara sana anakuwa kama amechanganyikiwa.
 
Hapo nimezungumzia kule kwenye kuopoa yale mamichanga kwenye zile tanks, juzi hapo kuna dogo kafariki alikua anaopoa carbon
 
Isitoshe hili suala linaweza kumalizwa hata na mkuu wa wilaya tu,sijui wanafeli wapi,wakati vijana nguvu kazi ya taifa inapotea kizembe kabisa!!!
Tanzania kweny industry ya mining hasa hawa wachimbaji wadogo na wachimbaji wa kati kuna changamoto sana, hizi plant zinaingiza hela sana ila ni kama serikali huwa inawapenda sana pale wanapokuja kukusanya kodi tu
 
Mkuu sidhan Kama umefanya tafiti sahihi kwasbb moyo wa plant wote utegemea mkemia. Mkemia fake si kuleta madhara kwa watu tu, Bali kuleta hasara kubwa kwa kutosababisha dhahabu ikamatwe kwenye cabon.

Kwa mmiliki wa plant au mtu aliyepeleka rundo kuozesha hawez kuwa na mkemia fake maana atajua yuko hatarin kupata hasara.

Jambo lingine zile kemikali ni hatari Sana kwa binadam na wanyana na hata mimea. Mfano sayanaidi ni sum mbaya, sidhan Kama kweli mtu anachezea maisha yake kijinga jinga.

Kama hiyo haitoshi sehem ya kujenga plant serikali kupitia watu wa mazingira NEMK, wako Makin Sana kutoa vibali haswa kwa kuangalia yale maji ya shimo la sumu.

So nakubaliana na wewe kwa kias kidogo, siyo plant zote Zina hatarisha maisha, uenda ni uko Kanda ya ziwa tu. Unaweza kwenda Kanda ya kati mfano pale dodoma kule NHOLI, plant zote ziko na wataalam na Serikali inasimamia usalama wa watu kwa ukaribu sana.
Umenena vyema
 
Na hilo ndo tatzo kubwa ila hii ni industry ambayo inatoa pesa nying tu sema vitu vingi vinafanyika kihuni tu na pia rushwa sana ila chemicala zote zina madhara makubwa sana
Wanavuna pesa nyingi sana, ndiyo maana wanatoa rushwa sana, pesa ipo.
 
Serikali ilaumiwe kwa kushindwa ku control cyanide. Ilitakiwa cynide isiuzwe hovyo iuzwe kwa wataalamu wenye vibali tu na akikutwa mtu anayo na hana permit ni jela. Tungeanzia hapo kwanza.
 
Isitoshe hili suala linaweza kumalizwa hata na mkuu wa wilaya tu,sijui wanafeli wapi,wakati vijana nguvu kazi ya taifa inapotea kizembe kabisa!!!
Wakuu wa wilaya wanawekwa mfukoni na hao wenye plants, kuna wilaya moja mwenye plants alikuwa amewaweka mfukoni mkuu wa Wilaya na mkurugenzi wote na amewazawadia hadi gari kila mmoja, JPM alipotembelea hiyo wilaya akampiga stop yule jamaa, na akamwambia mkuu wa wilaya hiyo warudishe gari walizopewa na huyo jamaa. Kwahiyo mambo sio mepesi.
 
Kumbe ndivyo hali ilivyo huko kwenye uchimbaji, duh Hii ni zaidi ya kubebeshwa unga (a.k.a kuwa punda) hali mbaya sana kwa vijana wenzetu as3
 
Hizo kemilaki zimegarimu sana maisha ya wengi hasa wasionufaika na madini kabisa...hasa watumiaji wa maji ya mito na mifugo
 
Wakuu wa wilaya wanawekwa mfukoni na hao wenye plants, kuna wilaya moja mwenye plants alikuwa amewaweka mfukoni mkuu wa Wilaya na mkurugenzi wote na amewazawadia hadi gari kila mmoja, JPM alipotembelea hiyo wilaya akampiga stop yule jamaa, na akamwambia mkuu wa wilaya hiyo warudishe gari walizopewa na huyo jamaa. Kwahiyo mambo sio mepesi.
Jamaa akawaziba midomo kwa kuwapa magari

Jpm alikuwa mbabe sana,apumzike salama mwamba!!!!
 
Tatizo shule. Mtu anaweza akasema eti uzoefu. Anayefanya kwa uzoefu na aliyepita shule ni vitu tofauti kabisa. Huyu wa mtaani anajua kuwa unachanganya cyanide. Lakini uliepita shule unafahamu kuwa unachanganya cyanide kutengeneza complex compounds, unakuwa unajua kinachofanyika. Unajua chemical reaction zinazofanyika. Unafahamu kuwa cyanide ni moja ya sumu hatari duniani. Ukijua hayo huwezi handle hizo kemikali kizembe, ni kama mabomu.

Sasa mtu anayefanyia uzoefu anafanya tu, yupo peku, hana googles nk. Hata principle rahisi za usimiminie asidi kwenye maji haifahamu. Ajali kila leo.

Japo watu wanatafuta pesa lakini serikali inabidi kuweka uthibiti mkali kwenye afya ya watu na mazingira. Afadhali ziwa victoria linatoa maji, maziwa yasiyotoa maji kama ziwa Rukwa miaka ijayo yatakuwa sumu tupu.
 
sio kila biashara lazima ifanywe na kila mtu, hapa ndio utaelewa kwanini lazima vitu fulani fulani lazima vifanywe na magiants......sisi pangu pakavu na mitaji yetu tutafuta vinavyofanana na mitaji yetu ili tufanye kwa ufanisi...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom