MLUGURU
JF-Expert Member
- Mar 30, 2012
- 2,836
- 3,537
Hii tabia sio nzuri mkuu tabia ya fisi mnaweza mkaamka asubuhi mkakuta kichwa bila kiwili wili cha ndugu yenu mlangoni sijui itakuwaje hapo.Ila sisi binadamu tuna uchuro sana. Kwanini ujengee kaburi? Tena ikiwa ni makaburi ya public?
Kama ni makaburi ya familia sawa jengeeni ila kama unazikwa kwenye cemetery za jumuiya msiwe mnajengea. Kwasababu kiuhalisia ni kuwa ingekuwa makaburi hayafukuliwi na kuzikwa wengine hapo Kinondoni pangeshajaa miaka ya zamani sana.
Wanaojengea makaburi ni wabinafsi tu. Mtu akishakufa amaekufa mzikeni sawa ila msijengee kaburi ili na wengine wakifa wapate pakusitiriwa.
Ifikie mahali pia tuwe na tamaduni za kufanya cremation (kuchoma miili baada ya taratibu za msiba). Hii itapunguza uhitaji wa ardhi ya kuzikia watu.
Sisi wamasai zamani mtu alikuwa akifa tunampaka mafuta ya kondoo na anapelekwa vichakani huko analiwa na fisi habari yakw inakuwa imeisha.