Zapa RadioFm
Senior Member
- Feb 12, 2016
- 112
- 171
Inasikitisha Sana kuona viongozi wetu wakisumbuka kutafuta nani ameficha sukari.
Viongozi wetu hawakutakiwa kusumbuka kujua nani ameficha sukari hali wakijua hakuna mfanyabiashara anayekosa stoo.
Kilichopo ni kwamba maamuzi ya kuzuia vibali vya sukari kutoka nje ni maamuzi sahihi lakini si kwa wakati huu.
Ikumbukwe kwamba viwanda vyetu vya sukari nchini ambavyo vinategemea malighafi ya miwa bado havijaanza kuvuna miwa mpaka ufikapo mwezi wa sita.
Hivyo basi viwanda kwa wakati huu vinazalisha sukari kidogo sana, kiasi kisichokizi mahitaji ya watanzania.
Na kwa kawaida viwanda vya sukari huzalisha asilimia sitini tu na asilimia arobaini kutoka nje ya nchi.
Ndio maana tunatumia nguvu sana kutafuta sukari huku ikiendelea kupanda bei siku hadi siku.
Siku moja Patrice Lumumba akasema "African make decision which require logic without using logic''
Yaan "waafrika wanafanya maamuzi yanayohitaji kushughulisha akili sana bila kushughulisha akili"
NINI KIFANYIKE???
hatupo hapa kulaumu sana sababu tunaweza kulaumu mpaka majasho yatoke lakini hatuwezi kubadilisha chochote?
HIVYO BASI
Mrisho Mpoto aliwahi kuimba akisema "mjomba chutama, muungwana akivuliwa nguo huchutama''
Cha msingi ni kuruhusu sukari toka nje wala sio kutafuta nani ameficha sukari.
Faida yake ni nini?
Tukiruhusu sukari toka nje hata walioficha sukari wataitoa tu,
Kwanini? Kwa sababu watahofia sukari yao kuharibika.
Kumbe tukitoa vibali tu sukari itashuka bei.
TUJIULIZE?
Kuna faida gani ya kutumia sukari yetu inayouzwa kwa bei ya sh zaidi ya 3000 kwa kilo, au kutumia sukari ya kwetu na ya nje kwa bei ya sh 2000 kwa kilo?
Kuna faida gani ya kusema walioficha sukari nitalala nao mbele halafu watu wakitoka hapo wananunua sukari kwa bei ile ile?
Kuna faida gani ya kuwa na maneno mengi bila vitendo?