Inasikitisha; Kijana ajiua baada ya kukosa ajira Jeshini

1gb

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
2,129
2,765
Kijana Sunday Matara(28)amejiua kwa kujinyonga baada uongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa kusitisha mafunzo kwa vijana wa kujitolea 2020/2021.

Marehemu tayari alikua amekamilisha mafunzo kwa miaka mitatu ambapo baada ya kutoka Jkt alikwenda kukaa kwa Kaka yake Pugu,Dar es salaam.

Huko ndiko alichukua maamuzi ya kukatisha uhai wake.

Mungu awatie nguvu familia yake,AMENI.




Serikali isipo ona haja/umuhimu wa kubadili mtaara basi tutarajie vijana wengi kufanya maamuzi ya kusikitisha na ya kuogofya mno kadri siku zinavyoendelea.

Elimu yetu tangu msingi ina mset kijana kusoma na kuajiriwa.

Na si kujiajiri,mwisho kwa uchache wa ajira inapelekea msongo wa mawazo na matatizo lukuki.

Na ukikuta kijana kajiajiri basi tegemea mambo mawili.

Mosi hakufaulu kuendelea na masomo.

Pili kamaliza elimu ya juu ila kasota sana kutafuta ajira bila mafanikio.

Nimefikiria huyu ni kijana wa kidato cha nne tu, je Ma graduates toka jalalani na kwingineko hali yao ikoje, too sad.

Hapa mimi sina ajira na mke wangu soon atajifungua,natarajia Mwanangu akianza masomo 2027-2040 A-Level atapita kwenye mtaala kama ule ule alopita baba yake.

Hali inasikitisha.

Heri walau A-level zote zigeuzwe technical school, angalau kijana akitoka advance akajiajiri mwenyewe.

Nawaza kwa sauti, nimesikitishwa mno.
 
Huo ni ukichaa mimi si laumu serikali hata kidogo. Ni wangapi hawana ajira yeye kapitia tu jeshi lakini kuna mtu anasoma hadi shahada ya uzamili lakini yuko mtaani.

Nina kijana mmoja namtolea mfano amesoma degree yake ya masters amemaliza chuo kikuu cha SAUT kaona ajira mchemsho kajikita kwenye kilimo ziwani ameniambia hana mpango wa kuajiriwa kutumikishwa kwa masaa amenivutia sana. Sio kila kitu mnatumpia serikali lawama serikali ina mipango yake.

Huyu hata angeajiriwa jeshini angekuwa mtu hatari sana angekuwa mtu rahisi kutoa roho ya mwenzake endapo kamuuzi akiwa ameshika bunduki RIP kijana.
 
Tatizo la Mtanzania huwa hamfikirii mwenzake baada ya yeye kupata ulaji tumekuwa wabinafsi sana. Bungeni kutwa kumsifia Rais, Spika, Naibu Spika kisha anamalizia na familia yake hakumbukuki hata watanzania walio muweka pale alipo.

Spika badala ya kuongelea maslahi ya watumishi wa umma yeye anaongelea swala la walimu kuongezewa somo lingine la kufundisha kama vile kufundisha ni kazi rahisi kila mtu anaweza kufanya au walimu wanapewa hela ya bure. INAUMA SANA

Hali ngumu sana mtaani na wateule wa Rais hawaoni huo ugumu maana wenyewe wapo kwenye kuneemeka ndio maana kutwa kucha ni kusifia tuu. Huyo kijana alikuwa na miaka 28 bila shaka ni umri wa kuwa na familia na kusettle halafu ghafla bi vuu hakuna ajira maana arudi upya kabisa mtaani aanze upya kabisa kupambana.

Miaka 3 kapoteza bure kabisa !! Mafunzo aliyoyapata huko ni bure kabisa !! Kachukua maamuzi MAGUMU ila ukijaribu kuvaa viatu vyake HAVITOSHI KABISA.

Inasikitisha sana kuona maisha yetu yanaamuliwa na mtu mmoja, yeye ndio anaamua uishije KISHETANI AU KIMALAIKA.

HATA HIVYO WANANCHI NDIO WENYE NCHI KAMA WAO WAPO KIMYA NDIO MANA WANAFANYA WATAKAVYO.

Aende salama.
 
Kijana huyo mkazi wa jiji la Mwanza ilemela amejinyonga kwa msongo wa mawazo baada ya kumaliza mkataba wa kulitumikia jeshi la kujenga taifa 'na kukosa ajira kwa miaka 3 kupitia kambi ya msange tabora na mgulali dares salam 'na kuchukua uamuzi wa kujinyonga tazama mkasa mzima kwenye video hapo chini kwa hisani ya millard ayo
 
Kawaida jeshini wapo wanaoenda kwenye mafunzo halafu mwisho wa siku wanakosa ajira, zaidi hupewa pesa ya sabuni na vocha, kula na malazi vipo kambini, mwisho wa siku wapo wanaobahatika kupata ajira wanaendelea na maisha ila kwa wale wanaokosa huamua kuondoka jeshini na kurudi uraiani.

Hawa huamua kutafuta kazi za ulinzi kwenye makampuni mbalimbali na wengi wao hupata kwasababu huwa na nidhamu ya jeshini, laikini pia huaminika kiwa ni wakakamavu zaidi.

Huyo dogo amejikatisha uhai wake mapema bila sababu, alikuwa bado na njia nyingi tu za kuishi, watu wakiwa na mawazo ni vyema wakawauliza wakubwa wao kupata ushauri na mara nyingi solution za matatizo ya watu huwa zipo kwa watu, hakuna tatizo jipya hapa duniani, kwani mengi tunayokutana nayo ni marudio ambayo wenzetu walishayapitia na kusonga mbele.
 
Sasa tusipoilaumu serkali mtuambie lawama tuzielekeze kwa nani. Serkali inajinasibu ni tajiri inashindwa nn sasa kuajiri japo kila wizara/taasisi ajira 50,000.

Hao wenye degree za sua wanatumia elimu yao kulima maboga mtoni,wamenufaika na course walizosoma. Je, wenye diploma ya mahusiano ya jamii wafanye nn? Wenye certificate je?

Acheni maskhara o-level kila mwaka inatema ma mia ya wahitimu, A-level inatema mamia,vyuo vinatema maelfu na wana wayawaya na serkali haijui iwapeleke wapi na majibu haina.

Twende mbele turudi nyuma,kuna kitu bado serkali inakwama.


Wewe na mimi ndo wenye majukumu ya kuishauli serikal kama si kwa amani hata kwa maandamo.

Kama mahali ilikosea ama inakosea tuseme tu,mmezidi mno kuipamba kwa mapambio ya sifa wakati vijana wapo chini ya mawe wamekaliwa na jiwe kuu.

Baadhi wanapoteza wapendwa wao, Kukosa ajira ni kama ugonjwa, unamla mgonjwa polepole wengine wanakuwa walevi kupindukia, wengine wezi, wengine kama mazezeta, wengine wanajiua kabisa.
 
Kawaida jeshini wapo wanaoenda kwenye mafunzo halafu mwisho wa siku wanakosa ajira, zaidi hupewa pesa ya sabuni na vocha, kula na malazi vipo kambini, mwisho wa siku wapo wanaobahatika kupata ajira wanaendelea na maisha ila kwa wale wanaokosa huamua kuondoka jeshini na kurudi uraiani...
Wewe unazijua kazi za ulinzi kwenye kampuni binafsi zilivyo?
 
Back
Top Bottom