Elections 2010 Inashangaza

Masika

JF-Expert Member
Sep 18, 2009
723
30
Wana jf
hivi kwa nini majimbo ambayo ccm imepigwa chini matokeo
yamecheleweshwa?
Kuna nini hapo?
Tujadili
 
Jibu ni kuwa walikuwa wanajaribu kuangalia reaction ya wanachi kabla ya kutangaza. Wanatangaza baada ya kuona kwamba hawana jinsi na ni hatari kutangaza vinginevyo. Pole zao, ni kama msiba maofisini sasa.
 
Umejuaje kama wameshindwa wakati matokeo hayajatangazwa?

Iko wazi, angalia Kawe, Ubungo, Arusha, Hai, Mbeya. Hayo matatu ya mwisho (Arusha, Hai na Mbeya), walikuwa wanagoma kutangaza mpaka wananchi wakafanya fujo ndio wakatangaza. Kawe na Ubungo wanasuasua, wakati kuna habari za uhakika (110%) kuwa Chadema imeshinda katika majimbo haya mawili. CCM ni waoga wa kupigwa chini, na mwaka huu mmepata message kuwa hatuwatakiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.....!!! Mnanuka udini, undugu, ufisadi, rushwa, umbumbumbu, ukilaza na kila kero ya dunia...........!!!! Hakuna mtu mwenye akili timamu atakipigia kura chama cha CCM, labda awe amekubali kuhongwa T-shirt, au kuhaidiwa hela, au uongozi wa kitongoji n.k. Kitu ambacho ni aibu ya hali ya juu....!!!

Upinzani hoyeeeeeee......!! Wananchi wa Tanzania mmenipa raha mwaka huu, tunataka bunge lenye akili na mchakamchaka, mabingwa wa kusinzia.
 
Mfano kigoma mjini Chadema walishinda ccm wakagoma kusaini na walipofanya recount wakachakachua ccm wakashinda inabidi tujue kwamba yale maamuzi magumu yaliyosemwa na Dr. SLAA ndo kama yale ya Arusha Mwanza na kwingineko bila vile ungeshangaa ccm wanashinda.
 
Back
Top Bottom