Inashangaza: Rais Samia mwezi Juni 2021 alisema akiba ya fedha za kigeni ni Dola bilioni 4,765

Achana hata na hilo. Anashindwa vipi kushtukia na kutambua nchi ina hazina kiasi gani, exactly? Maana sisi raia tumemwajiri Rais ili a-deliver matokeo yenye viwango visivyoweza kutiliwa mashaka. Hivi angekuwa CEO au mkurugenzi mahali fulani, asingetumbuliwa jana yake, kabla hata hajafanya kosa?
Magu amekufa mkuu, na ameshazikwa, na ameshaoza. Nothing less nothing more. Iwe utililie shaka au usitie, Samia ndiyo Rais wako hadi 2030 kama atapewa uhai.
 
Ndugu zangu haya mambo yanashangaza sana.Katika kipande cha video hapo chini Rais Samia Suluhu Hasan akiwa Mwanza mwezi juni 2021 alidai kuwa akiba yetu ya fedha za kigeni ni dola za kimarekani bilioni 4765.

Ndugu zangu Mwezi Juni 2021 tuliambiwa tuna akiba ya fedha za kigeni dola bilioni 4765. Mwezi Disemba ikapanda na tukaambiwa akiba yetu imefika Dola za kimarekani bilioni 6253. Mwezi Juni 2021 mbona taarifa ya ufafanuzi kuwa Serikali imekosea haikutoka?

Kuna uwezekano mkubwa sana kuwa haya mambo yanapangwa kimkakati na kwa makusudi kwani siyo rahisi Rais akosee mara mbili.

Huenda nchi inaongozwa kwa propaganda.Ni vyema tukajua ukweli uko wapi kwani hii nchi ni yetu sote.

Kwa mtu mwenye akili zake ukiunganisha doti ya hizi hotuba mbili ni lazima upate harufu ya kitu ambacho siyo kizuri.

Kitendo cha Rais kukosea mara mbili kinaibua tena maswali kadha ambayo ndani yake yanatupa taarifa kuwa huenda nchi inaongozwa kwa propaganda.

1.Inawezekana Rais amekosea mara mbili?

2.Mbona mwezi juni 2021 hatukupata ufafanuzi kuwa Serikali imekosea?

3.Kama Rais anakosea kirahisi hivi,ni mangapi anakosea?
View attachment 2066406
Ikulu ni mzigo - JK NYERERE
 
Jamaa aliazima sufuria, baada ya wiki akarudisha sufuria kadogo sana, tofauti na aliyoazima, akamwambia sufuria yako bado ninayo hii hapa imezaliwa toka kwa sufuria yako, jamaa alifurahi sana, wiki ya pili alienda toa taarifa kuwa mama sufuria yule amekufa na tayari amesha zikwa. Hapa kuna siku utasikia hamna fedha ya kigeni wala kienyeji, tulieni tu!
 
Najaribu kukusoma mahala sikuelewi, unasema mwezi Juni 2021 tuliambiwa tuna akiba ya dola 4765, then mwezi Dec 2021 tukaambiwa tena tuna akiba ya dola 6253, unapouliza mbona taarifa ya mwezi Juni 2021 hatukupewa unakuwa na maana gani?
Hivi mtoa Thread sijamuelewa, kwani tatizo hapo liko wapi? Ni namba ndio zinamchanganya au ni nini?

Najaribu kuichambua hotuba/taarifa ya mama kama ifuatavyo:
  • Mwezi wa sita 2021, taarifa ya mama inasema akiba ya pesa za kigeni ni dola bilioni 4765
  • Mwezi disemba (yaani baada ya miezi sita hivi) akiba ya pesa za kigeni ni dola bilioni 6253
Sasa kosa liko wapi kwa sababu akiba imeongezeka toka dola bilioni 4765 mpaka dola bilioni 6253 au ongezeko/tofauti ni dola bilioni 1488. Tupo pamoja jamani! Nisahihisheni nilipokosea.
 
ikulu_mawasiliano~p~CYO1dI1r51-~1.jpg

Nadhani sasa utakuwa umemuelewa
 
Hivi mtoa Thread sijamuelewa, kwani tatizo hapo liko wapi? Ni namba ndio zinamchanganya au ni nini?

Najaribu kuichambua hotuba/taarifa ya mama kama ifuatavyo:
  • Mwezi wa sita 2021, taarifa ya mama inasema akiba ya pesa za kigeni ni dola bilioni 4765
  • Mwezi disemba (yaani baada ya miezi sita hivi) akiba ya pesa za kigeni ni dola bilioni 6253
Sasa kosa liko wapi kwa sababu akiba imeongezeka toka dola bilioni 4765 mpaka dola bilioni 6253 au ongezeko/tofauti ni dola bilioni 1488. Tupo pamoja jamani! Nisahihisheni nilipokosea.
Hizo namba unaona zipo sahihi? Hizo ni pesa nyingi sana hata Marekani hawana, na hapo ndipo mjadala ulianzia.
Ikulu imekuja kutoa ufafanuzi kuwa kulikua na makosa kwenye uwasilishaji wa hizo taaarifa na hivyo sio dola bilion Bali ni dola million.
Lakini hii si Mara ya kwanza raisi kukosea, alikosea pia kwenye hotuba yake ya June na ndio huyu mtoa post kakumbushia
 
USD 6253 Billion = 6,253,000,000,000 USD = 6,253,000,000,000 x 2306 Tsh = 1.4419418E16 = (1.4419418E16/1E12) = 14,419.418 Trillion Tanzania shillings

W’re one among the rich Countries on this hell of the planet
 
Yes, Rais amekosea then what? Kuna kifungu chochote cha Katiba kilichovunjwa kwa Rais kukosea? Rais JPM alikosea na kusema Saddam Hussein Rais wa Kuwait, ilimfanya kukiuka Katiba? Let's deal with tangible issues, at least zile zenye makosa ya kikatiba au kisheria wajamen.
 
Back
Top Bottom