Inashangaza: Kumbe wajumbe wa kumi kumi bado wapo na wananguvu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inashangaza: Kumbe wajumbe wa kumi kumi bado wapo na wananguvu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Amiliki, Feb 10, 2012.

 1. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Jana nilikuwa na akina mama ambao ni Wanachama wa CCM kwenye msiba wa ndugu yangu Kimara. Katika maongezi yao, wakaanza kuzungumzia Uchaguzi wa ndani unaoendelea hususan wa kuwapata Wajumbe/Mabalozi wa nyumba kumi.

  Kwa mshangao nikauliza kumbe hawa watu bado wapo na wanafanya nini! Ndipo wale akina mama wakaniambia kwamba hawa watu wapo na Wananchi huwapelekea matatizo yao na kuyatatua. Pamoja na hivyo ni kwamba hawa watu hutoza shilingi Elfu mbili kwa fomu za kuwadhamini watu ili waweze kupata barua ya Mtendaji(ambayo nayo wanailipia) kama wanataka kumdhamini mtu mahakamani.

  Nikajiuliza, Ina maana hizi barua za Wajumbe wa nyumba kumi kumi wa CCM zinatambulika Kisheria!

  Naomba kujuzwa.

  My take: Hivi vyama vingine navyo vikianza kuwatumia viongozi wake wa chini kufanya hivyo si itakuwa vurugu mechi! CCM acheni kuendelea kuwapumbaza Watanzania kwa kutumia ujinga wao kama Mtaji wa kuwaibia.

  Waelekezeni kwamba nyie si mahakama waende wenyewe kwa Watendaji kama wanashida ya Kiserikali. Msiendelee kuwaibia bana!.
   
Loading...