Elections 2010 Inasemekana Wenje alikataa mil 900 za kumwachia jimbo Masha!

Hero

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
3,932
2,832
Taarifa zisizo rasmi zinasema JK alikuja Mza kujalibu ku'rescue' situation, na moja ya mbinu mbovu iliyotumiwa baada ya zote kugonga mwamba ilikuwa akubali kupokea kiasi hicho ili JK atimize azma yake ya kumapisha Masha kwa mara nyingine tena kama alivyoahidi kwenye ufunguzi wa campaign!

Bwana mdogo Wenje aliwajibu kuwa waende kuwapa kiasi hicho wananchi waliokuwa na hasira nje ya fensi, wakikubali, basi yeye angeachia jimbo hilo. Wakati huohuo, wapiga kura walikuwa wameahidi kuwa endapo Wenje angekubali hongo basi angekuwa nyama yao na kwa kuanzia wangeimaliza familia yake!

Na baada ya tafrani kuanza, mpango ulikuwa kuteketeza jiji la Mza kwa kulipua vituo vya mafuta vilivyopo jijini kitu kilichowafanya jeshi la polisi kushinikiza kutangazwa kwa matokeo!

Can u imagine, how far can ccm go to ensure it remain in power! ccm is :evil::evil::evil::evil:
 
Mkuu hii mbinu ilitaka kutumika Arusha bahati nzuri watu wakawa ngangari kuliko serekali ya CCM walivyotarajia.
 
Duh, mkuu napata picha halisi inatisha na hapo ndo kungekuwa mwanzo wa vurugu kubwa nchini, na bado mwanza ndo kuna Tarime yote milimani hawaogopi kitu wala kuua ni kawaida. Lakini yote hayo ni kwa sababu watu wanatamaa na madaraka saaana.
 
Poole sisiemu. Mngewapa nao wananchi hizo kodi zao watumie. Mnajidai mnaehela sana. :bowl:
 
JK alifikiri watu wanaweza kudanganyika kwa kuwapa wabungu wao nafasi ya uwaziri wa kifisadi.
Kwa sasa asije akadhani Watanzania watadanganyika kwa hongo ya aina hiyo.
 
Taarifa zisizo rasmi zinasema JK alikuja Mza kujalibu ku'rescue' situation, na moja ya mbinu mbovu iliyotumiwa baada ya zote kugonga mwamba ilikuwa akubali kupokea kiasi hicho ili JK atimize azma yake ya kumapisha Masha kwa mara nyingine tena kama alivyoahidi kwenye ufunguzi wa campaign! Bwana mdogo Wenje aliwajibu kuwa waende kuwapa kiasi hicho wananchi waliokuwa na hasira nnje ya fenci, wakikubali, basi yeye angeachia jimbo hilo. Wakati huohuo, wapiga kura walikuwa wameahidi kuwa endapo Wenje angekubali hongo basi angekuwa nyama yao na kwa kuanzia wangeimaliza familia yake!
Na baada ya tafrani kuanza, mpango ulikuwa kuteketeza jiji la Mza kwa kulipua vituo vya mafuta vilivyopo jijini kitu kilichowafanya jeshi la polisi kushinikiza kutangazwa kwa matokeo!
Can u imagine, how far can ccm go to ensure it remain in power! ccm is :evil::evil::evil::evil:


Walishaanza na Ofisi ya kata ya CCM. Imeteketezwa kwa moto mchana kweupe............. Cheza na wajinga wa Dar sio huku kwetu MURA.
 
JK ni mmoja wa watu wasioweza kutafsiri mabadiliko ya mazingira yaliyowazunguka wa ajabu kabisa!Yeye anafikiri kuwa kila mtu ana bei ya kununulika kama yeye na wenzake?Vizuri sana kumfundisha the hard way huyo mbweha asidhani kuwa kafika.TENA ATAMBUE KUWA UMMA UKISHAAMUA HAOUGOPI RISASI, BOMU,JENEZA WALA FEDHA NA DHAHABU.HATASAHAU UCHAGUZI HUU HT AKIWA MZEE.NA MASHA ARUDI TU DAR,MAFISADI WANA KESI NYINGI ZA KUHITAJI MSAADA WA MWANASHERIA FISADI PIA!HAYA TUSONGE MBELE TUZIDI KUJENGA A STRONG OPPOSITION,AND I HAVE A DREAM, THAT THE NEXT PRESIDENT IN 2015 OR 2020 WILL BE A CANDIDATE FROM THE OPPOSITION!I HAVE A DRE4AM THAT FROM 2015 CCM WILL BE AN OPPOSITION PARTY AND I HAVE A DREAM THAT JK AND WANAMTANDAO WILL APPEAR IN COURT TO ANSWER CHAARGES OF CORRUPTION,NEPOTISM,AND THE LIKES!
 
Jamani Hii si harufu nzuri at all,Tutayasikia vizuri tu as time goes on!!Wanasiasa watambue kuwa Uongozi ni dhamana wanayopewa na wananchi na wakiamua kuichukua basi wasione kama wao ndio pekee wanastahili kuiongoza jamii.Waache mawazo ya kitoto,maana mtoto ukimpa kushikilia kitu kizuri basi tayari anahesabu ni chake!!CCM na wengine wote watambue hawana haki ya kuwaongoza watu milele,anytime anything can change!
 
Watu wanadhani JK ni msafi kama wanavyomuona, ukweli ni kwamba huyu mkwere amelowa damu mikononi!!!
 
Walishaanza na Ofisi ya kata ya CCM. Imeteketezwa kwa moto mchana kweupe............. Cheza na wajinga wa Dar sio huku kwetu MURA.

Arusha, Mara na Mbeya ni mikoa ambayo nina iaminia sana kwa misimamo.
 
Wengi sana wamenunuliwa kwa mtindo huu... aliekera zaidi ni yule mgombea wa CHADEMA pale songea...
 
Huu ndio uchaguzi wa kidemokrasia tanzania. Hongera kikwete, hongera ccm.
 
Huku Arusha mjini walitaidi kuchachua ikashindikana kwasababu mbunge wa cahde alikuwa na kura kama 50,000 na ccm walikuwa 20,000 hivi hasa ikashindikana ingekuwa tofauti ya 5000 wangebadilisha matokeo.Mpaka mzee mzima alikuja yaani lowasa alikuja kuokoa jahazi wampe angalau milion 150 aachie jimbo wanachi wakasema hizo ni kula zetu wakasema mbunge wetu akikubali hizo pesa akitoka nje halalia yao yaani wangempiga na vurugu ingetokea ARUSHA isingekalika.
 
Duh, mkuu napata picha halisi inatisha na hapo ndo kungekuwa mwanzo wa vurugu kubwa nchini, na bado mwanza ndo kuna Tarime yote milimani hawaogopi kitu wala kuua ni kawaida. Lakini yote hayo ni kwa sababu watu wanatamaa na madaraka saaana.
Actually ni uroho wa madaraka, na kwa bahati mbaya, they dont deliver people's expectations! They entirely do 4 their own interest regardless the citzen safely. Hali ya jana Mza imeonyesha jinsi gani amani ilivyo volatile (easily evaporative). CCM is acts at an extream delicate balance of peace/war!
matukio ya huko Shy, Kg, Mby, Dsm and other tell the whole story!:A S angry::A S angry::A S angry::A S angry:
 
Nakumbuka niliandika story hiii kwenye thread hii hii.................kabla hata ya uchaguzi kuwa he was offerd 900Mil nikaambiwa mzushi leo hii imekuwa ni yakuwekwa tena hapa........................na inaonekana ni kweli je ule Uzushi wana JF mliosema mwanzo mko wapi......the problem hatujuani kuwa nani ni nani.... ila nashukuru kuwa leo imeonekana ni kweli na learn to follow up on stories......:yield::doh::doh:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom