Inasemekana walimuibia,tatizo wezi walikuwa wana nguvusana kumshinda

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
4,981
2,000
Shaaban-Robert1.jpg1.Waliiba waibaji,hata sasa wanaiba
Kaibiwa mtungaji,moyoni kachomwa mwiba
Walikaba wakabaji,wakamwachia msiba
Kafa na lake moyoni,hakiye hikusikizwa.

2.Waliiba wanyonyaji,wakaiba wakashiba
Yeye kwa wake uchaji,mdomo akauziba
Hakuridhika na taji,la ukoka lenye miba
Ila angefanya nini,wakati kesha ibiwa.

3.Wakafaidi walaji,walao sasa vibaba
Walijua tena haji,ju yake ipo miraba
Nani wakumfariji,hali maisha ni haba
Walijua ni mnyonge,hanapo pa kusemea.

4.Mbora mpambanaji,fasihi kaipa tiba
Chozi li ndani ya maji,bahari iliyaziba
Si Bure chake kipaji,wala Jana walishiba
Kafa na mengi moyoni,hali alidhulumiwa.

5.Wakala wake mtaji,vibao wakamzaba
Kimya hao wasutaji,vidume haba na haba
Sioni waropokaji,tunapandaje uhaba
Majizi yalishaiba,na bado twayachekea.

6.Ingawa Mola mpaji,kimya chetu siyo twiba
Zama za ulipuaji,tuyachinje mangariba
Wajifanya wajuaji,mashetani makahaba
Walimwibia kwa siri,na siri itafichuka.

SHAIRI-ALIIBIWA
MTUNZI-Idd Ninga, Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom