Inasemekana marehemu mzee Kingunge hakuwa na dini, atazikwa kwa utaratibu gani?

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
MAZISHI.jpg

Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru anatarajiwa kuzikwa Jumatatu Februari 5, 2018 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa kamati ya maziko ya mwanasiasa huyo, Omary Kimbau amesema Kingunge atazikwa saa tisa alasiri.
Hata hivyo, amesema leo Ijumaa Februari 2,2018 kuwa utaratibu na mipango mingine inaendelea kufanyika.

Kingunge amefariki dunia leo alfajiri akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Alikuwa akiuguza majeraha baada ya kung'atwa na mbwa mwishoni mwa mwaka jana nyumbani kwake.

Mpwa wa Kingunge, Tony Mwiru akizungumza na MCL Digital amesema familia inapitia kipindi kigumu kwa kuwa hivi karibuni wamempoteza mama yaom, Peras.

Enock Mwiru ambaye ni mdogo wa marehemu na mtangazaji wa zamani wa iliyokuwa Redio Tanzania (RTD), amesema Kingunge alikuwa kiunganishi cha familia.Mabalozi Juma Mwapachu na Ali Mchumo waliowahi kufanya kazi na Kingunge wamefika nyumbani kwa marehemu Kijitonyama kuhani msiba huo.

Mytake:

Kingunge hana dini. Sijui itakuwaje mazishi yake!
 
Siyo lazima azikwe na dini fulani.

Halafu, huwezi ukataja madhehebu mawili tu as if hapo Tanzania pana madhehebu mawili tu.

Acha unaaaaa (in Hon. Mrema's voice)

Acha unaaaa, mleta uzi.
Mzee Kingunge amelala.,
Acha azikwe kama familia yake watakavyopenda au yeye mwenye kama aliweza kutoa maelekezo hiyo namna.

R.I.P Mzee Kingunge.

Poleni wafiwa wote.
 
kingunge sio hana dini ... kingunge ni mbantu na dini yake ni bantuism.. je kabla ya kuja wakoloni waafrica hawakuabudu?

Hawakuwa na dini za asili..note; dini hizi ni ni tofauti kutokana na kabila, koo na tamaduni tofauti ndipo yeye alipoamua kubaki mwingine ninayemfahamu yuko hivo ni wakili munuo wa moshi mume wa jaji munuo
 
Sijui ila ninamini yule anayesemaga anamtanguliza mungu mbele HATAHUDHURIA maombolezo wala mazishi.
 
View attachment 689244

Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru anatarajiwa kuzikwa Jumatatu Februari 5, 2018 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa kamati ya maziko ya mwanasiasa huyo, Omary Kimbau amesema Kingunge atazikwa saa tisa alasiri.
Hata hivyo, amesema leo Ijumaa Februari 2,2018 kuwa utaratibu na mipango mingine inaendelea kufanyika.

Kingunge amefariki dunia leo alfajiri akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Alikuwa akiuguza majeraha baada ya kung'atwa na mbwa mwishoni mwa mwaka jana nyumbani kwake.

Mpwa wa Kingunge, Tony Mwiru akizungumza na MCL Digital amesema familia inapitia kipindi kigumu kwa kuwa hivi karibuni wamempoteza mama yaom, Peras.

Enock Mwiru ambaye ni mdogo wa marehemu na mtangazaji wa zamani wa iliyokuwa Redio Tanzania (RTD), amesema Kingunge alikuwa kiunganishi cha familia.Mabalozi Juma Mwapachu na Ali Mchumo waliowahi kufanya kazi na Kingunge wamefika nyumbani kwa marehemu Kijitonyama kuhani msiba huo.

Mytake:

Kingunge hana dini. Sijui itakuwaje mazishi yake!
Atazikwa jinsi itakavyosemekana
 
Back
Top Bottom