Inasemekana huyu ndiye binadamu mzee kuliko wote duniani, Yupo Tanzania

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
505
871
18157237_765697656944665_904771553321385645_n.jpg

BINADAMU MWENYE UMRI MREFU ZAIDI DUNIANI ANAISHI TANZANIA.

Ndugu Ambilikile Mwanyaluke Panja Mkazi wa Kijiji cha Majengo Kata ya Ihanda ndiye Binadamu aliye na Umri mkubwa kuliko wanaodaiwa kushikilia Rekodi ya kula Chumvi nyingi Duniani kwa sasa.

Mzee Ambilikile Panja ambaye alishuhudia Vita kuu zote Mbili za Dunia kwa ukaribu, anakadiriwa kuwa na Umri wa zaidi ya miaka 127 leo.

Mkazi huyo wa Kitongoji cha Izyika ambaye kwa sasa haoni wala Kusikia vyema amemsimulia mwandishi wa makala haya kuwa wakati wa Vita ya Maji Maji dhidi ya Wakoloni alikuwa tayari anachunga mifugo ya Baba yake Marehem Mwanyaluke Panja.

Mzee Ambilikile Panja Kabila Mndali kutoka Tarafa ya Bundali Ileje anasema, Wakati wa Vita ya Maji Maji "Wazazi wetu walitwambia tukiona Wazungu tuiache mifugo tukimbie kurudi nyumbani" anasema Mzee Panja.

Mzee Panja ambaye kwa sasa hawezi kusimama wala kutembea anasema, Vita ya Kalenga (Mkwawa) haikuwahi kufika kwao Ileje, Isipokuwa Vita ya Pili ya Dunia ilifika mpaka Mbozi.

Anasema Vita ya Hitler, (Vita ya Pili ya Dunia) ilianza Wakati yeye akiwa ameshakimbia kutoka Ileje na kuhamia Mbozi (Kijiji cha Ihanda) baada ya Kupora Mke wa Chifu. Anasema yeye mwenyewe alishuhudia Mzungu aliyekuwa na Nywele mwili Mzima mithili ya Mnya akiwa amekimbia kujiokoa na Maadui zake. "Tulipo muona huyo Mzungu, tulidhani ni Mnyama kumbe ni Binadamu", anasema kwa Kindali huku akishusha Kicheko hafifu kilichofuatiwa na Kikohozi cha Ukongwe.

Mzee Ambilikile anasema Wakati wa Vita ya Hitler tulilazimika kuchimba Mashimo {Mahandaki} ya kujificha kuleee Lwibhaaa (Kitongoji cha Mlimani Kijiji cha Ihanda) <<Handaki hili lipo mpaka sasa eneo hilo.>>

Mzee Panja ambaye mtoto wake wa Kwanza Marehemu Leonard Panja alifariki dunia kutokana na Uzee, mwaka 2014 akiwa na Umri wa miaka 98 anasema Marafiki zake wote, pamoja na Maadui zake wakiwamo Machifu aliokuwa anapingana nao, wote wameshatangulia mbele za haki amebaki pekee yake.

"Mimi nilitoka Kapelekeshi nikaenda kuishi Ibungu Itumba na baadae nikahamia hapa Mbozi. Hapa nilikuja na Mke wangu Mkubwa Agnes Mlawa na Watoto wangu watatu Leonard, Lassary na Pitros pamoja na Zacharia Panja na marehemu Mbonasi Panja (watoto wa ndugu zake)"
anasimulia mzee Panja.

Mzee Ambilikile kwa sasa ni Kikongwe asiyeweza kufanya Chochote bila ya Msaada wa mtu mwingine. Mzee kwa sasa hubebwa au kusukumwa na Kiti cha Magurudumu (Wheel Chair) ambayo humsaidia kwa ajili ya kusogezwa eneo moja hadi jingine.

Kwa sasa Mzee huyu anaishi na Mke wake wa 4 Bi. Atusajigwe Mshani wa Mwisho katika wake zake ambaye naye kwa sasa ni mzee mwenye Umri wa miaka 89 licha ya Kuwa ana umri sawa na Mzaliwa wa tano wa Mzee Ambilikile Panja.

Aidha, kwa mujibu wa mtoto wa Mwisho wa Mzee Panja ambaye ndiye hutunza takwimu za familia ya Mzee Ambilikile, Ndugu Lawrence A. Panja; Baba yake anadhaniwa alizaliwa mwaka 1890 Katika Kijiji cha Kapelekeshi Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe.

Kikongwe huyu hajulikani popote zaidi ya Vijiji vinavyo mzunguka. Hata Serikali ya Wilaya tu haijui kuwa ina Raia wake mwenye Umri mkubwa namna hii.

Ni wajibu wetu kama Nchi kusaidia dunia kumfahamu Babu huyu mwenye Umri Mkubwa kuliko wengine. Ni jukumu la Wandishi na Vyombo mbalimbali pamoja na Mitandao ya Kijamii kuujulisha Ulimwengu Mtu huyu anayeishi maisha ya mwendo wa Marathon kwa sasa.

Sio kila siku tunafuatilia na kusimulia mambo ya Mataifa ya Nje wakati MUNGU na sisi katupendelea. Kama tumeweza kuuambia ulimwengu Mlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania na sio Kenya basi na hili tunaweza tukiamua.

Mwisho naomba Viongozi wa Serikali, Siasa, Dini Mashirika ndani na nje ya Nchi, pamoja na Wananchi mbalimbali kujitolea kumsaidia na kumtunza Mzee Panja ambaye kwa Umri wake ni kama Lulu iliyosalia Duniani kwa sasa.

Mwandishi wa Makala hii ni Ndugu Abel Sichembe

Email abelchembe37@gmail.com

Simu No. +255757281046

WhatsApp No. +255655281046

Share, Like, Coment, Re post, Sambaza mpaka iwafikie Guineas World of Record.
 
Sasa kama ulienda kuchukua habari za huyo mzee hujaweka hapa picha tutaamini vipi ?.

Unaleta habari za miaka ya 1606 pasipo hata picha
 
IMG-20170427-WA0001.jpg
huyu ndio mzee panja anaesadikika kuwa na umri mkubwa zaidi duniani.
 
kkakakakakakakakkakaaa.png

Utakuwa umesikia rekodi ya binadamu mzee zaidi duniani ambaye anatokea katika nchi ya Jamaica Bi. Vailet Brown ambaye amezaliwa March 10, 1900 ambapo kwa sasa ana umri wa miaka 117 huku mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 97.

Ayo TV na millardayo.com inakuletea rekodi mpya kutoka Tanzania – nayo ni kuhusu mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani ambaye anaishi Mkoa mpya wa Songwe katika Wilaya ya Mbozi, Kata ya Ihanda, Kijiji cha Majengo.

Kutoka huko nakuletea Ambilikile Panja ambaye anakadiriwa kuwazaliwa mwaka 1890 ambapo kwa mwaka 2017 atakuwa ametimiza miaka 127 na kumzidi mtu anayetambuliwa na Guinness Book of World Records Vailet Brown kwa miaka 10.

VIDEO: Binadamu mzee zaidi duniani anayepatikana Tanzania - millardayo.com
 
vijini ambako vyombo vya habari havifiki, kuna wazee zaidi Ya huyo. namwona Kama bado .ila hongera zake amekula chumvi vya kutosha
 
tatizo la wazee wetu vigumu kuingizwa kwenye world recods ni sababu hawajui exactly umri wao, wengi wanafanya makadilio kwahiyo ni ngumu kuushawishi ulimwengu
 
Back
Top Bottom