Inasemekana Azam na Yanga nazo zina wagonjwa wa "mafua makali"

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,933
25,268
Habari zinazozunguka mtandaoni kwa sasa zinasema kuwa klabu ya Yanga na Azam zina wagonjwa wa mafua makali na homa ambapo zinaweza kupelekea wachezaji hao kukosa mechi za ligi kuu zinazowakabili.

Kocha wa Yanga,Nasreddine Nabi amesema kuwa kuna wachezaji wagonjwa klabuni hapo kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya Tanzania Prisons kwenye dimba la Nelson Mandela.

Pia kocha huyo ametoa pole kwa kikosi cha Simba ambacho kimetangaza kuwa na wagonjwa 16.

Inasemekana Klabu ya Azam ina wachezaji watatu ambao wamekumbwa na ugonjwa huo wa mafua makali. Habari hizi zinakuja wakati Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania chini ya miaka 20 (Tanzanite) ipo nchini Burundi ikiwa na wachezaji 8 tu, baada ya wengine kubainika kuugua UVIKO19. Katika mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia uliochezwa Dar es Salaam, Tanzanite ilishinda 3-2.
 
Simba ni Posho na Mishahara na si ugonjwa kama taarifa ya wataalamu ilivyosema.

Kumbe Yanga nao Mishahara na Posho. Hakika hakuna Msemaji Fala kama yule, yaani analeta ujinga hata kwenye maswala mazima ya afya.
Wataakam wa Michongo
 
Back
Top Bottom