Inaruhusiwa kusafirisha mtungi mtupu wa gesi kwenye gari ya abiria?

Mamylicious

Senior Member
Apr 22, 2017
110
100
Naomba kujua Kama inawezekana kusafirisha mtungi mtupu wa gesi kwenye gari ya abiria.Nataka kuutoa Arusha kuupeleka Tanga.
 
Mm nilisasafirisha toka Mwanza to Dar ukiwa na Gas, niliweka kwenye Diaba na nikaweka na vyombo juu hivyo ukafka japo ni hatari sana!
 
Inakatazwa sana na hairuhusiwi kwa mujibu wa sheria za barabarani
Nakumbuka December nlkua nahama kutoka dar kuja mbeya mtungi wangu ulishushwa palepale ubungo ila faster nikajiongeza nikauweka kwenye box af juu nikaweka sufuria nikasafirisha kwenye gari tofauti nliwadanganya kuwa ni vyombo vya ndani walivoona sufuria wakajaa
 
Fanya lakini kwa kuvunja sheria, hata kama ni mtupu hairuhusiwi. La kufanya usafirishe kwa siri au afikiana na wenye gari, mfn Kondo, tarehe 4/12/2016 nilisafirisha mtungi mdogo empty from Kilimanjaro to Bukoba, nilikamatiwa bukoba stend. It was very bad, nilitumia nguvu ya mshua la sivyo na ningepigwa faini kubwa
 
Hairuhusiwi kabisa kisheria.

Mwaka jana mwezi wa 10 nilisafirisha kutoka KLM kuja DSM. Ulikuwa mtupu. Konda na Dereva walinikatalia lakini nililazimisha wakanipa tahadhari kuwa wakikamatwa faini nalipa mimi. Nikaitikia poa.

Njiani siku hiyo kulikuwa na Ukaguzi mzito. Mtungi wangu ukaonekana, gari ikaamuliwa iwekwe pembeni. Konda akaja kunichomoa fasta eti nimewatishia lazima wasafirishe. Nililiwa 60,000 lakini nilifika nao fresh.
 
Inakatazwa sana na hairuhusiwi kwa mujibu wa sheria za barabarani
Nakumbuka December nlkua nahama kutoka dar kuja mbeya mtungi wangu ulishushwa palepale ubungo ila faster nikajiongeza nikauweka kwenye box af juu nikaweka sufuria nikasafirisha kwenye gari tofauti nliwadanganya kuwa ni vyombo vya ndani walivoona sufuria wakajaa
Duh itabidi nitafute namna ya kuusafirisha maana usawa huu kwenda kununua mwingine ni tatizo
 
Hairuhusiwi kabisa kisheria.

Mwaka jana mwezi wa 10 nilisafirisha kutoka KLM kuja DSM. Ulikuwa mtupu. Konda na Dereva walinikatalia lakini nililazimisha wakanipa tahadhari kuwa wakikamatwa faini nalipa mimi. Nikaitikia poa.

Njiani siku hiyo kulikuwa na Ukaguzi mzito. Mtungi wangu ukaonekana, gari ikaamuliwa iwekwe pembeni. Konda akaja kunichomoa fasta eti nimewatishia lazima wasafirishe. Nililiwa 60,000 lakini nilifika nao fresh.
Nitaongea na konda nione ananisaidiaje?
 
Back
Top Bottom