Inapendeza milioni 900 ya Dr. Shika ni funzo kwetu

Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,456
614
Pamoja na ukweli kuwa zoezi zima la mnada wa nyumba za Rugumi limegeuka kuwa ni kichekesho pengine cha kumaliza mwaka, kwangu mimi kuna fundisho kubwa. Kwenye mambo mengi watanzania tumekuwa tunajikita sana kutaka kuona matokeo na hatuna muda wa kujiridhisha na mchakato wa kupata matokeo yenye tija. Hili linatugharimu sana kwenye mambo mengi ya kiuchumi na medani za kisiasa.

Hatuna muda wa kujiridhisha, tumekuwa tukiamini au hata kuchagua watu bila hata kujiuliza au kuwafahamu watu vizuri. Kwenye hili la Dk. Shika limenishangaza sana kuwa kumbe mtu yeyote anaweza kwenda kwenye mnada bila ya kuwepo na utaratibu wowote wa kumtambua mtu uwezo wake, historia yake au hata uraia wake. Wapiga mnada wale inavyoelekea walijikita ktk kutimiza majukumu yao ambayo ni kuuza ili wapate mgao wao. Hawakuwa na muda wakuhakiki wateja wao. Kama sheria haipo nafikiri ni wakati sasa wa kuwepo na utaratibu wa kutambuana mapema ili utani ule usijirudie. Kwa mwonekano wa nje wa Dk. Shika kama umakini ungekuwepo, sidhani kama Yono wangeingizwa mkenge kirahisi vile bila kushtuka. Ukiachilia mbali mambo ya Dk. Shika Watanzania kwa miaka hii ni muhimu sana kuwa makini sana na watu au wanasiasa ambao wanakila dalili za kufilisika kisera na kiuwezo lakini tumekuwa watu wa ushabiki na kuwaamini, baadae tumekuwa watu wakulaumu na kukejeli. Wenye matatizo sio Wakina Dk. Shika bali ni sisi tunao waamini na kuingizwa mkenge.
 
900 itapendeza zaid alijitambulisha kama mkurungenz wa shirika la kutengeneza kemikali huko moscows urus kwa putin

Kingine huwez kumdharau mtu kwa muonekano wake

Yono walikuwa sawa wala usiwalaum kiongoz
 
Dr. Shika amekuwa mtamu Sana mitandaoni ! Ha ha ha ha ! Tanzania Kuna Mambo kweli kweli!
 
DOb21DfXkAEhM5f.jpg
DOb27sLXcAEnc8q.jpg
 
Pamoja na ukweli kuwa zoezi zima la mnada wa nyumba za Rugumi limegeuka kuwa ni kichekesho pengine cha kumaliza mwaka, kwangu mimi kuna fundisho kubwa. Kwenye mambo mengi watanzania tumekuwa tunajikita sana kutaka kuona matokeo na hatuna muda wa kujiridhisha na mchakato wa kupata matokeo yenye tija. Hili linatugharimu sana kwenye mambo mengi ya kiuchumi na medani za kisiasa.

Hatuna muda wa kujiridhisha, tumekuwa tukiamini au hata kuchagua watu bila hata kujiuliza au kuwafahamu watu vizuri. Kwenye hili la Dk. Shika limenishangaza sana kuwa kumbe mtu yeyote anaweza kwenda kwenye mnada bila ya kuwepo na utaratibu wowote wa kumtambua mtu uwezo wake, historia yake au hata uraia wake. Wapiga mnada wale inavyoelekea walijikita ktk kutimiza majukumu yao ambayo ni kuuza ili wapate mgao wao. Hawakuwa na muda wakuhakiki wateja wao. Kama sheria haipo nafikiri ni wakati sasa wa kuwepo na utaratibu wa kutambuana mapema ili utani ule usijirudie. Kwa mwonekano wa nje wa Dk. Shika kama umakini ungekuwepo, sidhani kama Yono wangeingizwa mkenge kirahisi vile bila kushtuka. Ukiachilia mbali mambo ya Dk. Shika Watanzania kwa miaka hii ni muhimu sana kuwa makini sana na watu au wanasiasa ambao wanakila dalili za kufilisika kisera na kiuwezo lakini tumekuwa watu wa ushabiki na kuwaamini, baadae tumekuwa watu wakulaumu na kukejeli. Wenye matatizo sio Wakina Dk. Shika bali ni sisi tunao waamini na kuingizwa mkenge.
Watu wanajifunza kutokana na makosa....so keep it low

inawezekana katika minada kumi ulioharibika ni huo

mmoja.....
 
Back
Top Bottom