James Martin
JF-Expert Member
- Apr 2, 2016
- 1,206
- 1,509
Tangu mwaka jana nimekuwa nikimsikiliza mfanyabiashara Ramadhani Ntunzwe anavyosumbuliwa bila kupata ufumbuzi.
Nina imani kabisa rais wa wakati huo kama kweli alikuwa na nia ya kumaliza jambo hilo lisingechukua muda mrefu kiasi hiki.
Pia nadiriki kusema mateso aliyoyapata huyu mfanyabiashara yalikuwa na baraka zote za mkuu wa nchi wa wakati huo. Mteule wake Sabaya alikuwa akitaka pesa kwa nguvu kutoka kwa wafanyabiashara, siamini kama Rais alikuwa hajui.
Kwa uchambuzi wangu nafikiri aliyekuwa rais wakati huo alitoa "maagizo" huyu bwana atatuliwe matatizo yake kama geresha.
Hao watu wa wizara ya fedha kufanya naye kikao kama kumzuga tu na Rais lazima alikuwa sehemu ya mkakati huo.
Kama bwana Ramadhani atakuwa anausoma uzi huu, watu wa wizara ya fedha hawakukuita kutatua tatizo bali ni kukulagai tu.
Sababu ya kwanza Rais kutoa "maagizo" ni kwamba huyu mfanyabiashara alipaza sauti kubwa kupitia vyombo vya habari. Ilibidi Rais ajifanye anamsaidia ili kujitoa lawama.
Sababu ya pili ambayo ni kubwa ni uchaguzi ulikuwa umekaribia. Kujifanya wanamsaidia huyu bwana ilikuwa ni njia ya kumnyamazisha kwenye kipindi cha uchaguzi. Wapinzani wangeweza kuitumia kesi ya huyu bwana kuipaka matope serikali ya awamu ta tano.
Kama kweli Wizara ya Fedha ilikuwa inataka kumsaidia bwana Ramadhan Ntunzwe ilikuwa na uwezo wa kufanya uchunguzi wake wa haraka kama wao wenyewe kuwasiliana na mahakama kujua kama kesi ilifunguliwa, kuhakiki stakabadhi za TRA, kuwasiliana na polisi n.k. Nchi za dunia ya kwanza wanaita multi agency cooperation.
Hivi vyombo vyote vingeweza kufanya kazi kwa pamoja kutatua hili tatizo kwa haraka bila kumlaghai huyu bwana kwa kumsumbua aende kwenye "mikutano"