Inaonekana kila wizi mkubwa wa mali ya umma upo mkono wa serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inaonekana kila wizi mkubwa wa mali ya umma upo mkono wa serikali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Byendangwero, Sep 11, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Katika hali halisi serikali ndiyo yenye dhamana ya kulinda mali ya umma.

  Mali hiyo ya umma siyo ya viongozi wa serikali bali ni ya watanzania wote. Katika miaka ya hivi karibuni kumezuka mtindo wa wale walioko madarakani kujiamria wao wenyewe kujigawia mali ya umma kama kwamba ni ya kwao binafsi. Na hivyo tumeshuhudia wakati wa awamu ya pili viongozi waandamizi serikalini wakijiuzia nyumba za serikali kwa bei ya kutupwa.

  Mbali ya hayo kumekuwepo matukio mengi ya wizi wa mali za umma k.m EPA, meremeta, Tangold, Rada n.k. Jambo la kushangaza badala ya serikali kuonyesha umakini katika kushughulikia masuala hayo imekua ikitumia nguvu nyingi kuzima ukweli husijitokeze! Wadadisi wa mambo wanasema hii inatokana na baadhi ya viongozi wa juu serikalini kuhusika moja kwa moja katika sakata hizo.

  Swali la kujiuliza ni je kama mikono ya serikali ya kuhifadhi mali ya umma hivi sasa imefungwa, nani mwenye dhamana ya kuhifadhi mali hizo?
   
 2. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2011
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kuiweka hii sawa ni viongozi wa awamu ya tatu (BWM) ndio waliojipa nyumba za serikali na sio awamu ya pili kama ulivyoandika kwani awamu ya pili ilikuwa ni ya mzee ruksa (Baba yake Hussein Mwinyi).
   
Loading...