Rais Magufuli: Watanzania kuamini kila kitu cha kwenye mtandao ni kutokana na sisi kutoi-control mitandao

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,396
Rais Magufuli leo akiwaapisha Majaji 10 aliowateua pamoja na Mawakili amesema kuwa Watanzania tunaamini kila kinachoandikwa kwenye mitandao ya kijamii. Hii inatokana na kutoku-control mitandao hiyo wamiliki wako huko wao interest yao ni kutengeneza biashara wala hawajali consequences zitakazotokea

> Rais Magufuli ameongeza kuwa hadhani kama ukienda kwenye nchi kama China utakuta wana 'Google' na 'WhatsApp' kama hizi za kwetu huku

> Rais Magufuli: Kila Mtu anapojifikiria anapost chochote kwenye mitandao ya kijamii

Rais ameelezea tabia ya kuamini mijadala ya mitandaoni kama ugonjwa ambao hafahamu umetoka wapi. Ameeleza kuwa siku moja alikua akisoma mtandaoni kuhusu serikali kuiba Trilioni 1.5 ikabidi ampigie CAG kuuliza kuhusu wizi huo

======
Ikumbukwe kuwa mnamo Septemba 28 mwaka 2016 Rais Magufuli alinukuliwa akisema kuwa ''Anatamani Malaika washuke wazime mitandao ya kijamii, irudi baada ya mwaka 1 ikute hatua kubwa za kimaendeleo tulizopiga''
 
Attachments

  • Rais Magufuli.mp4
    4.6 MB · Views: 84
Si dalili nzuri hiyo!

Lakini hilo ni suala la ujinga na upumbavu wa mtu kuliko udhibiti wa hiyo mitandao.

Mimi naamini katika uhuru na haki ya watu kuwa wajinga na wapumbavu.

Hivyo waachwe tu wawe wanavyotaka wao. Waamini watakacho. Imani yao kama siyo ndo uhalisia wenyewe haitobadili chochote.
 
Kwenye ripoti yake, CAG hajasema popote kuwa TZS 1.5trn zimeibiwa. Alichosema leo Ikulu ndio msimamo wake uliopo kwenye Taarifa yake ukurasa wa 34. Fedha hizo HAZIONEKANI kwenye matumizi ya Serikali ya mwaka 2016/17.

Ndio maana tunahoji zipo wapi. Tunataka Ukaguzi Maalumu ili kuhakiki majibu ya Serikali na kujua hela zetu zipo wapi. Hilo tu, hakuna lingine.

Vitisho vya hatua za kisheria ni tambo tu za watawala, hazina maana yeyote. Kumsimamisha CAG Ikulu na kumhoji mbele ya Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ni kumtisha CAG, ni kinyume na misingi ya Katiba yetu. Ripoti ya CAG ikishakuwa mbele ya Bunge sio Ripoti ya Executive tena. Ni mali ya Bunge. Kama Rais ana majibu aende akayaseme Bungeni mbele ya PAC.

Rais sio wa kumchekea chekea anapovunja misingi ya nchi yetu. Ni lazima ADHIBITIWE na Taasisi za Kikatiba ikiwemo Bunge. Rais leo amekosea. CAG naye amekosea kwenda Ikulu.

Watanzania sikilizeni, mimi nimekuwa Mwenyekiti wa PAC/POAC miaka 8, ninajua kusoma, kuchambua na kutafsiri Taarifa ya CAG. TZS 1.5trn hazina maelezo, hazipo Benki Kuu na Maelezo ya Naibu Waziri Fedha leo ni kujikosha tu.

Nikiwa Mwenyekiti wa PAC, Mwaka 2013 Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli alikutwa na Hoja ya ukaguzi ya TZS 252 bilioni ya ujenzi wa barabara hewa ambayo mpaka sasa haijajibiwa na utaikuta kwenye Hoja za CAG za mwaka 2016/17. Hivyo ni Kawaida yake kutoheshimu sheria za Fedha na kutojibu Hoja za Ukaguzi.

Kama Serikali ina uhakika kabisa hii hoja ya TZS 1.5trn haipo inipeleke mahakamani hata leo. Nitawashinda hata Jaji akiwa mmoja wa majaji wapya walioapishwa leo.

Mimi siogopi. Nitasema UKWELI daima fitina kwangu mwiko.

Zipo wapi TZS 1.5trn?

Zito kabwe
 
Mitandao ni swala geni hapa kwetu na nchi nyingine, laiti kama kungekuwa na elimu kama ilivyo elimu ya hesabu na sayansi mashuleni, watu wangejuwa matimizi stahiki ya mitandao.
Matumizi stahiki ni kama haya kuwatambua mijizi
Kwani wanaposema social media wewe unaelewa nini?
Trump ana tweet kila siku yahusuyo serikali yake sasa cha ajabu nini Waafrica kufanya haya
Trillion zinawatoa ufahamu kutetea majizi
Mitandao si swala geni linakwenda sambasamba ulimwenguni kote acheni kuwabeza WaTz
 
Yaani una post maneno ya Zitto kama umeandika wewe. Sio fair. Weka source vinginevyo ni uhuni wa kiuandishi.
 
Watanzania wenzangu,

Hakuna uongo kuhusu udikteta wake, ukwapuzi wa nyumba za Serikali, ukwapuzi wa bilioni 16 za wahanga wa tetemeko, ununuzi wa kivuko uozo, kuchota trillions hazina bila idhini ya Bunge, ubaguzi wake wa kutisha etc.

Rais Magufuli leo akiwaapisha Majaji 10 aliowateua pamoja na Mawakili amesema kuwa Watanzania tunaamini kila kinachoandikwa kwenye mitandao ya kijamii. Hii inatokana na kutoku-control mitandao hiyo wamiliki wako huko wao interest yao ni kutengeneza biashara wala hawajali consequences zitakazotokea

> Rais Magufuli ameongeza kuwa hadhani kama ukienda kwenye nchi kama China utakuta wana 'Google' na 'WhatsApp' kama hizi za kwetu huku

> Rais Magufuli: Kila Mtu anapojifikiria anapost chochote kwenye mitandao ya kijamii

Rais ameelezea tabia ya kuamini mijadala ya mitandaoni kama ugonjwa ambao hafahamu umetoka wapi. Ameeleza kuwa siku moja alikua akisoma mtandaoni kuhusu serikali kuiba Trilioni 1.5 ikabidi ampigie CAG kuuliza kuhusu wizi huo

======
Ikumbukwe kuwa mnamo Septemba 28 mwaka 2016 Rais Magufulia alinukuliwa akisema kuwa ''Anatamani Malaika washuke wazime mitandao ya kijamii, irudi baada ya mwaka 1 ikute hatua kubwa za kimaendeleo tulizopiga''
 
Matumizi stahiki ni kama haya kuwatambua mijizi
Kwani wanaposema social media wewe unaelewa nini?
Trump ana tweet kila siku yahusuyo serikali yake sasa cha ajabu nini Waafrica kufanya haya
Trillion zinawatoa ufahamu kutetea majizi
Mitandao si swala geni linakwenda sambasamba ulimwenguni kote acheni kuwabeza WaTz

Mimi sikatai umuhinu wa mitandao ya kijamii, lakini je ni wangapi wanajuwa kupanga na kupanguwa kilicho kwenye hiyo mitandao? hata huyo Trump mwenyewe, mara ngapi anadika vya uwongo na baadhi ya watu wanaamini. Kuna kijana mmarekani alianika mwili wa mjapani aliye jingonga bila kujali madhara ya hizo picha kwa wanadugu wa marehemu, Je kwako wewe huo ndio matumizi stahiki ya mitandao. Hata kama watu wanataka kuibuwa wizi Je aliye andika kama kadanganya na nchi ikavurugika kwenu hili ni jambo jema?
 
Ukitaka kula vizuri na kipofu na ufaidi usimshike mkono we cheza na timing za movement za mikono yake. Akichukua tonge wewe unachukua paja, mwisho wa siku kiroho safi anaridhika kumbe kihalisia umempunja.

Sirikali yetu haijui maana ya hii kitu.
 
Mitandao ni swala geni hapa kwetu na nchi nyingine, laiti kama kungekuwa na elimu kama ilivyo elimu ya hesabu na sayansi mashuleni, watu wangejuwa matimizi stahiki ya mitandao.

..uzuri wa mitandao ya kijamii ni UHURU wa kutoa mawazo.

..kuna kipindi Magufuli alikuwa anakubalika sana ktk mitandao ya kijamii.

..kukubalika huko kunaelekea kupungua sasa hivi.

..sasa anachotakiwa kukifanya ni kujisaili kuelewa ni wapi amepungukiwa na kupafanyia marekebisho.

..hatakiwi kuichukulia mitandao ya kijamii kama MAADUI, WAHUJUMU, au WASALITI.

..badala yake aichukulie mitandao kama TOCHI inayomulika maeneo yanayohitaji marekebisho kutoka kwa watawala.
 
Mimi sikatai umuhinu wa mitandao ya kijamii, lakini je ni wangapi wanajuwa kupanga na kupanguwa kilicho kwenye hiyo mitandao? hata huyo Trump mwenyewe, mara ngapi anadika vya uwongo na baadhi ya watu wanaamini. Kuna kijana mmarekani alianika mwili wa mjapani aliye jingonga bila kujali madhara ya hizo picha kwa wanadugu wa marehemu, Je kwako wewe huo ndio matumizi stahiki ya mitandao. Hata kama watu wanataka kuibuwa wizi Je aliye andika kama kadanganya na nchi ikavurugika kwenu hili ni jambo jema?
Kwa nini umetolea mfano wa marehemu na sio mfano wa hili lililopo mbele yetu
Hii ni pesa ingemtiba baba yako bibi yako mke wako watoto wako tungeweza kuwa na shule bora (zifundishe hiyo elimu uliyotaja)Tunapozungumzia upotevu wa pesa ya Mtz maskini mkulima mvuja jasho wakati wengine wanazifuja kwa kujenga nyumba za kifahari Mwanza Chattle na kwingineko wakati vijijini watu wanateseka please msije hapa kuwabeza WaTz eti hawajui matumizi ya mitandao.
Trump ni mfano tu nimekupa sasa wewe utakuwa unajua social media kuliko mzungu mwenyewe aliyeileta
Wewe kazana kusoma Uhuru na Mzalendo tupishe sisi na social media zetu
Mnawaziba watu midomo kwa maovu yenu
Hii dhambi mtailipa even 50 years down the road kama hutailipa wewe atalipa mwanao au mjukuu wako au kitu kuu chako
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom