Inakwaza sana mtu anakupiga picha bila idhini yako halafu anakutandaza chini ukalipie

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,597
2,000
hili jambo limekuwa likinikera sana. ni utaratibu wa hovyo sana kuwah kutokea kwenye sherehe na mikutano mbalimbali. wewe huna hili wala lile umemaliza sherehe au mkutano unatoka nje unakuta picha chini zimesambazwa na wewe upo na ukichukulia hukuomba upigwe picha. na jamaa bila aibu anakwambia hiyo picha umpe tsh 4000.

we ulijuaje kama mimi nina hela? haya mambo ni kuharibiana siku. mi siku moja nipo na demu mkali sana kwenye sherehe alinisindikiza kumbe mpiga picha kila akizunguka anarudi kwenye meza yetu anagonga picha. anaenda tena akirudi anagonga picha. mwishoni tumemaliza tunatoka akanishika bega. "bro picha zako hizi hapa"... nlimuuliza picha gani.(maana akili lishtuka nikadhani ni za utupu zimevuja) akanijibu huku akikenua meno yake "hizi umepiga na mrembo hapa" astaghafilulah zilikuwa picha 17 katika hizo kuna za tsh 4000 na nyingine 2000 . yule dada kwa ujinga kabisa anafurahia kutaka kuzikusanya.

nlimwambia tu afanye haraka alipie tuondoke mi nimechoka.yule dada akashtuka kuwa hakubeba pesa alibeba pochi tu. then nikamgeukia mpiga picha kuwa achane picha zangu pale pale au nizichane mwenyewe. maana mimi sitaki zibaki kwake na wala silipi pesa ya kuzichukua.kiukweli nliziachana zile picha na yule dada naye nlimwambia kama ningetaka picha ningemwita mpiga picha aje apige picha.so nikampandisha kwenye gari and we left.

hii biashara ya kupiga picha bila concern ya mtu si nzuri na inakwaza sana. wewe hujui mi nimekujaje kwenye party.sometime mtu unaweza kuwa ulilipiwa kadi so ukatafuta tu nauli uje ushereheke. then mtu mmoja anaamua kuku photoa bila kukushirikisha. kama vile haitoshi anaenda kukulaza chini...anakutandaza na unaweza hata kanyagwa. haya mambo ni ya ajabu na yanaleta hasira sana. sasa nasema ole wenu ninyi wapiga picha.ukinipiga picha utanilipa picha yangu kuiweka kuwa ya maonesho. otherwise nipe bure niondoke nayo au basi ichane tu ila usidhani utabaki na picha yangu.
 
chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
2,932

pesa ya kulazimisha.huo mchezo hupo kwenye vipaimara sana
 
Daudi1

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
6,842
2,000
Naunga mkono hoja Mimi huwa naziacha maana nakuwa sijamuomba
 
Wajad

JF-Expert Member
Jul 20, 2012
1,321
2,000
Wengi wanaamua kuzichukua kwasababu wanaogopa wakiziacha zinaweza kuangukia mikononi mwa watu wabaya wakazifanyia mchezo mchafu. Kwa mfano wewe hapo ulikuwa na mchepuko, mtu mwingine anaweza kuzinunua hizo picha na kuzipeleka kwa mkeo au kuzipost mitandaoni.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom